Karibuni ADC kwa wote waliochoshwa na ufisadi wa CCM na CCM 'B' na ubabe wa CHADEMA

ADC - DIRA YA MABADILIKO ADC - TUMAINI LA MTANZANIA

Madhumuni yetu ni:

1. Kushika Dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
2. Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa Watanzania wote.
3. Kujenga Uchumi Imara na kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania wote.
4. Kupinga kwa nguvu zote aina zote za ubaguzi na ukandamizaji.
5. Kuheshimu mikataba ya kimataifa inayohusu haki halisi za binadamu.

ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.

Hiki chama chako mbona kimeanza vibaya? Yaani unaanza kwa kuvikandia vyama vyenzio vya upinzani? Hapa kazi ipo!!!

Tiba
 
Sidhani kama ni tatizo kutumia kiingereza katika jina la chama kwani ni lugha official hapa nchini Tanzania. Mashuleni inatumika kufundishia na maofisini pia. Plus Uhuru wetu tuliukwaa kutoka kwa haohao Waingereza.
Hoja kuhusu Upandikizi na kwamba Uzuri wa Chadema sio kila mtu anaukubali na ndio maana hasa ya demokrasia. Lakini pia huko kuungana nadhani chadema ndio wa mwanzo kupinga muunganiko huo. Tumeona baada ya kuukwaa Ukuu wa Upinzani Bungeni hawajataka kushirikiana na chama chochote cha Upinzani.

Mkuu Chadema hawataki ushirikiano na vyama vingine kwa sababu vingi ya vyama vilivyosajiliwa ni CCM B. Utakuwa na akili timamu ushirikiane na chama kama CUF ambacho tayari ni CCM B?

Acha utani bwana!!!!!!

Tiba
 
Hiki chama chako mbona kimeanza vibaya? Yaani unaanza kwa kuvikandia vyama vyenzio vya upinzani? Hapa kazi ipo!!!

Tiba

NARUDIA TENA
Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema:
Haki ya Uhuru na Mawazo:
18. Kila Mtu-
(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

Kifungu kimeafikiwa?
 
Uhakiki unaendelea....mambo ya Mara haya kwa kina Mtatiro yule wa Cuf na the late Chacha Wangwe (May God rest his soul in ertenal peace).
View attachment 59355 19[1].jpg 24[1].jpg
 
Haijataja pumba wala no research no right to speak, ila imesema tu kwamba 18. Kila mtu (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake. (b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi. Sasaa sijaona sehemu waliyoandika Pumba No Reseach No..... Usiwe kama hilo jina lako kiongozi, Nijuavyo mimi Fungo ni kijimnyama fulani hv. Kipo kipo tuu. ok! Aliyekuita hvyo hajakosea.

madrasa inakutesa wewe ndo maana hata kifungu cha uhuru wa kuabudu mkatumbukiza mahakama ya kadhi kaz mnayo vlaza nyinyi?
 
kwa aina hii ya coment unanipa mashaka kidogo kujua nani akili zake zinafanya kazi vizuri na nani zinamtindio kwa kweli. Nimeona nikushike hapo kwny blue tu kuweza kukujuza ni namna gani kauwezo kako kalivyo kadogo kwenye kukokotoa mambo especially haya ya kisiasa.

Mfano mdogo tu ninaoweza kukupa kuhusiana na siasa na muda ni kwa majirani zetu tu wa hapo KENYA. PNU ie: Party of National Unit kilianzishwa rasmi tar. 16-sept-2007 na mwaka huohuo mwezi Dec 2007 wakasimamisha Mgombea wa RAISI ambaye ndie still President of the so called 'Republic of Kenya'
Imekaa vipi hii?

Hiyo bluu iko mapi Fisadigamba!
 
Samaki wana nafuu labda kama hata dagaa ni samaki pia!!

ADC; another surrogate son of CCM?!

hawa ni mijusi hata dagaa nako ni kuwapendelea,

si unajua mjusi hutingisha mkia naye hujiona kama vile ni kenge?!
 
NARUDIA TENA
Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema:
Haki ya Uhuru na Mawazo:
18. Kila Mtu-
(a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake;

Kifungu kimeafikiwa?

nadhani unajishangaa mwenyew upo peke yako hapa,
 
Adc chama cha wagonjwa wa fikra kiko kwa maslahi ya ruzuku hata aibu hakina hawooooo.....!
 
madrasa inakutesa wewe ndo maana hata kifungu cha uhuru wa kuabudu mkatumbukiza mahakama ya kadhi kaz mnayo vlaza nyinyi?

Katiba yetu hiihii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sehemu ya tatu inayohusu Haki na Wajibu Muhimu....ibara ya 19(1) Kila mtu anastahilikuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu kubadilisha dini au imani yake.
Sasa Mtanganyika mwenzangu FUNGO jr. hiyo madrasa na mahakama ya KADHI VIMETOKEA WAPI? Sehemu gani nimeonyesha kuwa nimeegema katika dini ya kiislamu? Una hakika gani kwamba kweli mimi ni Muislamu? HILO JINA? AU NAWE ndio walewale wa kufuata mkumbo?
Sehemu hiihii ya tatu Ibara ya 15(1) inasema: Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru. 'Tafadhali usiutumie uhuru wako wowote ule vibaya. aidha Uhuru wa kuishi ama kutoa mawazo, japo ni kweli kikatiba una uhuru wa kufanya hivyo. Ndio zileee pumba na No research No Right to speak zako zinaweza kuingia hapo.
Mwisho namnukuu Makamu wa Kwanza wa Rais ZNZ....Mhe. Maalim Seif Sharif 'SAWASAWAAAAA?' Naamini umenipata vizuri.
 
Jina la chama linasadifu ukoloni wa mawazo. Jina la chama kwa Kiingereza. Chama hiki ni cha Tanzania au cha Waingereza? Sipendi sana watu wasiopenda kushirikiana na wenzao. Kuna vyama vingi sana hapa nchini je mmeona hakuna hata kimoja mnachoweza kushirikiana nao? Hii ndiyo maana naweza kusema mnatumika kuvuruga vyama. Ni kitu gani kitakacho nishawishi nisisema kwamba nyinyi ni chama pandikizi? Kama Chadema inafanya vizuri kabisa na bado hamwezi kushirikiana nao si mnataka kugawa kura ili CCM iendelee kutawala? Acheni ubinafsi.
mafala ndo watajiunga huko
 
Ofisi zenu hapa ruvuma ziko sehemu gani?

Tumewasikia tutawafikia.......Kwa kuanzia tu ni kwamba tuna wanachama wetu Tunduru na Songea mjini ambao mara tu baada ya usajili wakudumu tutawawezesha na utaona mambo yetu. Ofisi zitakuwepo na mambo yatafunguka tu. Karibu ADC.
 
Back
Top Bottom