Kamanda Suleiman Kova astaafu rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

Jambo wadau,
nimesikia asubuhi hii Kamanda Kova akisema kuwa nafasi yake inachukuliwa na Simon Sirro kuanzia kesho.
Nijuzeni kama uteuzi wa Simon Sorro ulitangazwa, au Kova ndiye kamteua?
 
simon nyakoro siro,

na wakurya ndiyo tunauweza sana huu mkoa wa Dar es Salaam na sasa majambazi na wahalifu wote mkae mkao wa kula na tambueni kuwa sisi wakurya huwa hatutanii na ukizingatia tuna sifa ya kuitwa kombania A huko majeshini. kama unajijua wewe ni mhalifu halafu upo mkoa huu wa Dar tafadhali sana upesi na haraka mno hamia Mikoa hii Kagera au Kigoma au Singida au Wilaya ya Kondoa lakini hapa Dar tunataka utulivu na nidhamu. wakurya oyeeeeeeeeeeee! jamani hiyo mikoa na hiyo wilaya niliyoitaja hapo ni ya watani zangu wakubwa na huwa napenda mno kuwatania humu hivyo msiogope.
 
na wakurya ndiyo tunauweza sana huu mkoa wa Dar es Salaam na sasa majambazi na wahalifu wote mkae mkao wa kula na tambueni kuwa sisi wakurya huwa hatutanii na ukizingatia tuna sifa ya kuitwa kombania A huko majeshini. kama unajijua wewe ni mhalifu halafu upo mkoa huu wa Dar tafadhali sana upesi na haraka mno hamia Mikoa hii Kagera au Kigoma au Singida au Wilaya ya Kondoa lakini hapa Dar tunataka utulivu na nidhamu. wakurya oyeeeeeeeeeeee! jamani hiyo mikoa na hiyo wilaya niliyoitaja hapo ni ya watani zangu wakubwa na huwa napenda mno kuwatania humu hivyo msiogope.
Mimi nahisi huyu jamaa ni mzanaki! Ila jamii ile ile
 
Kuna jamaa amenidhulumu kiwanja changu huko Bunju. nilipoenda polisi kufungua mashtaka Huyu Silo akaja kumkingia kifua. sasa akipanda cheo si ndo kiwanja changu sikipati tena. Dah dunia hii figisu figisu tu

daah pole sana ndugu, ila huyu jamaa mbona ni mtu ambaye ana akili sana, na huwa anajitahidi kuitumia akili hiyo, ukiona wanakuzingua kuhusu hicho kiwanja chako tafuta mwanasheria kisha kafungue kesi ili iwe na nguvu ya kupelekwa mahakaman haraka
 
Jk ndo kamteua haujamuona na Jana anakagua miradi ya maji .jamaa bd yupo kazini ndo tatizo kuchagua viongozo vijana wabishi kutoka kma kagame na nkurunzinza .shein wa watu wanamlazimisha tuu ila nafsi inamsuta
 
Mimi nahisi huyu jamaa ni mzanaki! Ila jamii ile ile

basi kama ni mzanaki basi nahisi atakuwa anatoka kijiji changu kata yangu maarufu ya BUTUGURI na pale kijijini kwangu KIBUBWA jirani kabisa na shule ya OSWALD MANG'OMBE SECONDARY SCHOOL. nimefurahi kusikia hivyo ila labda nikuambie tu kuwa sisi wana mkoa wa Mara hata kama tuna makabila tofauti tofauti lakini tukiitwa wakurya huwa tunakubali na hatuanzi kulikataa hilo kabila. sasa nenda kwa Wahaya au kutana na Mhaya halafu mwambie wewe ni Mhaya utaona anaanza kukataa na kukuambia kuwa yeye ni muhangaza au mnyambo eti kwakuwa tu wanaogopa kukubali kuitwa Wahaya kwakuwa wana sifa yao moja KUU.
 
Ametangaza leo katika kipindi cha kumekucha cha ITV.
kwani siku hizi ukiwa kamanda wa polisi unayemaliza muda wako wa utumishi
unaenda ITV kutangaza kustaafu ...? au ni taratibu mpya za utumishi wa umma.
 
Moja ya maadui wakubwa wa demokrasia na siasa za Tanzania ni kwa mtazamo wangu ni polisi. Huwezi kuwataja polisi bila kumtaja mkubwa wao.Hawa wanatekeleza amri wapewazo.Hapo KOva anahusika.

Baada ya uchaguzi mkuu mji ulijaa askari kila mahali.Kova lazima alishiriki kwa namna moja ama nyingine. walioenda kuchukua computer za wanaharakati walitumwa na nani? KOVA hakujua?

Mimi nasema adui mmoja wa demokrasia kaondoka. Rais ahakikishe anatupa mtu mwingine sahihi wa kulea demokrasi.Atupe mtu atakayefanya watanzania wawaone polisi kama walinzi wao wao na sio watu wa kukimbiwa.Vijana wengi wakiwaona polisi wanakimbia.Hili sii sahihi kabisa.

Kamanda ulijitahidi lakini sikupongezi.Wale wanaokuja mjini asubuhi kupitia kinondoni watakumiss sana kwa sababu gari zilikuwa zinavutwa kwa haraka pale Salender ili upite.

Mapunziko mema mkuu.
 
Ninaona kitete ndani ya mwenendo wa ustaafu huu. Kuna nini nyuma ya pazia?

Yeye anatangaza anayechukua nafasi yake, kwani yeye ndiye anaamua? Ukiliangalia kwa jicho la ki saikolojia, moja kwa moja unagundua kuna tatizo ambalo kwa aibu Kova anataka kuwaaminisha watu kwamba kila kitu ni kawaida.

Muda utasema.
Kova alikua astaafu kitambo sana akaongezewa muda na jk sasa kuna ajabu gani hapo?
 
Back
Top Bottom