Kanuni inasemaje: Waziri mkuu au Kiongozi wa Upinzani asimamapo bungeni?

quote_icon.png
By Ritz

Yote haya yametokana na kitendo cha kipuuzi alichofanya Mbowe leo, tatizo la Mbowe ni elimu.

Bado hujajibu swali la msingi. Hebu angalau jitutumue kidogo na ujibu iwapo ni kweli au siyo kweli anaposimama KUB bungeni asikilizwe. JIBU HILO TU NA NITAKUONA WEWE NI MWANAUME WA SHOKA!

HAWEZI KUJIBU HII
 
Tangu nizaliwe sijawahi kuwa mpuuzi kama wavaa suti wa leo bungeni hasa naibu spika. Nachukia kuvaa suti kwa sababu hata wahuni wanazivaa na mimi sio mhuni.
 
Badala ya kutukana ungetoa ufafanuzi. Hii inaonesha jinsi ambavyo unatumika kama tambara la deki.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Huyu usipoteze muda wako kumjibu,unaweza kupata BAN bure.Maana yeye mbichi anaziita kavu.Na kwa kutomjibu itamsaidia hata yeye kuona anatakiwa kupost nini kulingana na wazo la mtu alilotoa.
 
Watu wengne inabidi kuanza elimu ya awali ndipo waanze kufunguka. KUB akiwa bungeni anaheshimika sawa na waziri mkuu. Nyie ambao mnajitia hamjui hayo ndio mnasababisha Watanzania wote hatujui kitu na hivyo nchi itafunwe na walafi wachache!
 
Kiongozi wa Upinzani na Waziri mkuu ni vyeo tafauti kabisa acha kutuletea mada zilizolegea kiasi hiki.

Simply WM yuko madarakani while KUB anawakilisha minority haibadili majukumu. You should learn how these titles works. Ndo maana siku ya maswali kwa WM anaanza KUB then the rest wanafuata.
 
Kiongozi wa Upinzani na Waziri mkuu ni vyeo tafauti kabisa acha kutuletea mada zilizolegea kiasi hiki.
Mtu kaleta Uzi apewe ufafanuzi,ama aeleweshwe juu ya kanuni za Bange..Sorry Bunge zinasemaje pindi asimamapo Waziri Mkuu au Kiongozi wa Kambi ya Upinzani...
Sasa wewe unaleta maneno gani hapa!!?
Kwani ni lazima utoe comments!?
 
Inawezekana kanuni hazisemi lolote. Lakini busara ingetumika na kumruhusu Mbowe kuzungumza. Ndiyo ni mbunge kama wengine lakini kofia yake inamfanya awe tofauti na wabunge wengine. Kilichotokea ni kumdhalilisha kwa makusudi. Alichofanya Ndugai ni uchochezi. Kivipi? Ni kwa sababu anaamsha hasira za watu/raia wazidi kuichukia serikali kutokana na ujinga wake wa kutoelewa mambo. Ingekuwa Mbowe katukana ama kupiga mbunge bungeni, hapo Ndugai angekuwa kwenye haki lakini kuomba kuzungumza tena kwenye suala nyeti la katiba, hakupaswa kuamuru atoke nje. Hilo la kulazimisha kuzungumza lingejadiliwa baadaye. CCM wamejisahau, wanawapa ujiko wapinzani.

Serikali pia inatambuia hilo kwamba huyu ni mtu mkubwa mno, ndiyo maana hata sisi wananchi tunachukulia hivyo kwa sbabu ni serikali yenyewe ilyomtambua hivyo, na kuna wengine tunaamini kuwa cheo chake cha u-enyekiti wa chama cha chadema kinampa hadhi nyingine kubwa mno ambayo ni sawa tu na ya mwenyekiti wa chama kingine chochote kile. Wananchi kwa kweli tusingependa kouna disrepect inafanyika kwa viongozi wetu bila kujali ni wa chama gani.
 
ndugai ni centre defender, ni dhaifu kibogoyo...naichukia sana sisiemu na sasa nashindwa kuelewa nimchukie yeye au bunge
 
Kanuni wametunga wenyewe, sasa zinawatafuna wanabaki kumlaumu NDUGHAI.

Hujui sheria kub na waziri mkuu bungeni ni vyeo vinavyofuata katika bunge hivyo acha ushabiki kuwa mkweli kama hujui muulize msekwa mpo nae
 
Simply WM yuko madarakani while KUB anawakilisha minority haibadili majukumu. You should learn how these titles works. Ndo maana siku ya maswali kwa WM anaanza KUB then the rest wanafuata.

Hivi unajuwa kuwa waziri mkuu ni KIONGOZI na MSIMAMIZI wa shughuli ZA SERIKALI BUNGENI, nje ya hapo ni mazoea na kukariri kwetu tu, upande wa KUB nakushauri nenda ukasome kanuni zinasemaje kuhusu yeye, maana nikikusimulia nitakuwa nakuongezea tatizo tu badala ya kukusaidia, maana hata hapo ulipofika ni matokeo ya kusimuliwa simuliwa tu, badala ya kurutubisha akili na uelewa wako kwa ku dig deep.
 
Kiongozi wa Upinzani na Waziri mkuu ni vyeo tafauti kabisa acha kutuletea mada zilizolegea kiasi hiki.

wewe nawe fafanua vizuri,ni kweli vyeo tofauti lakini kila mmoja ana nafasi yake ktk bunge na mamlaka,ndo mana anaongoza waziri vivuli,eleza vizur tu lakini sio kumkrash mtu,onyesha upeo wako wa kuelekeza kama hujui uliza kwanza,
 
nimemsikia mara kwa mara Naibu spika mh Ndugai akiwaomba wabunge kuzielewa kanuni na kujua kuzitafsiri hii imekua ni kauli yake kila siku ndani na nje ya bunge. lakini kinachonishangaza mara kwa mara ni namna ambavyo kiongozi huyu wa bunge ambavyo amekua akiliendesha bunge kiubabe na kutokuzieshimu kanuni na imekua akiliendesha kwa matakwa na mwitikio wa hisia zake ikiwewemo na ubinafsi wake juu ya kulinda na kukuza interest za chama chake hii inanifanya nisimwelewe kuwa ni binaadamu wa namna gani mwenye kukataa jambo analolipenda na kulifanya kila wakati na ndio hapa natambua dhairi kua mtu huyu ni mwenye unafiki wa hali ya juu tena wa wazi kabisa naamini na nafahamu kanuni nyingi za bunge na tafsiri zake naamini na nafahamu kua KUB na waziri mkuu ni watu muhimu sana kwa bunge na hawa ndio wanaweza kulifanya bunge kua la utulivu ama la vurugu kwa maana kwamba kama WAZIRI MKUU hatashindwa kuwathibiti wabunge wakambi yake ambayo ndio kambi ya serikali basi ni lazima usawa upotee na vile vile kama KUB atakua wa ovyo kushindwa kuwaongoza hawa wachache basi ni hatari zaidi kwa maana waswahili wanasema kua vurugu ya watu wachache ndio vurugu kubwa kuliko ile ya wengi sasa huyu KUB Abaye ndiye mbowe akishindwa kuwa makini ama akapingwa na kunyanyaswa bungeni basi hawa wachache watachukia kwa sababu jemedali wao ananyanyaswa na vurugu zake ni kubwa kutokana na uchache wa watu hawa wa KUB sasa watu wa hivi kama ndugai wenye kuzalau mawazo ya wachache kupitia KUB nihatarina hawana sifa za kuongoza chombo hiki(BUNGE(
 
Shida inakuja pale bunge linapoongozwa kiushabiki wa ki-ccm na kuonekana wengine hawana haki ya kusema. Nijuavyo mimi kwa akili zangu ndogo KUB ni waziri mkuu kivuli na wakati wowote anaweza kusimama na kuweka sawa mambo.

Hivyo ni ujuavyo wewe, maandiko ktk kanuni za bunge hayako hivyo, yamefafanuliwa jana wakati kabla ya kuahirisha bunge. Priority ya KUB ni wakati wa maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu tu.

Tatizo hapa ni mazoea hujenga tabia, yale mazoea ya kwamba 'hebu tumsikilize KUB' mtu anajiaahau na kujivisha joho lisilo lake.
 
Back
Top Bottom