Jesca Magufuli achangia Ujenzi Nyumba ya Katibu UVCCM Wilaya ya Chato. Asisitiza Kumuenzi Hayati Magufuli

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
"Mimi nikasema si vibaya nikajumuika na vijana wenzangu (UVCCM) Wilaya ya Chato katika ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Chato na kuhakikisha inakamilika, nikasema nichangie kidogo nilichobarikiwa kuhakikisha kazi za Chama na pia siyo mwisho, nitaendelea kuchangia zaidi na zaidi mpaka kuhakikisha nyumba imekamilika kabisa" - Jesca Magufuli (Mtoto wa Hayati JPM)

Jesca Magufuli amesema kuwa amewiwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi vya nyumba ya Katibu wa UVCCM kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za vijana wa CCM ambao wameonyesha dira ya uwajibikaji

Bi. Jesca Mafuguli ametoa vigae kwa ajili ya kukamilisha nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Chato ambayo kwa sasa imefikia Asilimia 90 ya ujenzi huku akiwaasa vijana kuendelea kushirikiana katika Kulijenga Taifa la Tanzania kupitia serikali ya awamu ya Sita.

Naye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutoka UVCCM mkoa wa Geita, Rubein Saganyika Amewataka Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Chato kumuenzi Rais wa awamu ya tano, Hayati Dk John Magufuli kwa kuchapa kazi na kuiishi slogan yake ya Hapa Kazi Tu.

Aidha, Ruben Sagayika amewaomba vijana kuendelea kujitolea kwa ajili ya kukijenga chama ambapo amemushukuru binti wa Hayati Dk Magufuli ambaye ni Jesca Magufuli kwa kujitolea baadhi ya vifaa ujenzi kukamilisha ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM Chato.

WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.32(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-17 at 17.19.33.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-17 at 16.37.04.jpeg
 
"Mimi nikasema si vibaya nikajumuika na vijana wenzangu (UVCCM) Wilaya ya Chato katika ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Chato na kuhakikisha inakamilika, nikasema nichangie kidogo nilichobarikiwa kuhakikisha kazi za Chama na pia siyo mwisho, nitaendelea kuchangia zaidi na zaidi mpaka kuhakikisha nyumba imekamilika kabisa" - Jesca Magufuli (Mtoto wa Hayati JPM)
Kwanini alitutosa wenzake UDOM wakati tulikuwa tunafanana kila kitu?
 
Back
Top Bottom