Karibu tushauriane juu ya nini cha kufanya na matokeo yako ya kidato cha 6

Kwa mujib wa tcu, kuingia chuo kikuu ni lazima uwe na principle 2 zenye jumla ya pointi 4.
Computer science ni physics na mathematics.
Physics kapata D na mathematics E. Ukihesabu points hapo, unapata D+E= 3. (Sababu D=2 na E=1).Kwa hiyo hatopokelewa chuo kikuu.
Vp kuhusu DDS chuo unaenda matokeo ya Mwaka huu
 
Wakuu nahitaj wanafunz wanasoma I T A(Institute of tax administration) anitext 0716479352 msaada unahitajika.... Natumai ntawapata
 
Habari Eric.
Watu Wengi Chuo Wanaangalia Vitu Vifuatavyo
-Interest yako. Yani ungependa kusoma nini?
-Mkopo. Kuna Kozi ni Nzuri ila priority zao kwenye mkopo ni ndogo sana. Kozi karibia zote za biashara including hiyo Human Resource huwa hazina kipaumbele. Hata Law. Kwa msingi unaeza kuta mtua anapenda Law ila kachagua Education kwa sababu ya mkopo hasa kwa watu wa familia za hali ya chini.

-Uwezekano wa Kupata Ajira Haraka na Yenye Mshahara Mzuri. Hapa ndo utakuta watu wanakuambia labda soma HR kwa sababu inalipa vizuri japo haina mkopo. Au hata mwingine atakushauri usome Kiswahili kwa sababu walimu wa kiswahili wanahitajika sana hasa nchi za Afrika mashariki.

Ushauri Wangu.
Tafuta Kile Kijitabu cha TCU hata cha mwaka jana then uangalie kozi ama kwa vigezo vyako au hivyo nilivyokushauri hapo juu.. Tembelea pia websites za vyuo kama udsm, saut, sua, ardhi, mzumbe n.k pia wameweka taarifa ya kozi zote za undergraduate na entry requirements..

Ushauri wa Wadau Wengine Humu Pia Uzingatie!
 
Mkuu kijana wangu amesoma PCB amepata 4.19 yaani S zote na F ya chemistry, anaweza kufanya nini kwa sasa???
mkuu sidhani kama anaweza endelea manake hiyo ni kmama sifuir kwa kipidi chetu sijui sasa labda ajaribu kufuatilia utaratibu wa diplooma.
 
Wakuu shikamoo,
Mimi ni mtahiniwa wa ACSEE 2016, naomba mnisaidie grades zilizotumika kwenye upangaji matokeo yetu wakati wa usahishaji make mimi kama mimi zinanichanganya..msaada tafadhali
a b c d e s a=5, b=4, c=3, d=2, e=1, s=0.5. usiwe nahofu kijana point 4 unaenda chuo kikuu TCU wamefafanua jana, ila niambie unataka soma kozi gani mkuu?
 
Nimeona kuna thread nyingi zimefunguliwa kila mtu akiulizia kuhusu kujiunga na chuoo na watu wamekuwa na Matokeo tofauti tofauti!!!

Kwa utaratibu ulio tolewa hivi karibu na tume ya vyuo vikuu ni kuwa CUTT POINT minimum ni 4.0 SASA BASI KATIKA MATOKEO YAKO AU YA NDUGU YAKO HAKIKISHA KUWA ANA (D,D)! NAKUENDELEA

Kama atakuwa ana D moja kushuka chini huyo chuo kikuu hataweza kwenda bila kujari combination alio isomaaa!!!

Na watu hao wengi wapo kwenye Division Three (3) ya point 15. Na wengine point 14! Usihangaike kuomba chuo kama huna D 2 na kuendelea!

Kwa watu wa Diploma ni GPA ya 3.5 kinyume cha hapo ni usisumbuke kuomba chuo kikuu

Huo ndio uelewa wangu kulingana na utaratibu wa chuo ulivyo kwa sasa!!!

Kama kuna mwenye nyongeza karibu
wamesema jana TCU wanaangalia cuttoff point tuu ambazo ni 4. nakwa mwaka jana diploma walikua wanachukua 2.7gpa. kuhusu diploma sijui ila f6 ni 4points
 
natumai mengi ushaambiwa kikubwa kozi za sanaa hazina soko. usijaribu kuomba ualimu jua ajira hamna nakuhakikishia serikali imetosheka wanahitajika walimu wa science tuu. labda omba human resource, law, pia omba wazazi wako wakuandalie ajira mapema kwa kuomba kwa marafiki zao hali ni ngumu sana best
 
Mimi nakushauri Chukua matokeo ya form four kama ni mazuli kasome certificate then diploma thrn utaenda degree,utachelewa kufika lakini utafika vizuli hizo S.S.Fzitakusumbua kupata chuo .Ukizingatia hivi karibuni kumekuwa na wanafunzi hewa,na wengine viwango kutotimia lakini wakaingia chuo. Chukua ushauri wangu mpeleke mwanao mwaka huu certificate september mwakani sio mbali atakuwa amemaliza certficate na baada ya hapo mwaka 2019 atakuwa amemaliza diploma.
 
alizotaja mkuu hapo juu its ok ila kombi za sanaa hazina lake saivi. kuhusu ualimu serikali ilisema haihitaji tena inatosheka. kwa sababu anaenda jeshini itakua poa sababu kule ukiwa na elimu kupata heo inakua simpo, me namshauri tuu asome sheria au human resource tena aombe mzumbe , udsm na nit kama itashindaniwa sana hiyo kozi aombe saut
 
Mimi nakushauri Chukua matokeo ya form four kama ni mazuli kasome certificate then diploma thrn utaenda degree,utachelewa kufika lakini utafika vizuli hizo S.S.Fzitakusumbua kupata chuo .Ukizingatia hivi karibuni kumekuwa na wanafunzi hewa,na wengine viwango kutotimia lakini wakaingia chuo. Chukua ushauri wangu mpeleke mwanao mwaka huu certificate september mwakani sio mbali atakuwa amemaliza certficate na baada ya hapo mwaka 2019 atakuwa amemaliza diploma.
uzima ni jambo la kwanza mkuu. pia kama anamatokeo mazuri diploma anenda
 
KE_PCM_ECE point 13,sijui watamchagua au ndio tumftafutie genge la nyanya maana pesa ya diploma hamna?
Mtafutie Genge la nyanya maana hata akichaguliwa kwa kigezo cha kuwa na point 4 yaani C na E mkopo hawezi kupata kama hana division II
1468770995499.jpg
 
Back
Top Bottom