Kamanda Suleiman Kova astaafu rasmi Jeshi la Polisi Tanzania!

Kustaafu hakuhitaji kutangazwa. Inapofika siku ya kuzaliwa kutimiza miaka 60 yatosha kusema fulani amestaafu. Asante Kamanda Kova kwa utumishi wako kwa Taifa. Kila la kheri!
 
Kwani kila anayestaafu ni lazima aende kwenye media kutangaza kuustaafu kwake? au ndio sera mpya ya utumishi wa uma?
Kule kalipia? au kapewa mwaliko? Na waliompa mwaliko leo hawakuwa na agenda muhimu za kulisongesha mbele taifa kwa kuelimisha maswala mbalimbali kwa watazamaji? Wadhamini muwe mnaomba theme nzima ya kipindi hata kabla hamjakizamini huu ni upotevu wa pesa hapa nauona!!
 
Tutamisi sana mkwara wake. Jamaa alikuwa akitema mkwara unaogopa hata kam isingestahili ivo. Apatikane wa design yake.
 
Amesema kwa sasa yuko tayari kufanya kazi yo yote kulingana na umri wake na hata kuanza kufanya siasa kwa kujiunga na chama cho chote cha siasa!
Chama hicho atakachojiunga nacho ni dhahiri kitakuwa chama cha magamba.
Atafuata nyayo ya maafande wenzie waliomtangulia IGP mstaafu Mahita na yule mwingine Tibaigana.
 
DSC_6401.JPG

Kamishina wa Polisi na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, Ametangaza asubuhi ya leo katika kipindi cha kumekucha cha ITV kwamba anastaafu rasmi kazi yake ya Upolisi.

Tunamtakia kila la heri huko aendako.
Alikuwa anasubiri kitu gani kustaafu
 
Kuna jamaa amenidhulumu kiwanja changu huko Bunju. nilipoenda polisi kufungua mashtaka Huyu Silo akaja kumkingia kifua. sasa akipanda cheo si ndo kiwanja changu sikipati tena. Dah dunia hii figisu figisu tu
Pole sana mkuu hiyo ndio dunia
 
Hata hivyo pia akachunguzwa pia ni kwa vipi katika kipindi chake cha kuongoza polisi ya kanda maalum ya Dar ndiyo kulitokea upotevu mkubwa sana wa maelfu kwa maelfu ya macontainer pale bandarini bila kulipiwa kodi.
Hivi ina maana ile intelejensia aliyokuwa akitamba kuwa Jeshi lake la polisi ilikuwa nayo ilikuwa inaishia kwenye mikutano na maandamano ya vyama vya Chadema na CUF pekee.
Wakati huko bandarini macontainer yanatoka bila kulipiwa kodi, intelejensia ya Jeshi lake la polisi ilikuwa inakwenda likizo?!
 
Last edited:
Kwangu mie kustaafu kwa Kova ni sawa na kuangalia Comedy katika TV halafu umeme ukakatika ghafla.
Kama kweli anakwenda kuwa mkulima awahi mrijo, haubi kabla Tractor za wachaga wasukuma hazijarudi makwao huu ndio msimu. Hima kamanda mstaafu
 
Baada ya kustaafu rasmi leo ndani ya jeshi la Polisi, Kamanda Kova katika utumishi wake uliotukuka ndani ya jeshi la polisi amefanya mengi sana, je wewe utamkumbuka kwa lipi kamanda Kova hasa wakati huu akianza maisha mapya kama raia.
 
There is something behind....kwanini kustaafu kwake kuende sambamba na taarifa za watoto wake kuhusika kwenye matumizi mabaya ya ofisi?
 
kwani siku hizi ukiwa kamanda wa polisi unayemaliza muda wako wa utumishi
unaenda ITV kutangaza kustaafu ...? au ni taratibu mpya za utumishi wa umma.
Hata wewe ukitaka unaweza kwenda kujitangaza ili mradi upewe nafasi! Ha ha ha ha ha ....
 
Back
Top Bottom