Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Mwaka 1964, Rais Nyerere na Karume Walipoamua kuunganisha Taifa la Zanzibar na Tanganyika, kila nchi ilipoteza katiba yake, bendera yake na Wimbo wa Taifa lake.
Wakati wa utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete, baada ya kupita zaidi ya miaka 40 tangu kuasisiwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Zanzibar walifanyia marekebisho makubwa ya katiba yao ya mwaka 1984, wakaitisha kura ya maoni, wazanzibari wakapiga kura kuipitisha katiba yao. Marekebisho hayo makubwa ya Katiba ya Zanzibar, ya mwaka 2010, yaliitambua Zanzibar kama nchi yenye katiba yake, bendera yake na wimbo wake wa Taifa. Marekebisho hayo makubwa ya katiba yakaainisha mipaka ya nchi ya Zanzibar. Marejebisho hayo ikayaondoa baadhi ya mambo yaliyokuwa ya Muungano kama bandari, gas na mafuta.
Kwa hiyo, tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzo, leo Zanzibar ina katiba yake ya nchi iliyoidhinisha bendera ya nchi ya Zanzibar, iliyoidhinisha vikosi vyake vya ulinzi vinavyofanana na polisi, iliyoidhinisha matumizi ya wimbo wake wa Taifa.
Kwa unafiki wa viongozi wetu wa wakati ule, wote walikaa kimya, kama vile hakuna kilichotokea.
Leo hii, sijui ni kwa ujinga au unafiki, mtu akitamka tu Tanganyika, eti ni mbaguzi na mtu mwenye dhamira ya kudhoofisha Muungano.
Tuwaulize hawa viongozi wanafiki na waongo, Zanzibar ilipokuwa inaandika katiba yake na kuitambua Zanzibar kama nchi, yenye alama zote za Taifa linalojitegemea, walikuwa wapi? Hawakuona? Au waliona, lakini waliona ni haki na ni sahihi?
Kama ni sahihi kwa Zanzibar, basi na sisi Tanganyika, tuandike katiba yetu, itakayoitambua Tanganyika kama nchi, katiba itakayorudisha nembo za nchi ya Tanganyika, na kuainisha mipaka yake. Na katiba ya Tanganyika ianishe wazi kuwa masuala yasiyo ya Muungano, na rasilimali za Taifa kama bandari na madini, iwe ni marufuku kwa asiye Mtanganyika kuyafanyia maamuzi.
Viongozi waache unafiki, wafumbe vinywa vyao kama walivyokuwa wamefumba wakati Zanzibar ikiandika katiba yake, na wakae kimya, wasinene lolote.