Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

prospilla

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
1,111
1,637
Yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL Ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia Dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililoathirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.

Anasumbuliwa na; MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHOPONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya Mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
 
Pole, lakini lazima NIKUAMBIE UKWELII.

Hiyo unayoiita TIBA MBADALA ndio TIBA HALISI, Mimea ya asili yenye nguvu ya kukuponya na kuhuisha mwili dhidi ya maradhi ya aina yoyote.

Hayo MAKEMIKALI ndio yalipaswa kuwa TIBA MBADALA. Ukishafeli kutumia MIMEA SAFI (kitu ambacho hakiwezekani) sasa ndio ukajijaze MAKEMIKALI MACHAFU na MIONZI.

Mkiambiwa MNABEZA, ooohh MIMEA NI UCHAWI! Haya sasa!!!!! Umerudi kule kule!!!

Oooohh, wewe hujui sayansi, wewe mchawiii!! Sayansi yenyewe ndio hiyo, umelipa MAMILIONI ukajazwa MIONZI LUKUKI mpaka mwili ukaharibika zaidi na zaidi.

Najua kuna MAKANJANJA watanivamia hapa, lakini sijali. MIMI NAPASUA UKWELI TU, tukana, bwata, lakini HABARI IMEFIKA.
 
Pole Sana Kiongozi..... Nayahisi maumivu unayopitia....

Sina ujuzi kwenye hili ila Naomba Mungu amlinde na kumpa nguvu Mke wako.

Amuondolee kabisa maumivu yanayomsumbua, na kumponya kabisa hiyo saratani Kwa Jina la Yesu Kristo.

Damu ya Yesu imfunike na naalika ufalme wa Mungu utawale Nyumbani kwako.

Pia mpende sana mke wako Kwa moyo wako wote Katika kipindi hiki anachopitia na Mungu wa Mbinguni atawabariki.

Hakuna linaloshindikana mbele zake Kwa Imani.

Amina.
 
Pole, lakini lazima NIKUAMBIE UKWELII.

Hiyo unayoiita TIBA MBADALA ndio TIBA HALISI, Mimea ya asili yenye nguvu ya kukuponya na kuhuisha mwili dhidi ya maradhi ya aina yoyote.

Hayo MAKEMIKALI ndio yalipaswa kuwa TIBA MBADALA. Ukishafeli kutumia MIMEA SAFI (kitu ambacho hakiwezekani) sasa ndio ukajijaze MAKEMIKALI MACHAFU na MIONZI.

Mkiambiwa MNABEZA, ooohh MIMEA NI UCHAWI! Haya sasa!!!!! Umerudi kule kule!!!

Oooohh, wewe hujui sayansi, wewe mchawiii!! Sayansi yenyewe ndio hiyo, umelipa MAMILIONI ukajazwa MIONZI LUKUKI mpaka mwili ukaharibika zaidi na zaidi.

Najua kuna MAKANJANJA watanivamia hapa, lakini sijali. MIMI NAPASUA UKWELI TU, tukana, bwata, lakini HABARI IMEFIKA.

Ati Kumuachia Mungu!! 🤣🤣🤣

Mmekaa mnasubiri CHANJOO! Aiseee!!

This LAZY MENTALITY and IRRESPONSIBILITY ndio chanzo cha nyinyi kuwa mazombi mnaobugia MAKEMIKALI BILA KUHOJI.

Unamuachiaje Mungu??? 🤣🤣
Inawezekana una hoja nzuri sana lkn uwasilishaji wako siyo rafiki kwa mtu anayeuguza.
Kama umeshawahi hata kumtembelea mtu mwenye kansa utaelewa hili.Sijawahi kuuguza ila nimeshawatembelea relatives kadhaa nyumbani na hospitalini aisee si kitu rahisi hata kidogo.
 
CHEMOTHERAPY haiwezi kukuponya KANSA, inakuongezea KANSA. Ni kama unajibanika kwenye TANURU LA MOTO.

Achana na CHEMOTHERAPY, angalia chakula chake cha kila siku ni chakula gani?

Kama una akili timamu, ungelima hapo bustani upande mchicha mwingi ambao hauna MAKEMIKALI, pamoja na KAROTI, hiyo iwe FIRST AID yake.

MAUCHAFU kwenye damu yake pia, SUMUU, UTANDO, MUCUS, afanye namna ya kuondoa yote hayo. DAMU CHAFU.

PAMBANA SANA, ATAPONA KAMA UNA AKILI TIMAMU.

Ukiendelea na MAKEMIKALI na hizo CHEMOTHERAPY utamuangamiza.
 
Back
Top Bottom