Kampuni/ ofisi kutokuwapa likizo wafanyakazi wake

linguistics

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
4,701
4,325
Habarini Great Thinkers
Kwa wale wanaofahamu vizuri sheria za kazi. Kuna ndugu yangu anafanya kazi kwenye ofisi moja Dar mwajiri wao hawapi likizo ya mwaka. Ana miaka zaidi ya 10 hajawahi kupata likizo kwa kuwa hakuna huo utaratibu wa kuomba likizo. Naombeni ushauri afanyeje ili bosi wake afate taratibu na sheria za kazi?

Nawasilisha
 
hivi unajua kuna watu wananunua likizo za employee...kama zinanunuliwa asilalamike, if not..aende akaombe likizo, lkn miaka 10 yote hy, ni kwamba hajataka kuomba, usiingilie kazi za watu
 
Habarini Great Thinkers
Kwa wale wanaofahamu vizuri sheria za kazi. Kuna ndugu yangu anafanya kazi kwenye ofisi moja Dar mwajiri wao hawapi likizo ya mwaka. Ana miaka zaidi ya 10 hajawahi kupata likizo kwa kuwa hakuna huo utaratibu wa kuomba likizo. Naombeni ushauri afanyeje ili bosi wake afate taratibu na sheria za kazi?

Nawasilisha

ni kampuni gani hiyo?
 
Kila mfanyakazi alieajiriwa kwenye secka rasmi, baada ya kufanya kazi kwa muda usiopungua miezi 12, anahaki ya kuomba na kupata likizo ya mwaka ya muda usiozidi siku 28 kila mwaka. Ila ni lazima aiombe mwenyewe. Kama asipoomba likizo ndani ya mwaka, na mwaka ukapita, the atakua amepoteza hiyo haki yake.
 
kuna watu wengine janja janja wanachukua likizo lkn hawashirikishi ndugu zao........anaenda kufanya mambo yake mengine...... ww ndugu unajua mtu anaenda kazini kumbe wala
 
Hakuna kitu kama hicho..

Hataki mmfatilie kwenye mamvo yake ndo maana anawambia hakuna likizo.
 
Je huyo ndugu yako ana mkataba wa Ajira au barua ya ajira?? Je barua hiyo inasema nini kuhusu likizo?? Nashauri anzia kwanza kuuona mkataba wake wa ajira ndio uingie kipengele cha likizo. Unaweza kulalamika likizo kumbe ndugu yako hana hata mkataba wa ajira ama likizo zake analipwa kwa mujibu wa mkataba wake. Endapo anao mkataba na umeweka wazi kua anastahili likizo. Tafuta nakala ya sheria ya ajira na mahusiano Kazini ya Mwaka 2004 iko wazi juu ya stahili ya likizo.
 
Hapo mleta mada hajafafanua vizuri.
Mara anasema hawapi likizo,ikiwa ni wengi,mara ndugu yake hampi likizo ikiwa ni peke yake.

Mie naona kwamba huyu atakuwa kibarua na hana mkataba
Na pili watu wengi hununua likizo na wengine pia ni uelewa mdogo mtu anaonaa akienda likizo day worker atakula ajira na kaumua kukomaa.
Ila kama yupo hapo kwa miaka kumi hiyo ni ajira tosha,anaweza kupata msaada zaidi.
 
Back
Top Bottom