Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa?

Kama Lowassa angepewa adhabu iliyo wazi haya yote yasingetokea.

Nani ana uhakika labda Lowassa ametubu? kwa Mungu kuna msamaha ndio maana wote tunakwenda misikitini na makanisani kutubu.
 
Nenda katafute kitabu kinaitwa IN GODS NAME ndo utajua uchafu wa vatican.
Msijidai nyie ndo wasafi kuliko wengine.
 
Unajua nguvu ya pochi katika srikali design ya Banana and Madafu Repuplic?
Wenye pesa hapa wanashindwa kutoa Rushwa iii mauti isiwaapoke tu.
Lupango wanaendawezi wa kuku, cheni na mikaba ya akina mama.
Waloiba mabilioni wantembea vifua mbele.
Wanaua watu kwa kuwagonga na magari yao au kuwatwanga risasi za vichwa wanapeta vifua mbele.
Jela ni ya masikini na watu duni au wale wanaopinga ubabe serikali na ufisadi wake.
Kuna aelfu ya wauaji na wezi wa mabilioni wapo wanatembea kama watakatifu wakisubiri mataji ya uzima wa milele.

Kama Lowassa angekuwa na makosa ambayo tunataka ahukumiwe basi asingekuwa Bunge, asingekuwa mjumbe wa NEC - CCM, asingekuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Lowassa angefunguliwa mashitaka tungejua kweli ana makosa.

hapa ni kulionea kanisa kwa kumtumia Lowassa wakati chama chake hakijathibitisha hilo ama kwa kumfungulia mashitaka au kumpokonya uanachama. Kwa nini tunataka kanisa ndilo limuadhibu Lowassa wakati kisiasa haijawekwa wazi kama ni fisadi/si muadilifu?

Kama si mwadilifu angeendelea kukitumikia chama chake?
 
Kama makanisa yanakubali fedha kutoka kwa mafisadi, kitu gani kitawazuia kufanya biashara ya madawa ya kulevya yanayoingiza pesa nyingi zinazoweza kutumika kujenga jimbo jipya?The Roman Catholic church is indicting itself!!
wewe kila jimbo linajengwa kutokana na michango ya waumini, tuna harambee za kila mwezi kwa ajili ya kujenga hayo makisa na hizo dawa za kulevya labda wewe ndo mnunuzi wa hizo dawa ndo mana unahisi tunauza dawa za kulevya, pesa za waumini ndo zinazojenga makanisa, shule na hospital. amia katoliki ndo utaelewa kinachofanyika.
 
Lowassa amekwenda kuungama kwa Mchungaji Emmanuel Joshua na alikwenda Hija Israel labda anajutia makosa yake kama ni kweli yapo.
 
Ndugu yangu Isango nakujua wewe umepata kusoma seminari, mara hii umesahau kuwa kanisa halimuhukumu mtu kwa kuwa tu wewe unamtuhumu!!! halafu pia mtu hata kama ana dhambi lakini kuna maungamo ambayo ni ya siri..! hakuna dhambi ndogo na kubwa wala sadaka kubwa na ndogo, hebu kumbuka mara ngapi tumezini, mara ngapi tumesengenya, mara ngapi tumedanganya au umetukana na kuwaza mabaya !!!!! bila mie kujua umetubu ama hujatubu lakini bado kanisa linapokea sadaka yako na wakati mwingine kushiriki meza ya Bwana. jamani tusitake kanisa lifanya kazi Kidunia kama mfanyavyo ninyi. hata mamlaka zenyewe zilizopewa haki kisheria kudeclare kuwa somebody is.guilty hazijawahi kufanya hivyo??? Ahhhhh.... hata kama humpendi Mzee EL lakini usilisakame kanisa kwa kuwa lipo kwa ajili ya kila aitwaye binadam
 
Nenda katafute kitabu kinaitwa IN GODS NAME ndo utajua uchafu wa vatican.
labda uwe mpagani mana kila dhehebu watu wanasema lina uchafu wake hata hilo dhehebu ulilokuwa nalo lina uchafu wake.
 
Bado narudia,
Kanisa katoliki hawajakurupuka, ni watu walio makini sana. Waamuacha sio Aamuacho, ni jopo linaamua. Hivyo naamini kabisa Kanisa Katoliki limejishibisha juu ya tuhuma zote juu ya Lowassa, linajua anahusikaje au hahusikaje.
Kanisa Katoliki linaye waziri mkuu aliye madarakani ambaye ni muumini wake, je halikumuona na kumualika aende pale na ving'ora na wapambe lukuki?
Hawa jamaa naamini fika WANAJUA WAFANYALO, NA WAKIAMUA KUYAWEKA BAYANA JUU YA SAKATA LA KUCHAFULIWA EL...nchi itayumba. Hawajakurupuka RC, ndio maana tangu sakata la EL lilipoanza jamii haijawahi kupokea karipio lao kupitia kwa Ruzoka etc.
Hakuna justification yeyote kwa Kanisa Katoliki kumtumia EL.Tunajua huyu anatuhuma ambazo hajawahi kukanusha na wananchi tukiwemo waamini wa RC tunaamini zipo hoja za msingi.kama kanisa limeona hana hatia wamsafishe wao basi ili tujue sababu! Michango ni ya sisi waamini na kanisa ni letu sote sasa ni kwa maono gani kanisa kumtumia huyu kila jimbo tena mtu mwenye tuhuma zisizo na majibu? Kanisa halina watu wa kufanya hayo zaidi ya EL? Kama leo kanisa linasema haliwezi kuhukumu mtu wanasahau elimu waliyotupa kipindi cha uchaguzi? Zile sifa huyu El yupo? Sasa anaitwa kwenye harambee kama nani? Wanafikiri tumesahau kauli ya askofu kule mwanza kuhaidi kumsaidia El kujijenga? Kanisa limepotoka na tutawaambia ukweli!
 
Mafisadi,Majambazi,Wezi Polisi wauaji na wandava wote wanaoishi na kula kwa kukiuk sheria za nchi, kwetu Tanzania ni Macelebrity kama wale wa Hollywood kule California.

Huu usingizi tulio lala sijui tutaamka lini?
 
Kashfa ya Richmond Lowassa kasema hahusiki bali aliwajibika kuinusuru serikali na chama chake. Vyombo vya habari vilisema msimamo huu aliutoa kwenye mkutano wa NEC - Dodoma. Hakuna aliyekanusha msimamo huu wa Lowassa na kwa kawaida taarifa isipokanushwa inakuwa na asilimia kubwa ya kuwa ni kweli.

Kanisa linahusika vipi kumhukumu Lowassa?
 
Bado narudia,
Kanisa katoliki hawajakurupuka, ni watu walio makini sana. Waamuacha sio Aamuacho, ni jopo linaamua. Hivyo naamini kabisa Kanisa Katoliki limejishibisha juu ya tuhuma zote juu ya Lowassa, linajua anahusikaje au hahusikaje.
Kanisa Katoliki linaye waziri mkuu aliye madarakani ambaye ni muumini wake, je halikumuona na kumualika aende pale na ving'ora na wapambe lukuki?
Hawa jamaa naamini fika WANAJUA WAFANYALO, NA WAKIAMUA KUYAWEKA BAYANA JUU YA SAKATA LA KUCHAFULIWA EL...nchi itayumba. Hawajakurupuka RC, ndio maana tangu sakata la EL lilipoanza jamii haijawahi kupokea karipio lao kupitia kwa Ruzoka etc.

Kufuatana na maelezo yako inaelekea unaamini kuwa kanisa Katoliki haliamini kabisa kuwa kulifanyika ufisadi katika kutoa tenda ya kufua umeme iliyopewa kampuni hewa ya Richmond? Kama ni hivyo kwanini alijiuzuru ili hali anajua hakuhusika; na kwanini barua yake ya kujiuzuru ikakubaliwa na Rais ambae Lowassa anamtuhumu kuwa alijua maamuzi aliyoyafanya? Hukumu ya vitendo vibaya alivyotufanyia Lowassa wananchi ataipata hapa hapa duniani na wala sio ahera!!Kujiuzuru eti kwasababu ya kukinusuru chama na serikali yake ni kukili kuwa makosa yalitendeka otherwise kwanini inusurike?
 
Pesa kiti ingine wasee! nani aachie mshiko wa bure kila kanisa na msikiti sasa hivi wapiga chapuo kumwalika mzee mzima kabla fungu halijakata; hata sisi pale usharikani sinza tutamwalika EL,na mimi nitaongoza pambio languvu toa ndugu toa ndugu ulichonacho wewe bwana anakuona mpaka rohoni mwakoX70 pesa kitu ingine waseeeeeeeeeeeeeee
 
kanisa lilikuwa linapiga kelele gani za ufisadi? Hao mafisadi ni akina nani?jamani wote tunalipenda kanisa lakini tuwe wakweli kwa dhamira iliyo safi hapa kuna tatizo tena si dogo!
 
MODS hii mada ni muhimu msiifunge sababu ya comments za udini za wachache,futeni comments za udini tu! Tujadili swala hili muhimu!
 
Kanisa Katoliki limejichanganya, ndo maana mimi binafsi kama mkatoliki niliyebatizwa, nikapa komunio na kipaimara hatimaye ndoa kwenye dini hii NIMEAMUA KUTOFUNGA KWARESIMA KWA KULAANI KITEND CHA KUMKARIBISHA HUYU FISADI AKARIBIE ALTARE YETU. Nitasali NOVENA kwa ajili hii (wakatoliki wanajua novena ni nini).

Kwenye familia yanetu kuna kaka, dada na wadogo zangu ambao wamewekewa wakfu. Kifupi hili kanisa linafumbia dhambi nyiingi san linapokuja swala la pesa, kwa kusingizia usimhukumu binadamu mwenzio. Ila watakunyanyasa kama hutoi zaka na saa nyingine hata ukifiwa padri hawezi kuja kusalia maiti kwa sababu hiyo.

Narudia sifungi ten kwaresima hadi ipite 2015, na kama rais anakuwa Lowasa naaha dini nakuwa kafiri.
 
Back
Top Bottom