Jibaba Bonge
JF-Expert Member
- May 6, 2008
- 1,246
- 401
Hivi huo ni msaada kweli au kodi inayotakiwa kulipwa TRA inapitia mlango wa nyuma??
Maneno umesema mengi sana lakini hayana uhusiano wowote na CCM kupokea msaada wa mwananchi, semeni labda tatizo ni kwa sababu ni Mhindi, dataz nilizonazo ni kwamba CCM enzi hizo ilikuwa haina bajeti wala responsibility, ilikuwa inachota tu serikalini bila idhini yetu wananchi, Mwalimu alikuwa na mazuri na mapungufu pia, lakini no way ninataka kurudi kwenye maisha yake tena yale ya foleni za unga wa njano no thank you!
Mhindi ni mwananchi ametoa mchango wake kwa chama cha siasa, kama kuna sheria inakataza isemwe, kama mhindi ni mwizi isemwe wizi wake, tule naye sahani moja, hisia haziwezi kuwa sheria ni just hisia tu!
Tunaelewa kwamba CCM ina ubovu, so is vyama vyote vya siasa, lakini tuwe na sababu ya kumshambulia mwananchi anayetoa msaada kwa taifa.
Some of us will soon be proved right. unahitaji moyo wa paka kutetea mambo mengine. Hata hivyo kinachogomba hapa nafikiri ni nani anapokea zaidi kuliko anayetoa huo msaada. Angekuwa anapokea dagaa tu duh JF hapangetosha lakini anayepokea, loh.... funika kombe. JF inapoteza hadhi, koleo haliitwi tena koleo, na nyani anaangaliwa kwanza sura lakini thubutu utamke hivyo. Hivi akina Lowassa, Mkono na hata Mkapa wameshitakiwa ? ..ama kweli, wanavyovaliwa njuga humu JF !!! Kichwa kimenasa, juhudi za kuokoa zapamba moto.... kulikoni ? Sasa ni wakati mwafaka wa kutamka wazi kuwa CCM imeoza, full stop.
Jamaa kwa kulia lia...Mmhm!The secretary-general of the opposition Chadema, Dr Wilibrod Slaa, said he was surprised that CCM, which had been calling for a law to guard against the influence of money in local politics, had made a swift about-turn in the "hour of need".
^^Wenye ufahamu wa mambo
Civic United Front (CUF) head of Foreign Affairs and International Relations Ismail Jussa told The Citizen that he had no qualms about the ruling party accepting such donations.
"As far as I am concerned, there is nothing wrong provided they followed all the required procedures," he said.
He, however, said it was important that the President fulfilled his promise of introducing a law on the funding of political parties "so that no individual will hold any political party to ransom".
Jamaa kwa kulia lia...Mmhm!
^^Wenye ufahamu wa mambo
Thank you Kevo. Ni aibu tupu lakini wengine wanataka kuhalalisha matajiri kupitia ufisadi kutoa michango mikubwa namna hii kwa CCM. Halafu tukisema CCM ni chama cha mafisadi wanakuja juu. Huyo Somaiya alikuwa ni mmoja wa watu wa karibu katika mkataba wa kununua rada ambayo baadaye mkataba huo ulionekana umejaa rushwa tupu na uchunguzi wake bado unaendelea.
Wakati serikali na CCM vimegubikwa na habari za ufisadi wa hali ya juu kupitia EPA, Richmond, ununuzi wa Rada, ununuzi wa ndege ya Rais, magari ya jeshi na helicopters za jeshi na jengo la UVCCM itakuwa ni utaahira kulifumbia macho hili la tajiri anayehusika kwa karibu na tuhuma dhidi ya rushwa katika ununuzi wa rada kutoa pesa nyingi kiasi hicho kwa chama ambacho kuna ushahidi wa kutosha kwamba viongozi wake wa juu wanahusika na ufisadi.
Huu msaada umetolewa na mtuhumiwa katika ununuzi wa rada na kupewa CCM ambayo kuna ushahidi wa kutosha kwamba ilihusika na wizi wa mabilioni ya BOT kupitia Tangold, Meremeta, Deepgreen na ili kuficha ushahidi dhidi ya wizi huo wanathubutu kusema kwamba hilo linahusu usalama wa Taifa!!!! Hili la kupokea pesa hizo linathibitisha kwa mara nyingine tena kwamba CCM ni chama cha mafisadi.
Kuhisiwa pekee yake kwa tuhuma nzito za Radar kunatosha kabisa kuifanya CCM ikatae 'msaada' wake. Na wangekuwa makini huyu angekuwa anachunguzwa alihusika vipi na kashfa ya Rada, lakini bado anapeta tu mtaani!!!!
Hili siyo swala la ubaguzi kwamba tunamjadili huyu kwa kuwa ni mhindi, bali tunamjadili huyo kwa kuwa ana tuhuma nzito dhidhi yake katika ufisadi wa ununuzi wa Rada. Huku ni kukumbatia mafisadi na ndiyo maana ufisadi utaendelea kushamiri Tanzania. Usilifananishe hili na ubaguzi hata kidogo. Utajiri wanaoupata kwa kupitia njia za haramu si utajiri unaostahili kupigiwa makofi hata siku moja.
Huo si ufahamu wa mambo bali ni kutojua kuchambua mambo kwa kina. Leo Somaiya kaipa CCM shilingi millioni 400 ili kukisaidia chama hicho katika uchaguzi wa tawi la vijana. Sidhani kama uchaguzi huo utagharimu pesa nyngi kiasi hicho. Kesho Manji naye anatoa milioni 400 ili zisaidie uchaguzi wa UWT na kesho kutwa Subhash Patel anatoa milioni 400 ili zisaidie uchaguzi wa jumuiya ya Wazazi. Hizi ni pesa nyingi sana na tayari zinaipa advantage kubwa sana CCM ukilinganisha na vyama vingine visivyokuwa madarakani.
Kwa maoni yangu kuwe na limit ya shilingi million 5 tu ambayo itatolewa katika kipindi cha kila miaka miwili na mchangiaji mmoja na pia chama kinachopokea mchango huo kitozwe kodi inayostahili kwa kiasi hicho ilichopokea. Hii itasababisha kupunguza matajiri wawe wa halali ama wa haramu kuipa advantage kubwa sana CCM katika chaguzi zetu maana sidhani kama uchaguzi wowote ule wa moja ya jumuiya za CCM unahitaji shilingi milioni 400 ili kugharamia uchaguzi huo.
Vizuri sana, naona sasa unarudi kinyume, ama umeshafahamu kuwa mchango wa Somaiya katika umoja wa vijana hauna tatizo kisheria. Aidha hofu yako ni juu ya matajiri wengine kuchangia CCM pekee na sio kwa vyama vingine.
Hilo lisikupe shaka, kwani nimesoma sehemu kuwa Chadema tayali wameshaanza kupokea matajiri waliokuwa wakiichangia CCM. Cha msingi ni kwa matajiri hao kuendelea kuchangia Chadema pasipo kuogopa.
Aidha suala la kiwango cha uchangiaji katika jumuiya za chama linazungumzika, kama lile la kuchangia kampeni wakati wa chaguzi. Kwa sasa ni heri kuwa umefahamu nini kinaendelea.
Vizuri sana, naona sasa unarudi kinyume, ama umeshafahamu kuwa mchango wa Somaiya katika umoja wa vijana hauna tatizo kisheria. Aidha hofu yako ni juu ya matajiri wengine kuchangia CCM pekee na sio kwa vyama vingine.
Hilo lisikupe shaka, kwani nimesoma sehemu kuwa Chadema tayali wameshaanza kupokea matajiri waliokuwa wakiichangia CCM. Cha msingi ni kwa matajiri hao kuendelea kuchangia Chadema pasipo kuogopa.
Aidha suala la kiwango cha uchangiaji katika jumuiya za chama linazungumzika, kama lile la kuchangia kampeni wakati wa chaguzi. Kwa sasa ni heri kuwa umefahamu nini kinaendelea.
Its an insult kumfananisha jeetu Patel na somaiya young man.Kma hujui watu aliochangia kuuleta uhuru wa nchii ni pamoja na somaiya thats why hata wakati wa ktutaifisha viwanda mwalimu aliviacha viwanda vya somaiya.usikurupuke kujifanya Mr Politician.Kwani Jeetu alichanga kiasi gani wakati wa kampeni za CCM/JK 2005? Sasa hivi yuko wapi? JK ni zaidi ya tunavyomfahamu!
Its an insult kumfananisha jeetu Patel na somaiya young man.Kma hujui watu aliochangia kuuleta uhuru wa nchii ni pamoja na somaiya thats why hata wakati wa ktutaifisha viwanda mwalimu aliviacha viwanda vya somaiya.usikurupuke kujifanya Mr Politician.
Mimi naamini kabisa hizi pesa za matajiri ndani ya vyama na jumuiya za vyama inabidi zithibitiwe
Transparent ndani ya vyama vya siasa kwa sasa hakuna kabisa hivyo ili kuhakikisha wanasiasa hawanunuliwi na matajiri ili wafanyiwe favours mbali mbali inabidi 'misaada' ithibitiwe barabara.
Mkuu Bubu, hapa ninakubaliana na wewe kwa 100%, yaani tupo ukurasa mmoja,
Tanzania tuwe na sheria ya kuthibiti zawadi au misaada kwa vyama vyetu vya siasa, lakini hatuwezi kuwa na sheria ya kuwalazimisha watoa misaada kutoa kwa pande ya siasa wasiyoitaka, hapana huo sio ustaarabu wala uhuru wa kisiasa, yaani wa wananchi ku-practice politics as they wish as long as hawavunji sheria za jamhuri,
Habari zote zilizo wazi so far hazionyeshi Somaiya kuwa ni fisadi, unless kuna habari ambayo haipo hapa tayari, kwa sababu kuwa na rafiki fisadi sidhani kama ni dhambi kwa sheria zetu za bongo, binafsi nina tatizo sana na tabia nyingi za Wahindi, lakini sio Wahindi wenyewe, Primary niliyosoma ilikuwa un-official ya Wahindi, na ninakumbuka sana tabia zao darasani, nimeenda Bombay nimewaona tabia zao kule wao wanaamini sisi waa-Africa ni wasi wasi, pamoja na kwamba kila mahali mjini kwao kuna kinyesi cha binadam, kitu ambacho sisi bongo hatujafikia bado,
Lakini still, hawa Wahindi bongo bado ni ndugu zetu Jumamosi nilikuwa ninaongea na mama mmoja wa Kiganda, akanipa darasa sana jinsi Wahindi kwao walivyo na heshima na wazawa toka kile kiboko cha Amin, na ni wachache sana sio kama zamani, sasa kwa kusoma betweeen the lines kwenye hii thread sio siri kwamba Tanzania tuna tatizo kubwa sana na Wahindi in general that hatuwezi kuona Mhindi akitoa hela zote hizi kwa chama cha siasa bila sababu nyuma yake, na kwamba ni lazima iwe sababu ya kifisadi, kwa kweli hakuna wa kulaumiwa kwa hayo mawazo,
Sasa tunafanya nini as a nation ku-deal na hii ishu ya Wahindi, kwa sababu the ishu hapa kama nina-read sawa sawa ni tabia za wahindi bongo, lakini sio Wahindi wenyewe au wote, au?
nyie mnapiga kelele zabure.. ni chama gani hapa au association yakibongo itakayokataa 400million zabure..lol.. lets be serious!