Wadau nimetoswa na bintii niliyempenda na bado nampenda kwa sababu ya wasiwasi wake kwangu kwamba siku moja nikimkataa ataumia sana.
Huyu binti nilimtokea na mazungumzo yalienda vizuri,na nilimuakikishia kwamba mahusiano yangu na yake ni ya yeye awe mke wangu na si vinginevyo.Ghafla alianza kubadilika nikawa simuelewi namna anavyojibu,anajibu kimkato haoneshii kujali nikimuuliza kulikoni ananijibu yupo kawaida tu.
Baadae rafiki yangu akaniambia huyu binti alimfuata na kumwambia kuwa ananipenda sana kiasi kwamba siku nikimkataa anaweza kuchangikiwa
na kuumia sana,kwa hiyo ameamua anikatae mapema ili kuepusha maumivu ya baadae.Baada ya maelezo hayo nimechanganyikiwa hata sijui
nimwambie nini ili aniamini si mtu wa aina anayoifikiria.Nimebaki kuwa kimya nikiendelea kutafakari ipo sababu nyingine au ni hii hii.
Wadau nimeyaleta kwenu kama mnaweza kunishauri juu ya jambo hili.