Tunaliheshimu sana Kanisa Katoliki, Tunawaheshimu sana viongozi wake. Kanisa Katoliki angalau mpaka ninapoandika uzii huu ni Kanisa tajiri sana, linamiliki Taasisi muhimu sana, Hospitali, Zahanati, vituo vya Afya, Shule za chekechea, msingi Sekondari, Vyuo, na vyuo vikuu, Bahati mbaya sana kanisa Katoliki linamiliki hadi Mkombozi Benk.
Kanisa Katoliki linapata sadaka na michango mbalimbali toka kwa waumini wake, ni kanisa ambalo kweli halipaswi kulia njaa, hadi kiwango cha kukimbilia Pesa ambazo zinazua maswali mengi. Walioandaa Chakula cha Hisani kwa ajili ya uanzishwaji wa Jimbo Katoliki Ifakara, walikosa mtu mwingine hadi wamwite Lowassa tu?
Wameenda wapi viongozi wa dini wenye maadili mazuri, mfano Balozi wa baba mtakatifu, mwadhama Kardinali, Maaskofu wakuu, Wakuu wa Mashirika au watu wengine? CCM walitamka wao kwa kinywa chao kuwa Lowassa ni FISADI. Nimejisikia vibaya sana kuona Kanisa limeamua kutoangalia upandaji wa maisha ya watanzania wa sasa kwa sababu ya gharama za Umeme amabazo chanzo chake kimekuwa Richmond, Dowans.
Kweli mmeamua kuyaishi yale mliyoyalaani?. Angalau kwa ajili ya wenye dhamiri changa mngeacha hili. Mihi Vivere Christus est......................