Hongera Kanisa Katoliki kwa kuendelea kusaidia jamii za watu masikini

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau,
Yapo mengi yasiyofaa yanayonenwa dhidi ya Kanisa Katoliki. Ukweli ni kuwa yeyote anayekusudia kuanzisha mradi wowote wa kiroho huanza kwa kulisakama kanisa Katoliki kuwa halifai.

Pamoja na mengi yanayosemwa bado kuna ukweli mchugu kuwa Kanisa Katoliki ndilo linaongoza kwa kutoa misaada kwa Jamii za Watu masikini duniani.

Kwa uchache ni pamoja na Shule mbalimbali kuanzia chekechea hadi Vyuo Vikuu, Vituo mbalimbali vya Afya hadi Hospital za Rufaa, Vituo vya kulelea watoto yatima, huduma za maji, ushauri nasaha, ujasiriamali n.k.

Kwa bahati mbaya wote wanenao mabaya dhidi yenu HAKUNA HATA MMOJA aliyewahi kujitoa Kikamilifu kwa Jamii Kama ninyi mlivyojitoa

Nawapongeza Sana Wakatoliki wote kwa Moyo wa kujitolea kwa hali na Mali.

Mungu wa baba zetu azidi kuwabariki
 
Kweli kabisa mchango wa Kanisa Katoliki Tanzania ni mkubwa sana; shule, vyuo, hospitali, vyuo vikuu, watoto yatima, na miradi mingi mno ya maendeleo kila wilaya nchini na kila nchi duniani.

Kama hujui ni kwamba Kanisa Katoliki ndio taasisi tajiri zaidi duniani, utajiri wake haujaweza kuwekwa katika thamani ya fedha kwani ni mkubwa mno.
 
Labda rekebisha hapo kwenye kusaidia watu maskini. Ilikuwa zamani mkuu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Kweli kabisa mchango wa Kanisa Katoliki Tanzania ni mkubwa sana; shule, vyuo, hospitali, vyuo vikuu, watoto yatima, na miradi mingi mno ya maendeleo kila wilaya nchini na kila nchi duniani.

Kama hujui ni kwamba Kanisa Katoliki ndio taasisi tajiri zaidi duniani, utajiri wake haujaweza kuwekwa katika thamani ya fedha kwani ni mkubwa mno.
Usisahau na MoU.
 
Ki Msingi uimara wa Ukristo Duniani ni Ukatoliki.
Sababu;

1. Uinjilishaji/Mahubiri ya ne no la Mungu yanaongozwa kwa utaratibu maalumu.
Haruhusiwi mtu kuongoza ibada takatifu mbele ya Kanisa kama si Padre, Askofu, Cardinal, au Pope.
Utaratibu wa Kuongoza Ibada takatifu ni zaidi ya Katiba ya Inchi ambayo viongozi wa juu huivunja kwa matakwa yao.
Anayetaka kuvunja desturi za kuongoza ibada takatifu hutengwa na Kanisa na baadaye mtu huyo huanzisha kanisa lake na kupewa jina Protestant .
2. Viongozi wakuu wa Dini kama Mapdre, Masista, Cardinal, Maaskofu na Pope hawaruhusiwi kuoa.
Hii humfanya kiongozi kuwa na jukumu moja tu la kumtumikia Mungu na Wauimini.
Mambo mengine ambayo watu wa Dini tofauti huyabebea pango kama kujamiana, hayo ni mambo binafsi ambayo hata watu Walioa/ kuolewa huvunja kiapo chao kwa kutoka nje ya ndoa.
3. Kanisa Katoliki hutoa huduma za Kiroho na Kimwili kwa nguvu zote. Hii ni tofauti sana na Makanisa Mengine ambayo hutumia muda mwingi kuinjilisha na Kumtaja Yesu tu bila kutaja jina la Mungu.
Kitu cha ajabu kwa Makanisa mengine hasa ya Walokole, huwa hawasali sala ya bwana kwa sababu wanadai wao ni Born again kwa hiyo hawatendi dhambi.
4. Viongozi wakuu wa Kanisa Katoliki huanza kuandaliwa kuanzia elimu za Msingi na husomeshwa masomo yote na utashangaa ndani ya Kanisa Katoliki kuna Mapadre, Maaskofu, Cardinal na Pope ni Madaktari, Wanasheria, Wahasibu, Wachumi nk.
Ili ufuzu kuwa Padre ni lazima usome na kufaulu Korani Takatifu ya madhehebu ya Kiislamu.
 
Back
Top Bottom