Kanisa kemeeni Uvunjifu wa Haki, Msipo badilika Makanisa yatabaki Magofu

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Ni kiri wazi mimi nina imani kali sana unapozungumzia Mungu au Yesu kristo, Ni moja kati ya watu ninaoamini Mungu yupo na sisi sote ni mali yake.

Lakini taratibu nimeanza kuwa mtoro kanisani, si kwamba siombi Mungu. Hapana, Namwomba Mungu lakini nikiwa nyumbani au popote nitembeapo kimya kimya.

Kwanini nasema imani yangu imeporomoka juu ya makanisa. Nimeshuudia viongozi wa dini wakila kuku ikulu huku wakiambiwa na Rais mikutano ya ndani haijakatazwa nao wakashangilia bila ku challenge chochote, Huku chadema wakiwa wamekatazwa kufanya mikutano yao ya ndani mara nyingi na Ccm wakiifanya kila uchwao tena mpaka ya adhara.

Hili viongozi wahubiri haki hawalioni, Mtakumbuka Rais mara kadhaa ametuambia mikutano ya ndani ni ruksa lakini imebaki ruksa ya mdomo, Pale vyama pinzani wakitaka kuifanya inasambaratishwa.

Hawa viongozi wa dini hawaoni? Nini kimewapofusha kiasi kikubwa namna hii, Maandiko yamebadilika? Leo nimeshuudia ACT wakinyimwa kufanya mkutano wao wa ndani, Tena kwa sababu dhaifu mno aliyoitoa mambosasa. Lakini Lipumba na ndugai wakiwa na mikutano aina hiyo hiyo ikipatiwa baraka zote na polisi.

Hizi ndimi mbili na ukimya juu ya dhuluma na ubaguzi ukiendelea, kwa viongozi wangu wa dini.Nimalizapo kwaresma na kanisa kwangu litakuwa bye bye. Nitalipinga hata kwa maombi.”

Nitaendelea kumwomba Mungu wangu bila kwenda kuwasikikiza Mapadri au Maaskofu wasioweza kukemea dhuluma na kutete haki za waamini.

Na hili sio kwangu tu, Kanisa lisipo badilika yatabaki kama makumbusho kama huko ulaya, Au watabaki vikongwe tu.

Ni Yesu yupi mnamuhubiri kama yote yatendekayo hamyaoni?

Hivi dhambi ni kuzini tu? Badilikeni kabla waamini hawajabadilika.
 
kijana nadhani hujui kuwa sisi viongozi wa dini tuna kazi nyingi sana,sio kila kitu mpaka mtutegemee sisi bana,nyie vipi?,kwani usipokuja kusali nani ataenda motoni?
 
kijana nadhani hujui kuwa sisi viongozi wa dini tuna kazi nyingi sana,sio kila kitu mpaka mtutegemee sisi bana,nyie vipi?,kwani usipokuja kusali nani ataenda motoni?

Dawa yenu sadaka zipungue ili akili iwajie, Nitaanzisha kampeni ya mgomo uone mtakula nini. Halafu sijasema sisali usinilishe maneno,Nitasali kwangu mbaki wewe na wazee wa kanisa ndio utajua upo hapo kuhubiri kweli na haki.
 
Unakosea, shusha lawama zako kwa viongozi na siyo kwa kanisa! Kristo ni kanisa, kupinga kanisa ni kumpinga Kristo

Kemea na walaumu akina Pengo, Mzee wa Upako na konyagi yake, Kakobe nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma waraka wa Kwaresima wa Baraza la Maaskofu wa kanisa Katoliki wa mwaka jana. Ulikemea ubinywaji wa demokrasia, kupotea watu na kutekwa na watu wasiojulikana.

Ni ule Waraka ambao Polycarp Pengo aliupinga na kuwageuka maaskofu wenzake.

Ukishamaliza kuusoma karibu kwenye kanisa Katoliki na kama upo hapo D'Salaam basi ameshakuja aliyeshiriki kuuandaa ule Waraka, Askofu Ruwa'ichi.
 
Washauri viongozi wako muanzishe makanisa na misikiti itakayokuwa ikifanya yatakayokuwa yakiwafurahisha CDM. After all ukihudhuria ama kutohudhuria kanisani ni nani atajali? Labda family yako kama unayo.
 
Utakuwa huko kanisani unataka kwenda kusikia habari za siasa na mambo ya ajabu ajabu.. utajiju
 
Dawa yenu sadaka zipungue ili akili iwajie, Nitaanzisha kampeni ya mgomo uone mtakula nini. Halafu sijasema sisali usinilishe maneno,Nitasali kwangu mbaki wewe na wazee wa kanisa ndio utajua upo hapo kuhubiri kweli na haki.

Wewe ni insignificant, huwezi lifanya chochote kanisa
 
Ukishamaliza kuusoma karibu kwenye kanisa Katoliki na kama upo hapo D'Salaam basi ameshakuja aliyeshiriki kuuandaa ule Waraka, Askofu Ruwa'ichi.
Mbona mwaka huu yupo kimya? Amewekwa kwapani mwa jiwe tayari, ndiyo maana hafunui kinywa chake tena.
 
Mara ya mwisho kugusa kanisan ni baada ya graduation yangu seminar baada ya hapo nasalia chumban. Haya makanisa hasa ya kilokole yamesababisha wazaz wangu wasiishi pamoja. Yamebaki kutabir nani mchawi ili yakupige pesa. Mwanangu ataendelea kusali katoriki ili ajifunze tabia njema ila kiimani hakuna
 
Back
Top Bottom