Kampuni nzuri ya kuagiza magari japani

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,611
4,354
Mimi leo nitaongelea kamapuni moja tu inaitwa NIKKYO ambayo imenipa huduma nzuri mimi na marafiki zangu. Nimesha agizia marafiki zangu watatu kwa kupitia kampuni hii ya Kijapani ijulikanayo kama NIKKYO
www.nikkyocars.com

Hii kampuni haina jina kubwa Tanzania ila nilipata recommendation kwa rafiki yangu anaishi nchini Kenya
Baada ya kuifuatilia niligundua kuwa ipo kwenye Biashara tangu mwaka 1995 hivyo ni wazoefu wa Biashara ya Magari

Sifa zake nilizo ziona:
  1. Wana wasiliana na wateja kwa haraka na kwa usahihi
  2. Magari yao hufanyiwa service kabla ya kusafirishwa hivyo ukipokea huna haja ya kwenda tena garage; wewe ni kujaza mafuta na kuondoka
  3. Wanauza magari yaliyokwenye hali nzuri; usitegemee kupata magari mabovu (mikweche kwao)
  4. Gharama zao zinaendana na ubora wa magari yao (kumbuka rahisi ni Ghali)
  5. Kama huna uzoefu wa magari, unaweza kutoa sifa ya gari unayoitaka na hivyo kupata ushauri wa bure kabisa na wa kiufundi kutoka kwa mafundi wabobezi
  6. Kununua gari NIKKYO huhitaji dalali wala mtu wa kati; unachotakiwa ni kujua kiingereza kidogo tu na mengine unafanya mwenyewe
  7. Unapata taarifa zote zinazo husu gari lako na shipping details. Unaweza kulifuatilia gari lako likiwa kwenye meli hadi linafika Dar na hata ukitaka ufikishiwe mkoani (ila utachangia ziada)
Kwa muda wote nilikuwa na wasiliana na Manager mauzo wa Afrika Mashariki (Zia Obaid) ambaye ni msomi mzuri wa mambo ya biashara na yupo friendly sana.
Yaani unafanya biashara kama vile upo naye hapa Dar Es Salaam (kwa simu, whatsApp, Skype na Email)

Unaweza kuwasiliana na Zia Obaid kupitia;
  • WatsApp # +81 80 5985 6023
  • Skype name; Nikkyo_ Obaid Zia
Email: zia.obaid@nikkyocars.com

Najua yapo makampuni mengine maarufu huku mjini ila leo nimeamua kuongelea uzoefu nilioupata kwa hii kampuni
Angalizo: mimi sifaidiki chochote na hii kampuni ila nitasikitika kusikia mtu kapoteza hela kwa kununua gari bovu au kuibiwa hela wakati tungeweza kumsaidia BURE!
 
Umeacha jambo la muhimu kuliko yoote, ni kwamba bei zao sio rafiki kwa wanunuzi wengi wa Kitanzania.
 
Umeacha jambo la muhimu kuliko yoote, ni kwamba bei zao sio rafiki kwa wanunuzi wengi wa Kitanzania.
Biashara huwasaidia sana wale wanaojua hesabu; mfano, uwekewe tairi mpya zote 4 OG kutoka Japani halafu uongezewe dola 100; au uwekewe batrii mpya OG halafu uongezewe dola 35; na service nyingine; Nafikiri ni wale wanao chambua mambo watao nielewa
Mimi nimetoa mtazamo wangu ikikupendeza wajaribu. mwandishi wa mashairi - Shaaban Robert alisema "rahisi ni Ghali"
Lakini usisahau kuwa kuna vilio huko mtaani kwa watu kununua mikweche kutoka japani kwa kuangalia bei poa
Huu ni ushauri tu, kuufuata au kuto ufuata ni uamuzi wako
 
Biashara huwasaidia sana wale wanaojua hesabu; mfano, uwekewe tairi mpya zote 4 OG kutoka Japani halafu uongezewe dola 100; au uwekewe batrii mpya OG halafu uongezewe dola 35; na service nyingine; nafikiri ni wale wanaochambua mambo watanielewa.
Mimi nimetoa mtazamo wangu ukikupendeza wajaribu
Lakini usisahau kuna vilio huko mtaani wa watu kununua mikweche kutoka japani kwa bei poa
Huyo anaelia gari ya miaka 10+ iliopita kuwa mkweche ana matatizo. Tusijidanganye ukinunua USED car na kuiita mpya hakuifanyi mpya. Na kwasababu ni used tegemea lolote. Uzuri kampuni Nyingine zinaweka wazi, kama tairi kipara utaliona,kama kuna scratches wanakuonesha ni wewe tu
 
Biashara huwasaidia sana wale wanaojua hesabu; mfano, uwekewe tairi mpya zote 4 OG kutoka Japani halafu uongezewe dola 100; au uwekewe batrii mpya OG halafu uongezewe dola 35; na service nyingine; nafikiri ni wale wanaochambua mambo watanielewa.
Mimi nimetoa mtazamo wangu ukikupendeza wajaribu
Lakini usisahau kuna vilio huko mtaani wa watu kununua mikweche kutoka japani kwa bei poa
Ttzo utamaduni wa idadi kubwa ya watanzania si wa huko kuchambua mambo

Ila hitimisho lako ndo zuri kuwa ikitupendeza tuwajaribu
 
Biashara huwasaidia sana wale wanaojua hesabu; mfano, uwekewe tairi mpya zote 4 OG kutoka Japani halafu uongezewe dola 100; au uwekewe batrii mpya OG halafu uongezewe dola 35; na service nyingine; nafikiri ni wale wanaochambua mambo watanielewa.
Mimi nimetoa mtazamo wangu ikikupendeza wajaribu. mwandishi wa mashairi - Shaaban Robert alisema "rahisi ni Ghali"
Lakini usisahau kuwa kuna vilio huko mtaani kwa watu kununua mikweche kutoka japani kwa bei poa
Na sio kuifanyia yoote haya uliyoyaorodhesha gari itakuwa mpya,itabaki ni mtumba ambao unaweza kukusumbua tuu

Ila tusikukatishe tama kwenye tangazo lako,tutawajaribu
 
Na sio kuifanyia yoote haya uliyoyaorodhesha gari itakuwa mpya,itabaki ni mtumba ambao unaweza kukusumbua tuu

Ila tusikukatishe tama kwenye tangazo lako,tutawajaribu
nitaweka maka la nyingine ya nilicho jifunza Be foward
 
Hiyo promo mm imenitisha. Uzoefu wa makampuni mengine wanakuelezea condition ya gari kama ilivyo na hawachukui risk ya kufanyia maboresho yoyote. Na endapo utaikuta tofauti na hali uliyoelezwa (exception kwa demage zinazoweza tokea wakati wa shipping au wizi wa vifaa kwa baadhi ya bandari ambapo DSM pia inatajwa) wanakurudishia fidia ya pesa yako. Hii ya kufanyia service huwezi kum-sue MTU popote endapo utakuta tofauti. Na mm pia nimeshaagiza sana magari mkuu.
 
Back
Top Bottom