Kamanda Lowassa ndani ya Singida, Afanya mkutano Manyoni

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,982
6,465
Ikiwa ni siku tulivu kabisa mhe. Ngoyai anatarajiwa kuwasili mjini Singida mishale ya saa sita akitokea mkoani Dodoma ampapo atafanya mkutano wa kihistoria kwenye viwanja vya peoples kuanzia saa 10 jioni. Maandalizi yamekamilika mji mzima ni shamra shamra kuashiria uwepo wa kiongozi mkubwa.
……………………………………………………………………………………

Nimeshapiga kambi hapa uwanjani kwa ajili ya kuwaletea updates kwa kila kitakachokuwa kinajiri.
……………

Stay tunes for updates and photos

Mgombea Urais kupitia UKAWA Edward Lowassa ameingia Manyoni asubuhi kwa kishindo kikubwa na kulakiwa na umati mkubwa wa watu uliokuwa unaimba Rais..Rais..Rais muda wote wa mkutano.

Lowassa aliuambia umati huo wa watu kwamba analifahamu tatizo kubwa la maji katika wilaya ya Manyoni na amewahakikishia wakazi wa wilaya hiyo kwamba atahakikisha wananchi watapata maji ya uhakika mara tu atakapoingia IKULU.

Lowassa aliwaambia wananchi wajitokeze kwa maelfu siku ya kupiga kura ili ushindi wake uwe wa uhakika ambapo umati huo ulijibu kwamba watalala vituoni usiku wa kuamkia siku ya kura.

Pichani chini:Umati uliomlaki Lowassa Manyoni
12003995_892211230861011_3828660544159273829_n.jpg



12009826_892211434194324_6427034648326584194_n.jpg
 
Singida kamanda lisu alishamaliza kazi,serekali za mitaa aliwapiga miguu juu kichwa chini,sipati picha mwaka huuu lisu wakishirikiana na lowasa itakuwa ni shida ya hatari
 
Yaani mpaka saivi RAIS ni LOWASSA jana Dodoma wamesema YESSSSS kwa LOWASSA mpaka IKULU.
 
Back
Top Bottom