Naombeni msaada wazoefu wa kuagiza magari Japan

Joyce wohwoh

Member
Sep 17, 2021
78
180
Naombeni msaada wazoefu wa kuagiza magari Japan.

Nimeagiza gari japan limefikia hatua wamepakia kwenye meli na wamenijulisha jina la meli, tarehe ya kuondoka na kufika japo wamenambia huwa zinabadilika sometimes.

Sasa utata uko hapa sijatumiwa TRACKING NUMBER.ili niweze kufatilia meli iko wapi. Wazoefu je ninatakiwa itumwe lini?
 
Kwenye documents panakuwa na jina la Meli pamoja na voyage no.. ukiweka details za meli kwa maana Meli au voyage no kwenye search engine kama google utapata details ya location ya meli.

Kama una wasiwasi unaweza kwenda kwa agent wa hiyo meli Shipping line wakakupa details.

Incase bado hujapata wakala yaani Clearing and Forwading agent nakukaribisha kufanya kazi na mimi kwa bei ya punguzo
 
Naombeni msaada wazoefu wa kuagiza magari Japan.Nimeagiza gari japan limefikia hatua wamepakia kwenye meli na wamenijulisha jina la meli,tarehe ya kuondoka na kufika japo wamenambia huwa zinabadilika sometimes.sasa utata uko hapa sijatumiwa TRACKING NUMBER.ili niweze kufatilia meli iko wapi.wazoefu je ninatakiwa itumwe lini?
Hawajakutumia document yoyote?
 
Yah bado sijatumiwa document yoyote,wameniambia watanitumia Bill of Landing through DHL.
Siyo landing mkuu, inaitwa Bill of Lading (BoL). Kwa vile wamekujulisha jina la meli na namba yake unaweza kuingia google ukaigugu hiyo meli. Utaona kwenye ramani kila kituo inapofika!
 
Mkuu kama uko mbali na Dar (yaani uko mikoani), kwenye kufanya malipo ya kodi na ushuru mbali mbali usije ukarogwa ukamtumia mtu hela ya kulipa eti akulipie, haki ya nani utapigwa cha juu mpaka uchanganyikiwe. Wajinga huwa wanachakachua zile document za charges ili uone ushuru uko juu. Mimi niliwastukia maana walitaka kunipiga pamoja na kwamba dogo aliyekuwa anashughulikia alikuwa mtoto wa shemeji yangu. Dar hakuna watu!

Mara ya kwanza akaniambia kwa mdomo kabla gari halijafika sijui port charges, wharfage, shipping line, TBS inspection, C&F agency fee. Kote huko wanaongeza gharama sasa kama unajidai kuwaamini utawatumia pesa ujue umeumizwa. Sasa nilichofanya gari ilipofika nikaenda na mimi mwenyewe, dogo akanipeleka kwa hao dealers (X), wakajichanganya wakanipa mahesabu tofauti na aliyonitamkia kwa mdomo huyo dogo.

Alipoiangalia ile document waliyonipa yenye mchanganuo nikamsikia dogo anaweka msisitizo mbona imekuwa tofauti hivyo utakuwa umetoa sheet nyingine siyo ile, hapo hapo halmashauri ya kichwa ikacheza, nikajiongeza kwamba hapa nataka kupigwa!

Maana walitaka niwape hiyo hela walipe wenyewe eti mimi niende tu hotelini nisubiri gari itoke usiku. Nikaweka msisitizo hela yangu silipi kwa cash nitakuwa nalipa kwa control number kadri ninavyopata documents Bandari na TRA. Ha ha ha haaaaa wakalowa vibaya sana.

Mwisho wa siku nakuja kulinganisha mahesabu waliyonipa na document za serikali nakuta walikuwa wamenipiga 500k na usheeee! Shenzy kabisa!!
 
Google vesselfinder.com
Then ingiza jina la Meli waliokutajia utaona Meli imefika wapi

Hongera realmotor wako vizuri magari mazuri bei chee
 
Acha na hii mambo ya kuagiza gari nje. Nenda yard kuna maga mengi mazuri na ya viwango unavyotaka. Pili mpaka gari ikufikie gharama zitakuwa kubwa sana kuliko ungeenda kununua yard. Kama upo na cash kanunue live bila chebga unachagua kama mtumba.
 
Daah asante sana kwa mawazo haya hawa watu wanatupiga sana hasa wa mikoani maana tuko mbali,shukrani mkuu.
Siyo landing mkuu, inaitwa Bill of Lading (BoL). Kwa vile wamekujulisha jina la meli na namba yake unaweza kuingia google ukaigugu hiyo meli. Utaona kwenye ramani kila kituo inapofika!
Asante mkuu.
 
Acha na hii mambo ya kuagiza gari nje. Nenda yard kuna maga mengi mazuri na ya viwango unavyotaka. Pili mpaka gari ikufikie gharama zitakuwa kubwa sana kuliko ungeenda kununua yard. Kama upo na cash kanunue live bila chebga unachagua kama mtumba.
Ushauri wa hovyo huu! Wote walioagiza gari kutoka Japan watakuwa mashahidi kwa hili. Gari ya Yard iko juu kuliko ya kuagiza.
 
Back
Top Bottom