Saratani ya Matiti, saratani inayowapata watu wengi

Kidaya

Member
Dec 20, 2011
55
49
Saratani ya Matiti ni nini?
Kwanza, Saratani ni ugonjwa unaosababishwa na kugawanyika kwa seli za kiungo chochote mwilini bila kufuata utaratibu wa kawaida hivyo kusababisha kuzaliwa kwa seli zenye ukubwa, umbo na uwezo wa kufanya kazi tofauti na inavyopaswa, na kusababisha dalili hatarishi kwa maisha ya mgonjwa kama vile maumivu, kutoka damu, kidonda kisichopona, uvimbe n.k.
Saratani ya matiti ni saratani inayoanzia kwenye seli za tishu zilizo kwenye matiti au saratani iliyosambaa kutoka kwenye kiungo kingine na kulifikia titi

Takwimu za Saratani ya Matiti
▪️ Kwa mujibu wa makadirio ya mtandao wa tafiti za saratani, Globocan, Saratani ya matiti ni saratani inayoongoza kuwapata watu wengi zaidi ambapo ni 11.7% ya saratani zote zinazowapata watu
▪️ Takwimu za kidunia za mwaka 2020 zinaonesha watu milioni 2.3 waligundulika na saratani ya matiti
▪️ Watu 7.8 wanaishi na saratani hii, miaka mitano tangu walipogundulika
▪️ Zaidi ya 99% ya wanaopata saratani ya matiti ni wanawake na chini ya 1% ni wanaume
- Hapa kwetu Tanzania, saratani ya matiti ni ya pili kwa kuwapata watu wengi kwa mujibu wa takwimu za makadirio ya mtandao wa takwimu za saratani (Globocan), ambapo watu 3,992 walipata saratani ya matiti kwa mwaka 2020
1698646196580.png
1698646006145.png

Vichocheo vya Saratani ya Matiti
Vitu vinavyomuongezea mtu uwezekano wa kupata saratani ya matiti ni;
1. Jinsia – wanawake wako hatarini zaidi kuliko wanaume
2. Umri – kuwa na zaidi ya miaka 50
3. Historia binafsi – kama umewahi kuwa na saratani kwenye titi moja kunaongeza uwezekano wa kupata saratani kwenye titi lingine
4. Kuwa na ndugu aliyewahi kuwa na saratani ya matiti, kurithi vinasaba vyenye hitilafu kutoka kwa wazazi
5. Kuanza hedhi mapema chini ya umri wa miaka 12
6. Kuchelewa kupata mtoto wa kwanza hasa baada ya umri wa zaidi ya miaka 30
7. Kutowahi kabisa kubeba mimba, na kutonyonyesha
8. Kuwa na uzito uliozidi usioendana na urefu
9. Matiti kupata mionzi wakati wa tiba ya mionzi
10. Unywaji wa pombe na ulaji usiofaa usiozingatia lishe bora
11. Kupata tiba ya vichochea mwili (hormonal therapy)venye homoni moja ya estrogen kwa zaidi ya miaka mitano.

Dalili za Saratani ya Matiti
Mtu mwenye saratani ya matiti huweza kuwa na dalili zifuatazo;
1. Kuwa na vivimbe kwenye titi, titi kubadilika umbo na ukubwa na mwonekano, titi kuvimba, kuwasha n.k
2. Kubadilika kwa ngozi ya titi na kuwa na madoa au vishimo, maumivu kwenye titi na eneo kuzunguka titi
3. Kutoa majimaji au damu kwenye chuchu, kuchubuka kuzunguka chuchu, chuchu kuingia ndani, kupata kidonda
1698646682859.png

Uchunguzi wa Saratani ya Matiti
Uchunguzi wa awali unaweza kujifanyia mwenyewe hasa baada ya kunaliza kuoga kwa kujichunguza matiti yako mbele ya kioo kama yana dalili tajwa hapo juu na unapoona yana matiti yako yana mabadiliko yasiyo ya kawaida basi uwahi hospitali kwa vipimo zaidi.
Kwa hospitali, kipimo cha maabara cha kuchunguza kinyama kutoka kwenye titi linalohisiwa kuweza kuwa na saratani hufanyika kuhakiki uwepo saratani ya matiti.
Vipimo vya picha (kama mammography, X-ray, ultrasound, CT scan, MRI na PET scan) huweza kufanyika kuchunguza dalili na hatua ya saratani matiti ilipofikia.

Matibabu ya Saratani ya Matiti
Kutegemea hatua saratani ilipofikia na hali ya kiafya ya mgonjwa, mgonjwa anaweza kupatiwa tiba ya upasuaji, tiba ya kemikali, tiba ya mionzi, tiba ya vichochea mwili (hormonal therapy) nk.
Tiba hizi huweza kutolewa moja au zaidi ili kuongeza mafanikio ya matibabu kwa maana mgonjwa apone kabisa ugonjwa wake, kumuondolea dalili hatarishi au kupunguza uwezekano wa ugonjwa kurudi.

Kujikinga na Saratani ya Matiti
Hakuna kinga ya kumzuia mtu kwa 100% asipate kabisa saratani kwenye maisha yake, yaani kwa lugha nyepesi kila mtu anaweza kupata saratani ya matiti. Lakini, unaweza kupunguza uwezekano kupata saratani ya matiti kwa kufanya yafuatayo;
1. Kumnyonyesha mtoto kila unapojifungua
2. Kuzingatia ulaji mlo kamili wenye matunda na mboga za majani
3. Kufanya mazoezi na kuwa na uzito unaoendana na urefu wako
4. Kupunguza unywaji wa pombe
5. Kupunguza utumiaji wa tiba/dawa zenye homoni moja ya estrogen peke yake.
6. Kujichunguza matiti mara kwa mara na kwenda hospitali unapohisi mabadiliko kwenye titi ili ugonjwa ugundulike mapema na hivyo kuongeza
mafanikio ya matibabu.

Wapi uende kupata huduma za Saratani?
Hospitali za serikali za Taifa, Kanda na Mikoa, huduma za saratani hupatikana kwa ufanisi mkubwa.
Pia zipo hospitali za mashirika ya dini, watu binafsi na za makampuni zinazotoa huduma za saratani ikiwemo elimu, uchunguzi na matibabu ya saratani.
1698647286915.png

Kumbuka
▪️Hakuna tiba mbadala, tiba za asili, tiba za kiroho wala dawa za mitishamba zilizothibishwa kuwa na uwezo wa kutibu saratani, fika hospitali kwa matibabu ya saratani.
▪️Hakikisha unamjulisha daktari wako kuhusu tiba au dawa zozote za ziada unazotaka kutumia au umeshauriwa na mtu mwingine utumie wakati tayari ukiwa umeshaanza matibabu ya hospitali, kwani kuna baadhi ya dawa au tiba huweza kuingiliana na dawa ulizopewa (drugs interaction), hivyo kuweza kupunguza ufanisi wa matibabu uliyopangiwa.
▪️Share na wengine elimu hii kama sehemu ya mchango wako katika kupambana na ugonjwa saratani.

Together🤝, we are stronger💪 than cancer🧬
 
Attachments

  • 1698646512230.png
    1698646512230.png
    134.9 KB · Views: 12
Saratani ya Matiti ni nini?
Kwanza, Saratani ni ugonjwa unaosababishwa na kugawanyika kwa seli za kiungo chochote mwilini bila kufuata utaratibu wa kawaida hivyo kusababisha kuzaliwa kwa seli zenye ukubwa, umbo na uwezo wa kufanya kazi tofauti na inavyopaswa, na kusababisha dalili hatarishi kwa maisha ya mgonjwa kama vile maumivu, kutoka damu, kidonda kisichopona, uvimbe n.k.
Saratani ya matiti ni saratani inayoanzia kwenye seli za tishu zilizo kwenye matiti au saratani iliyosambaa kutoka kwenye kiungo kingine na kulifikia titi

Takwimu za Saratani ya Matiti
Kwa mujibu wa makadirio ya mtandao wa tafiti za saratani, Globocan, Saratani ya matiti ni saratani inayoongoza kuwapata watu wengi zaidi ambapo ni 11.7% ya saratani zote zinazowapata watu
Takwimu za kidunia za mwaka 2020 zinaonesha watu milioni 2.3 waligundulika na saratani ya matiti
Watu 7.8 wanaishi na saratani hii, miaka mitano tangu walipogundulika
Zaidi ya 99% ya wanaopata saratani ya matiti ni wanawake na chini ya 1% ni wanaume
- Hapa kwetu Tanzania, saratani ya matiti ni ya pili kwa kuwapata watu wengi kwa mujibu wa takwimu za makadirio ya mtandao wa takwimu za saratani (Globocan), ambapo watu 3,992 walipata saratani ya matiti kwa mwaka 2020
View attachment 2797666View attachment 2797664

Vichocheo vya Saratani ya Matiti
Vitu vinavyomuongezea mtu uwezekano wa kupata saratani ya matiti ni;
1. Jinsia – wanawake wako hatarini zaidi kuliko wanaume
2. Umri – kuwa na zaidi ya miaka 50
3. Historia binafsi – kama umewahi kuwa na saratani kwenye titi moja kunaongeza uwezekano wa kupata saratani kwenye titi lingine
4. Kuwa na ndugu aliyewahi kuwa na saratani ya matiti, kurithi vinasaba vyenye hitilafu kutoka kwa wazazi
5. Kuanza hedhi mapema chini ya umri wa miaka 12
6. Kuchelewa kupata mtoto wa kwanza hasa baada ya umri wa zaidi ya miaka 30
7. Kutowahi kabisa kubeba mimba, na kutonyonyesha
8. Kuwa na uzito uliozidi usioendana na urefu
9. Matiti kupata mionzi wakati wa tiba ya mionzi
10. Unywaji wa pombe na ulaji usiofaa usiozingatia lishe bora
11. Kupata tiba ya vichochea mwili (hormonal therapy)venye homoni moja ya estrogen kwa zaidi ya miaka mitano.

Dalili za Saratani ya Matiti
Mtu mwenye saratani ya matiti huweza kuwa na dalili zifuatazo;
1. Kuwa na vivimbe kwenye titi, titi kubadilika umbo na ukubwa na mwonekano, titi kuvimba, kuwasha n.k
2. Kubadilika kwa ngozi ya titi na kuwa na madoa au vishimo, maumivu kwenye titi na eneo kuzunguka titi
3. Kutoa majimaji au damu kwenye chuchu, kuchubuka kuzunguka chuchu, chuchu kuingia ndani, kupata kidonda
View attachment 2797669

Uchunguzi wa Saratani ya Matiti
Uchunguzi wa awali unaweza kujifanyia mwenyewe hasa baada ya kunaliza kuoga kwa kujichunguza matiti yako mbele ya kioo kama yana dalili tajwa hapo juu na unapoona yana matiti yako yana mabadiliko yasiyo ya kawaida basi uwahi hospitali kwa vipimo zaidi.
Kwa hospitali, kipimo cha maabara cha kuchunguza kinyama kutoka kwenye titi linalohisiwa kuweza kuwa na saratani hufanyika kuhakiki uwepo saratani ya matiti.
Vipimo vya picha (kama mammography, X-ray, ultrasound, CT scan, MRI na PET scan) huweza kufanyika kuchunguza dalili na hatua ya saratani matiti ilipofikia.

Matibabu ya Saratani ya Matiti
Kutegemea hatua saratani ilipofikia na hali ya kiafya ya mgonjwa, mgonjwa anaweza kupatiwa tiba ya upasuaji, tiba ya kemikali, tiba ya mionzi, tiba ya vichochea mwili (hormonal therapy) nk.
Tiba hizi huweza kutolewa moja au zaidi ili kuongeza mafanikio ya matibabu kwa maana mgonjwa apone kabisa ugonjwa wake, kumuondolea dalili hatarishi au kupunguza uwezekano wa ugonjwa kurudi.

Kujikinga na Saratani ya Matiti
Hakuna kinga ya kumzuia mtu kwa 100% asipate kabisa saratani kwenye maisha yake, yaani kwa lugha nyepesi kila mtu anaweza kupata saratani ya matiti. Lakini, unaweza kupunguza uwezekano kupata saratani ya matiti kwa kufanya yafuatayo;
1. Kumnyonyesha mtoto kila unapojifungua
2. Kuzingatia ulaji mlo kamili wenye matunda na mboga za majani
3. Kufanya mazoezi na kuwa na uzito unaoendana na urefu wako
4. Kupunguza unywaji wa pombe
5. Kupunguza utumiaji wa tiba/dawa zenye homoni moja ya estrogen peke yake.
6. Kujichunguza matiti mara kwa mara na kwenda hospitali unapohisi mabadiliko kwenye titi ili ugonjwa ugundulike mapema na hivyo kuongeza
mafanikio ya matibabu.

Wapi uende kupata huduma za Saratani?
Hospitali za serikali za Taifa, Kanda na Mikoa, huduma za saratani hupatikana kwa ufanisi mkubwa.
Pia zipo hospitali za mashirika ya dini, watu binafsi na za makampuni zinazotoa huduma za saratani ikiwemo elimu, uchunguzi na matibabu ya saratani.
View attachment 2797679
Kumbuka
Hakuna tiba mbadala, tiba za asili, tiba za kiroho wala dawa za mitishamba zilizothibishwa kuwa na uwezo wa kutibu saratani, fika hospitali kwa matibabu ya saratani.
Hakikisha unamjulisha daktari wako kuhusu tiba au dawa zozote za ziada unazotaka kutumia au umeshauriwa na mtu mwingine utumie wakati tayari ukiwa umeshaanza matibabu ya hospitali, kwani kuna baadhi ya dawa au tiba huweza kuingiliana na dawa ulizopewa (drugs interaction), hivyo kuweza kupunguza ufanisi wa matibabu uliyopangiwa.
Share na wengine elimu hii kama sehemu ya mchango wako katika kupambana na ugonjwa saratani.

Together, we are stronger than cancer
LIBARIKiwe Tumbo lililokuzaa,
Tutawasaudia sana akina mama, na akina dada na watoto wetu miaka ijayo kwa andiko lako.

Big up.for evidence based.
 
Back
Top Bottom