Kampeni chafu zaanza UVCCM

Date::11/21/2008
Kampeni chafu zaanza UVCCM
Exuper Kachenje
Mwananchi

KAMPENI chafu na za kupakana matope zimezuka miongoni mwa makundi ya wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM imebainika.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Mwananchi inazo, wagombea hao kwa upande mmoja, wamekuwa wakiendesha kampeni chafu za chuki na kupakana matope kwa misingi ya rangi.

Habari za uhakika zilizoifikia Mwananchi zinaeleza kuwa, kumezuka kundi ambalo kwa makusudi linaendesha kampeni za kumpaka matope mmoja wa wa wagombea wa nafasi hiyo kwa kusambaza ujumbe mchafu kumhusu yeye kwa njia ya simu selula na kueleza kuwa UVCCM, ipo hatarini kutekwa na maharamia.

"Wanafanya hivyo kwa kasi chini ya ufadhili wa mgombea mwinigine wa nafasi hiyo ya juu ya uongozi katika UVCCM," kilieleza chanzo cha habari hizi

Habari zaidi zinabainisha kuwa, anayekusudiwa kupakwa matope na kuchafuliwa ni Hussein Bashe, mgombea mwenye asili ya kisomali ambaye Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ilipitisha jina lake kugombea nafasi hiyo.

Sehemu ya ujumbe huo ulisomeka: " Kama meli za mfuta zinavyotekwa na maharamia ya kisomali vivyo hivyo wana CCM tuwe macho, kwani UVCCM iko hatarini kutekwa na maharamia hao wa kisiasa toka ughaibuni. Shime Watanzania wenzangu tuamke tusikubali kuongozwa na ma-tx."

Akizungumzia tukio hilo, Hussein Bashe alisema kuwa wanaosambaza ujumbe huo wamefilisika kisiasa na kwamba badala ya kupoteza muda kwa kupakana matope waeleze wataisaidia nini UVCCM.

"Wanaosambaza ujumbe huo wamefilisika kisiasa, waeleze wataisaidia nini jumuia. Hata mwalimu Nyerere aliwahi kusema: watu waliofilisika kisiasa hukimbilia mambo madogo madogo yasiyo na msingi," alisema Bashe.

Well, ingawa nachukia sana siasa hizi za kikaburu lakini ni muhimu wasomaji wakajua kuwa Hussein Bashe alikuwa na bado mpambe mzuri sana wa ROSTAM AZIZI ambaye alikuwa bosi wake wakati Hussein akifanya kazi katika kampuni ya Mwananchi Communications inayomiliki gazeti hili liloandika hii habari.

Hussein Bashe mwenye ufadhili mkubwa wa ROSTAM na anayetokea mkoa wa TABORA alihusika kwa namna fulani katika kufanikisha zile siasa chafu za kibaguzi dhidi ya Dr Salim Ahmed SALIM.

Wanasema...........

Tanzanianjema
 
Fedha ya wizi iliwapa nguvu CCM na kutwaa madaraka ya kuiongoza nchi sasa fedha hiyohiyo imegeuka kuanza kuwatafuna wenyewe.
Udhaifu siku zote huzaliwa pale penye uimara na palipo egemeo kuu, Fedha haramu.

Kile kiwatiacho nguvu CCM ndicho kitakachowaliza wabakie jivu la kumwagwa Bahari ya Hindi.
 
Well, ingawa nachukia sana siasa hizi za kikaburu lakini ni muhimu wasomaji wakajua kuwa Hussein Bashe alikuwa na bado mpambe mzuri sana wa ROSTAM AZIZI ambaye alikuwa bosi wake wakati Hussein akifanya kazi katika kampuni ya Mwananchi Communications inayomiliki gazeti hili liloandika hii habari.

Hussein Bashe mwenye ufadhili mkubwa wa ROSTAM na anayetokea mkoa wa TABORA alihusika kwa namna fulani katika kufanikisha zile siasa chafu za kibaguzi dhidi ya Dr Salim Ahmed SALIM.

Wanasema...........

Tanzanianjema

Tanzania Daima

Inaonyesha huna taarifa sahihi juu ya hili awali ni kuunge mkono kuchukia ubaguzi na kuuita ni ukaburu.

Juu ya ulicho ongea si kweli 2005 Bashe alikua mfanyakazi wa mwananchi bali kipindi hicho alikua mfanyakazi wa kampuni ya CELTEL.

Swala la uhusiano wao hatuwezi kuutazama kwa kuwa wametoka mkoa mmoja BASHE 2007 alihujumiwa na walokua wana mtandao na jina lake likapotea ktk mazingira ya kutatanisha ingawa wachunguzi wa Duru waligundua kua bwana huyu alishinda NEC na alipata kura ZAIDI ya 1000 lakini samweli sita chini ya maelekezo ya ROSTAM AZIZI jina likafichwa na kusababisha ukumbi kupiga kelele lakini jina likapotea.

Bashe 2005 alihujumiwa ktk uchaguzi wa jimbo nzega na Bwana Rostam akimsaidia bwana Seleli,pia 2007 Bashe alitofauutiana na Bwana Rostam katika uchaguzi wa Mkoa wa Tabora Bashe akimsaidia Mzee anaeitwa Nkumba walitofautiana

Naeleza haya ili usipotoshe watu si kweli kua huyu bwana ni mpambe wa Rostama AZIZI.
 
..conspiracy..
 
Ningepata nafasi ya kukaa nae na kumshauri( japo nahisi hashauriki), 'Ningemwomba' akae pembeni apumzike! Si vema kujishuhudia ukifa kwenye kifo kibaya kama cha moto au maji!
 
Na Simon Mhina

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema utaendelea kupokea fedha kutoka kwa wafadhili bila kujali zimetoka wapi au mfadhili amezipata kwa njia gani.

Akizungumza na Nipashe Makao Mkuu ya Umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji Charles Charles alisema UVCCM haikuwa na sababu ya kuchunguza wala kusita kupokea fedha za kugharamia uchagizi toka kwa kada wao Tanil Somaiya, kwa vile hawana vyombo vya dola.

Charles ametoa kauli hiyo kujibu msimamo uliotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jerry Slaa ambaye alisema hatua ya Somaiya kuamua kugharamia uchaguzi huo kwa Sh. milioni 400 ilikuwa na walakini.

``Mtu yeyote ambaye anaamua kutusaidia, hatuna sababu ya kuanza kuchunguza vyanzo vya mapato yake ili mradi tu awe anafuata taratibu za kutoa mchango. Kazi ya kumchunguza mtu kuwa kapata wapi fedha hatuwezi kuifanya sisi,`` alisema.

Alisema si haki kuhoji ni vipi mfanyabiashara huyo anachangia UVCCM pekee na kuacha jumuiya nyingine, kwani mfadhili ndiye siku zote huamua fedha zake azipeleke wapi.

``Kumtuhumu Somaiya eti kwanini kama ana mapenzi na CCM asichangie jumuiya nyingine, ni upungufu mkubwa wa kuwaza na kupembua mambo na pia ni udhaifu wa fikra na upeo wa kisiasa,`` alisema.

Charles alisema Somaiya alikuwa mjumbe katika kamati ya kutafuta fedha za kugharamia uchaguzi huo na ni mmoja wa watu walioombwa kuchangia.

``Mbali na hivyo, siku zote mtoaji hachaguliwi wapi apeleke fedha zake, bali anaamua mwenyewe,`` alisema na kuongeza ``huenda Jumuiya nyingine hazikumuomba ndio maana hakuzichangia``.

Alisema ameshangazwa na kauli hiyo ya Slaa, ambao kwa kiasi kikubwa inafanana na ile ya Mkurugenzi wa Vijana (Chadema), John Mnyika.

Alisema kama kweli Slaa anaona Somaiya ni fisadi, basi amripoti kwenye vyombo vya dola.

Pia alisema Slaa akiwa mjumbe wa vikao vya CCM alipaswa kupeleka malalamiko yake huku badala ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Akijibu `madongo` hayo, Slaa alisema Charles hajui kitu kwa vile licha ya kwamba amerukia jukwaa la CCM hivi karibuni akitokea upinzani, lakini pia majibu yake kwamba UVCCM inapokea fedha popote bila kuchunguza uhalali wake, yanaonyesha jinsi `shule` ilivyompiga chenga.

``Huwezi ukapokea fedha tu kwa chombo cha watu kama UVCCM, huyu haelewi kwamba kuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, nadhani haya ni matatizo ya elimu, tunashukuru yupo CCM tutamfundisha kidogo kidogo ataelewa. Lakini wakati anajifunza, asiwe mpayukaji, anatutia aibu,`` alisema.

Slaa alisema anachopigia kelele sio hatua ya UVCCM kuchukua fedha haramu za Somaiya, lakini anahoji ni vipi umoja unashindwa kujigharamia hadi watokee wafadhili.

``UVCCM ndipo chimbuko la viongozi hivyo, ninahofu kwa mtindo huu tunazalisha viongozi ombaomba hata watakapokuwa serikalini,`` alisema.

Alisisitiza kwamba, Somaiya si mtu safi na hatua yake ya kumwaga fedha UVCCM inalenga kufunika tuhuma dhidi yake.
SOURCE: Nipashe

Hawa ndio viongozi wetu: Im out of words...
 
Like a son like a father. Hakuna cha ajabu hapo isipokuwa wameamua kusema ukweli tu kwani wamekuwa wakipokea fedha chafu kwa muda mrefu tu.
 
Tutapokea fedha bila kujali zinakotoka-UVCCM

2008-11-24 09:59:56
Na Simon Mhina

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema utaendelea kupokea fedha kutoka kwa wafadhili bila kujali zimetoka wapi au mfadhili amezipata kwa njia gani.

Akizungumza na Nipashe Makao Mkuu ya Umoja huo jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji Charles Charles alisema UVCCM haikuwa na sababu ya kuchunguza wala kusita kupokea fedha za kugharamia uchagizi toka kwa kada wao Tanil Somaiya, kwa vile hawana vyombo vya dola.

Charles ametoa kauli hiyo kujibu msimamo uliotolewa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jerry Slaa ambaye alisema hatua ya Somaiya kuamua kugharamia uchaguzi huo kwa Sh. milioni 400 ilikuwa na walakini.

``Mtu yeyote ambaye anaamua kutusaidia, hatuna sababu ya kuanza kuchunguza vyanzo vya mapato yake ili mradi tu awe anafuata taratibu za kutoa mchango. Kazi ya kumchunguza mtu kuwa kapata wapi fedha hatuwezi kuifanya sisi,`` alisema.

Alisema si haki kuhoji ni vipi mfanyabiashara huyo anachangia UVCCM pekee na kuacha jumuiya nyingine, kwani mfadhili ndiye siku zote huamua fedha zake azipeleke wapi.

``Kumtuhumu Somaiya eti kwanini kama ana mapenzi na CCM asichangie jumuiya nyingine, ni upungufu mkubwa wa kuwaza na kupembua mambo na pia ni udhaifu wa fikra na upeo wa kisiasa,`` alisema.

Charles alisema Somaiya alikuwa mjumbe katika kamati ya kutafuta fedha za kugharamia uchaguzi huo na ni mmoja wa watu walioombwa kuchangia.

``Mbali na hivyo, siku zote mtoaji hachaguliwi wapi apeleke fedha zake, bali anaamua mwenyewe,`` alisema na kuongeza ``huenda Jumuiya nyingine hazikumuomba ndio maana hakuzichangia``.

Alisema ameshangazwa na kauli hiyo ya Slaa, ambao kwa kiasi kikubwa inafanana na ile ya Mkurugenzi wa Vijana (Chadema), John Mnyika.

Alisema kama kweli Slaa anaona Somaiya ni fisadi, basi amripoti kwenye vyombo vya dola.

Pia alisema Slaa akiwa mjumbe wa vikao vya CCM alipaswa kupeleka malalamiko yake huku badala ya kuzungumza na vyombo vya habari.

Akijibu `madongo` hayo, Slaa alisema Charles hajui kitu kwa vile licha ya kwamba amerukia jukwaa la CCM hivi karibuni akitokea upinzani, lakini pia majibu yake kwamba UVCCM inapokea fedha popote bila kuchunguza uhalali wake, yanaonyesha jinsi `shule` ilivyompiga chenga.

``Huwezi ukapokea fedha tu kwa chombo cha watu kama UVCCM, huyu haelewi kwamba kuna sheria ya kudhibiti fedha haramu, nadhani haya ni matatizo ya elimu, tunashukuru yupo CCM tutamfundisha kidogo kidogo ataelewa. Lakini wakati anajifunza, asiwe mpayukaji, anatutia aibu,`` alisema.

Slaa alisema anachopigia kelele sio hatua ya UVCCM kuchukua fedha haramu za Somaiya, lakini anahoji ni vipi umoja unashindwa kujigharamia hadi watokee wafadhili.

``UVCCM ndipo chimbuko la viongozi hivyo, ninahofu kwa mtindo huu tunazalisha viongozi ombaomba hata watakapokuwa serikalini,`` alisema.

Alisisitiza kwamba, Somaiya si mtu safi na hatua yake ya kumwaga fedha UVCCM inalenga kufunika tuhuma dhidi yake.

SOURCE: Nipashe
 
Tanzania Daima

Inaonyesha huna taarifa sahihi juu ya hili awali ni kuunge mkono kuchukia ubaguzi na kuuita ni ukaburu.

Juu ya ulicho ongea si kweli 2005 Bashe alikua mfanyakazi wa mwananchi bali kipindi hicho alikua mfanyakazi wa kampuni ya CELTEL.

Swala la uhusiano wao hatuwezi kuutazama kwa kuwa wametoka mkoa mmoja BASHE 2007 alihujumiwa na walokua wana mtandao na jina lake likapotea ktk mazingira ya kutatanisha ingawa wachunguzi wa Duru waligundua kua bwana huyu alishinda NEC na alipata kura ZAIDI ya 1000 lakini samweli sita chini ya maelekezo ya ROSTAM AZIZI jina likafichwa na kusababisha ukumbi kupiga kelele lakini jina likapotea.

Bashe 2005 alihujumiwa ktk uchaguzi wa jimbo nzega na Bwana Rostam akimsaidia bwana Seleli,pia 2007 Bashe alitofauutiana na Bwana Rostam katika uchaguzi wa Mkoa wa Tabora Bashe akimsaidia Mzee anaeitwa Nkumba walitofautiana

Naeleza haya ili usipotoshe watu si kweli kua huyu bwana ni mpambe wa Rostama AZIZI.

Kaka kazi ya propaganda humu huiwezi. Nakushauri kwanza uende ukamjibu Nape Nnauye kwenye ule uwongo wako mwengine katika thread inayodai kuwa yeye anamuunga mkono/anakuunga mkono (BASHE). Yaani huwezi hata kuangalia kama kuna mtu anaweza kuaamini kuwa NAPE NNAUYE kumuunga mkono mgombea wa MTANDAO MASLAHI.

Salam wote kambini...

Tanzanianjema
 
Watoto wa vigogo wapata ushindi kuongoza UVCCM
Na Waandishi Wetu
KATIKA hali inayoonyesha utaratibu wa kurithishana uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kushamiri , watoto wa vigogo kadhaa wa chama hicho akiwemo wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wamechaguliwa kushika nyadhifa mbalimbali kwenye Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM).

Matokeo ya uchaguzi huo yaliyopatikana jana kutoka mikoa mbalimbali, yameonyesha kuwa mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan Kikwete ni miongoni mwa viongozi waliochaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM taifa, akipata kura 274 kati ya 315 zilizopigwa.

Wengine waliochaguliwa na Ridhiwan kuongoza jumuiya hiyo mkoani Pwani na nyadhifa zao kwenye mabano ni Abdalah Ulega (mwenyekiti) na Mkomwa Mtiga (Mjumbe wa Mkutano Mkuu taifa).

Kwa mujibu wa matokeo hayo yaliyotangazwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, wengine waliochaguliwa kuongoza jumuya hiyo mkoani Pwani ni Josephat Msonde (Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM mkoa), Hilda Mzengo (Mwakilishi wa UWT) na mwakilishi wa wazazi mkoa, Siza Mjokaba

Mkoani Morogoro, mtoto wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, Lucy Nkya, Jonas Nkya, alichaguliwa kwa kura 290 kuwa Mwenyekiti wa Mkoa UVCCM.

Jonas aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wapinzani wake Musa Kingu ambaye ni ndugu wa katibu wa uchumi na fedha wa CCM Taifa, Amos Makala na Adela Ng'atigwa.

Nkya alishinda katika kura za marudio baada ya matokeo ya awali kushindwa kumtoa mshindi aliyepata zaidi ya nusu ya kura zote zilizopigwa.

Hata hivyo, Musa Kingu alibahatika kushinda nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM taifa, huku Pili Jabiri akijishindia nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM taifa.

Aliyechaguliwa kuwakilisha vijana UWT mkoani Morogoro ni Sepesina Lugalila, huku Masumbuko Igebya akichaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mkoa na Antony Muhando akiwawakilisha wazazi.

Amosi Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uchaguzi huo, aliwataka vijana kuwa na mshikamano na kutokubali kugawanywa na viongozi wachache ndani ya chama kwa kuwa vijana ndio nguzo kubwa na tegemeo la chama.

Naye mtoto wa Mbunge wa Jimbo la Kwella, wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, Chrisant Mzindakaya, Paul Mzindakaya, ameibuka mshindi wa kiti cha mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoani humo

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo kutoka Makao makuu ya umoja wa vijana, Thomas Mwang'onda ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa, alimtangaza Paul Mzindakaya kuwa amewashinda wenzake kwa kupata kura 205

Katika uchaguzi huo mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Afrika, Kituo cha Rukwa, Sammy Kissika, alishinda nafazi ya ujumbe wa Baraza Kuu la Vijana taifa

Mwang'onda alimtangza Bernard Mukasa kuwa ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa.

Mkoani Mwanza, Maghembe Boniphace Koneli amechaguliwa Mwenyekiti wa UVCM katika uchaguzi huo uliofanyika juzi.

Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mwanza, Barnabas Essau aliliwaambia waandishi wa habari jana kwa kura 365 na kuwashinda wagombea wenzake Abel Maiga Kaitila aliyepata kura tisa na John Dea aliyepata kura 184.

Essau alisema kuwa nafasi ya mjumbe wa Baraza Kuu Taifa la chama hicho ilikwenda kwa Barnabas Mathayo, mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa amechaguliwa Barnabas Mathayo, nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa ilikwenda kwa Peter Yona Minga, uwakilishi wazazi ilikwenda kwa Muhoja mwinamila Mapande na uwakilishi wa UWT ilikwenda kwa Rehema Laurent.

Mkoani Mbeya UVCCM ilipata sura mpya baada ya kumchagua Regnand Msomba kuwa Mwenyekiti wake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Naye Benedict Ngwenye alichaguliwa mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Ruvuma kwa kura 331.

Akitangaza Matokeo hayo jana katika ukumbi wa shule ya wasichana Songea Msimamizi wa uchaguzi huo Livingstone Msinde ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tunduru alisema,wajumbe waliopiga kura ni 391 ambapo kura halali ni 387 na kura nne ziliharibika.

Mkoani Kagera, Deusdedith Katwale kuwa mwenyekiti mpya ya jumuia hiyo

Mkoani Kimalinjaro Godliving Mosha ambaye ni mpiga debe alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa mkoa baada ya kumpa kura 259 dhidi ya Antony Malisa kura 127 na Gilbert Temu aliyeambulia kura 102.

Mosha mwenye elimu ya Sekondari, aliwabwaga wasomi wawili Malisa na Temu ambao wana elimu ya chuo kikuu.

Wakizungumza na Mwananchi baada ya matokeo kutangazwa, baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu walisema wameamua kumchagua Mosha kwa vile anafahamu vema shida na matatizo ya vijana wa mkoa wa Kilimanjaro.

Habari hii imeandaliwa na Julieth Ngarabali, Kibaha, Lilian Lucas,Morogoro, Paulina David, Mwanza, Brandy Nelson, Mbeya, Joyce Joliga, Songea, Lilian Lugakingira Bukoba, Mwandishi Wetu, Sumbawanga na Ally Sonda,Moshi
 
Amosi Makalla hajui anachosema, ufisadi ungekuwa uzushi huyo Rajab Maranda mweka hazina wa CCM Kigoma na wenzie kumi na nane wanafanya nini mahakamani Kisutu? Tatizo la ccm ni kuokoteza watu barabarani na kuwabatiza majina eti "KADA WA CCM" ndio inakuwa qualification ya kuwa "TREASURER" wa ccm Taifa!! Makalla ana utaalam gani wa kuwa mweka hazina wa chama cha siasa kinachojiheshimu mtu ambaye wengi tunamjua utaalam wake ulikuwa kuhesabu vigae pale Mbezi Tiles; ndio maana anabwabwaja hovyo hovyo tu!!.
 
Chrisant Mzindakaya lazima amehonga sana akitumia fedha alizokwapua kwa mgongo wa BOT ili mwanae apate uenyekiti wa vijana CCM huko Rukwa. Matokeo haya yanaonyesha jinsi mafisadi wa ccm wanavyowatayalisha watoto wao kurithi chama chao ili hapo baadae waweze kuficha siri za maovu ya baba zao; unaona hata yule Mwang'onda wa Kagoda amehakikisha mwanae pia ameingia kwenye ulingo wa siasa.
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,Amos Makala ni miongoni wa viongozi wa CCM wenye upeo wa kuona mbali
 
Bulesi
kwa taarifa zako Amos Makala ni msomi CPA holder,vile vile ana Advance Diploma ya Business Admnistration na Postgraduate degree ya procurement and supply kutoka chuo cha usimamizi wa fedha IFM
Maranda ni maimuna kaishia darasa la saba kuna kipindi alijaribi kujiunga na Elimu ya watu wazima Unfortunately akafeli akiwa form 2
 
Back
Top Bottom