Karibuni ADC kwa wote waliochoshwa na ufisadi wa CCM na CCM 'B' na ubabe wa CHADEMA

hasan124

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
716
128
ADC - DIRA YA MABADILIKO ADC - TUMAINI LA MTANZANIA

Madhumuni yetu ni:

1. Kushika Dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
2. Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa Watanzania wote.
3. Kujenga Uchumi Imara na kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania wote.
4. Kupinga kwa nguvu zote aina zote za ubaguzi na ukandamizaji.
5. Kuheshimu mikataba ya kimataifa inayohusu haki halisi za binadamu.

ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.
 
Nadhani ulipaswa kwanza kuwakaribisha CCJ alafu cck na kisha ADC na sasa chauma.kuanzisha chama cha siasa ni ngumu sana hivyo walioweza kuanzisha adc na hivyo vyama vingine wanastahili pongezi.

Lakini kuna jambo moja la kweli japo halita kuipendeza wewe na wengine wasiopenda kufikiri kama wewe na hilo ni kuwa kuendesha chama cha siasa cha upinzani kwa mafanikio kama ya NCCR Mageuzi na zaidi leo cdm si kazi nyepesi.

Waulize au tazama(kama una uwezo)muda na nguvu walizotumia cdm kujijenga na kufika hapo walipo.ukishapata majibu sahihi(kama akili zako zitafanya kazi vizuri)ndio utakuwa katika katika nafasi nzuri ya kuipokea ADC.
 
ADC - DIRA YA MABADILIKO ADC - TUMAINI LA MTANZANIA

Madhumuni yetu ni:

1. Kushika Dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
2. Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa Watanzania wote.
3. Kujenga Uchumi Imara na kulinda rasilimali za nchi kwa manufaa ya watanzania wote.
4. Kupinga kwa nguvu zote aina zote za ubaguzi na ukandamizaji.
5. Kuheshimu mikataba ya kimataifa inayohusu haki halisi za binadamu.

ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.

hata samaki nao wana ndoto zao,
 
nadhani ulipaswa kwanza kuwakaribisha ccj alafu cck na kisha adc na sasa chauma.kuanzisha chama cha siasa ni ngumu sana hivyo walioweza kuanzisha adc na hivyo vyama vingine wanastahili pongezi.lakini kuna jambo moja la kweli japo halita kuipendeza wewe na wengine wasiopenda kufikiri kama wewe na hilo ni kuwa kuendesha chama cha siasa cha upinzani kwa mafanikio kama ya nccr mageuzi na zaidi leo cdm si kazi nyepesi.waulize au tazama(kama una uwezo)muda na nguvu walizotumia cdm kujijenga na kufika hapo walipo.ukishapata majibu sahihi(kama akili zako zitafanya kazi vizuri)ndio utakuwa katika katika nafasi nzuri ya kuipokea adc.

Akili nyepesi unazo wewe babaangu kwani huwezi hata kuweka space kwny posts zako, nukta...mmmh! Jipange hakurupuki mtu hapa.:loco:
 
adc itakufa hata kabla ya 2015,
nimesahau kumbe bado hata hamjapata usajili wa kudumu!

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema ibara ya 18(a) kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.
Ni haki yako kikatiba bwana. naamini unalijua hilo.
 
nadhani ulipaswa kwanza kuwakaribisha ccj alafu cck na kisha adc na sasa chauma.kuanzisha chama cha siasa ni ngumu sana hivyo walioweza kuanzisha adc na hivyo vyama vingine wanastahili pongezi.......

kwa aina hii ya coment unanipa mashaka kidogo kujua nani akili zake zinafanya kazi vizuri na nani zinamtindio kwa kweli. Nimeona nikushike hapo kwny blue tu kuweza kukujuza ni namna gani kauwezo kako kalivyo kadogo kwenye kukokotoa mambo especially haya ya kisiasa.

Mfano mdogo tu ninaoweza kukupa kuhusiana na siasa na muda ni kwa majirani zetu tu wa hapo KENYA. PNU ie: Party of National Unit kilianzishwa rasmi tar. 16-sept-2007 na mwaka huohuo mwezi Dec 2007 wakasimamisha Mgombea wa RAISI ambaye ndie still President of the so called 'Republic of Kenya'
Imekaa vipi hii?
 
Jina la chama linasadifu ukoloni wa mawazo. Jina la chama kwa Kiingereza. Chama hiki ni cha Tanzania au cha Waingereza? Sipendi sana watu wasiopenda kushirikiana na wenzao.

Kuna vyama vingi sana hapa nchini je mmeona hakuna hata kimoja mnachoweza kushirikiana nao? Hii ndiyo maana naweza kusema mnatumika kuvuruga vyama.

Ni kitu gani kitakacho nishawishi nisisema kwamba nyinyi ni chama pandikizi? Kama Chadema inafanya vizuri kabisa na bado hamwezi kushirikiana nao si mnataka kugawa kura ili CCM iendelee kutawala? Acheni ubinafsi.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema ibara ya 18(a) kila mtu anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake.
Ni haki yako kikatiba bwana. naamini unalijua hilo.

ibara ya 18a hair0husu kuongea pumba no research no right to speak upo hapo au umekunywa urojo wenye mafuta ya nguru ukalewa teh teh teh
 
Jina la chama linasadifu ukoloni wa mawazo. Jina la chama kwa Kiingereza. Chama hiki ni cha Tanzania au cha Waingereza? Sipendi sana watu wasiopenda kushirikiana na wenzao. Kuna vyama vingi sana hapa nchini je mmeona hakuna hata kimoja mnachoweza kushirikiana nao? Hii ndiyo maana naweza kusema mnatumika kuvuruga vyama. Ni kitu gani kitakacho nishawishi nisisema kwamba nyinyi ni chama pandikizi? Kama Chadema inafanya vizuri kabisa na bado hamwezi kushirikiana nao si mnataka kugawa kura ili CCM iendelee kutawala? Acheni ubinafsi.

Sidhani kama ni tatizo kutumia kiingereza katika jina la chama kwani ni lugha official hapa nchini Tanzania. Mashuleni inatumika kufundishia na maofisini pia. Plus Uhuru wetu tuliukwaa kutoka kwa haohao Waingereza.

Hoja kuhusu Upandikizi na kwamba Uzuri wa Chadema sio kila mtu anaukubali na ndio maana hasa ya demokrasia. Lakini pia huko kuungana nadhani chadema ndio wa mwanzo kupinga muunganiko huo. Tumeona baada ya kuukwaa Ukuu wa Upinzani Bungeni hawajataka kushirikiana na chama chochote cha Upinzani.
 
ibara ya 18a hair0husu kuongea pumba no research no right to speak upo hapo au umekunywa urojo wenye mafuta ya nguru ukalewa teh teh teh

Haijataja pumba wala no research no right to speak, ila imesema tu kwamba 18. Kila mtu (a) anao uhuru wa kuwa na maoni na kueleza fikra zake. (b) anayo haki ya kutafuta, kupokea na kutoa habari bila ya kujali mipaka ya nchi. Sasaa sijaona sehemu waliyoandika Pumba No Reseach No..... Usiwe kama hilo jina lako kiongozi, Nijuavyo mimi Fungo ni kijimnyama fulani hv. Kipo kipo tuu. ok! Aliyekuita hvyo hajakosea.
 
Hapa ulitaka kusema nini...

Kwakweli Crashwise neno 'INJI' nalipenda sana kulitumia kwani mimi huwa ni shabiki sana wa Speech za Mhe. Lyatonga, na hakika akizungumza kama usipocheka utakua na hitilafu kwenye brain yako. Yani huyu Mzee miaka yote yuko mjini lakini STILL hajaweza kutamka neno Nchi. Utamsikia tu 'INJI HII'.
Note: Sikuwa na lengo la kuelekeza kidole changu kwny chama fulani. Hapana Msininukuu Vibaya tafadhali.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom