Kamati ya Zitto kumweka kitimoto gavana wa BoT

Kwa mtazamo wangu ni kuwa wanakamati walishindwa kutafuta the right question. Nina hakika hata huyo mkaguzi mkuu akienda kukagua vitabu hatakuta kosa lolote. Kwa nini? Kwa sababu kwenye bajeti ya BOT, kuna line item inayohusu hizo nyumba kwa cost ya 1.2b, na matumizi yake nayo yamepitia hatua sahihi za PPPR. Swali la msingi, je ni sawa kuweka bajeti ya kiwango hicho kwa ujenzi wa nyumba za/ya mtu mmoja?

"Bila shaka jibu ni ndio, kwavile yote hayo yalipita kwakufuwata kanuni na sheria za manunuz yaserikali, pili kitu kiliwakuna wabunge ni pale alipo sema Hii nyumba sio yangu ila ni ya BOT, so even nikiondoka gavana mwingine atakaa,pia ile valuation ya faida yaujenz au kuendelea kupanga ilionyesha bora kujenga so prof Amekuwa ktk watu wenye uchungu na pesa ya walipa kodi.
 
Zitto anapaswa kuwekwa kitimoto yeye mwenyewe kwanza kwa utumbo aliousema kuhusu dowans nk. hawezi kuwa muamuzi hata wa kukagua nyumba ya katibu kata tukamuamini, ni mganga njaa na juha asiye na dira wala mwelekeo.
 
Zitto anapaswa kuwekwa kitimoto yeye mwenyewe kwanza kwa utumbo aliousema kuhusu dowans nk. hawezi kuwa muamuzi hata wa kukagua nyumba ya katibu kata tukamuamini, ni mganga njaa na juha asiye na dira wala mwelekeo.

Zitto?????

My bet is that he's being used to justify the unjustifiable, outrageous & unrealistic costs for those houses.

We can neither forget nor forgive his views about Richmond/Dowans... as well as other recent views of his, most of which are pro-fisadis.

The issue here is not the procedure used, but is VALUE FOR MONEY.
 
Upo walakini mkubwa wa matumizi ya Shs. zaidi ya bilioni mbili kutumika kujenga nyumba mbili ama tatu wakati mamilioni ya wananchi wanakufa kwa kukosa tiba, mamia kama si maelfu ya watoto wanakufa kwa kukosa lishe bora kutokana na hali duni ya maisha ya wananchi mijini na vijijini.

Wengine tulitegemea kwamba Kamati pamoja na kukubali maelezo (technical) ya Ndullu kwamba hakwenda kinyume na bajeti n.k. wangelimpa darasa Ndullu na wengine wote wenye kasumba na mawazo hayo kwamba nchi maskini kama Tanzania inaweza ku-afford kuwa na luxuries kama hizo za majumba yenye swimming pools kwa ajili ya watendaji wake wakuu.

Je, kama zingelijengwa nyumba za kawaida kwa bei nafuu, fedha ambazo zingelisalia zingeliweza kuokoa maisha ya watanzania wangapi?

Hakuna yeyote aliyeweza kumuuliza Ndullu swali hili au ndio tuseme kwenye vikao hivyo watu wanaulizwa maswali technical tu maswali ethical/moral hayapaswi kuulizwa? Au hiyo Kamati ya Bunge haioni mushkeli uliopo na unaolalamikiwa katika suala zima la ujenzi wa nyumba hizo za gharama kubwa mno?
 
Huu uwajibikaji mbele ya kamati ni mzuri na gavana atajibu maswali. tatizo kwa kamati kama hii ni kutokuwa na meno. Watajadili alafiu wanaishauri serikali. Hatahivyo 2.5 bilion kwa nyumba mbili ni sawa. Tatizo jiingine ni umaskini. Watu wamekuwa maskini kiasi kwamba wanataka gavana aishi kwenye nyuma kama za manzese

Nasikia kichefuchefu...
 
Back
Top Bottom