Kama yupo Mwana JF mwenyeji wa Mbekenyela- Msaada please!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
Mwishoni mwa juma linalokuja, natarajia kusafiri kwenda Mbekenyela huko Lindi, kuhudhuria na kuwa msimamizi wa ndoa ya shoga yangu wa siku nyingi sana. Kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri maeneo hayo huko Bara, ningependa kama yupo Mwana JF mwenyeji wa huko anielezee mazingira yakoje? Je kuna baridi, au joto, umeme upo, mitandao inapatikana, kwa maana ya simu na internet. Vipi maji ya kunywa ni salama, je kuna mbu na hali ya barabara na usafiri ikoje?

Nimesita kumuuliza mwenyeji wangu, naogopa asije akadhani namdharau na ninapaona kwao ni Bush.
 
Mazingira mengi ya vijijini yanafanana TZ, kama uliwahi kwenda kwenu kabisa jiandae hivyo hivyo tu labda kwenye suala la hali ya hewa. Lindi hakuna baridi kwa ujumla. kama umeamua na kukubali kwenda kumsimamia rafiki yako we nenda tu, hayo ya internet achana nayo kwanza sio mbaya hata kama hamna kwa siku 2 au 3
 
ukiona kimya ujue huko hamna mitandao ya simu wala internet (wavuti)
 
Mazingira mengi ya vijijini yanafanana TZ, kama uliwahi kwenda kwenu kabisa jiandae hivyo hivyo tu labda kwenye suala la hali ya hewa. Lindi hakuna baridi kwa ujumla. kama umeamua na kukubali kwenda kumsimamia rafiki yako we nenda tu, hayo ya internet achana nayo kwanza sio mbaya hata kama hamna kwa siku 2 au 3

Ina maana panafanana na huku kwetu Jambiani ZNZ? Inawezekana nikakaa kwa wiki moja, na sipendi nimiss JF na FB, si unajua mambo ya kuchapa umbea mitandaoni?
 
Tena huo upwani uko sawa tu, mtakuwa mnatofautiana kwa wale kula ugali wa muogo na nyie kula wali na tambi labda
 
Mwishoni mwa juma linalokuja, natarajia kusafiri kwenda Mbekenyela huko Lindi, kuhudhuria na kuwa msimamizi wa ndoa ya shoga yangu wa siku nyingi sana. Kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusafiri maeneo hayo huko Bara, ningependa kama yupo Mwana JF mwenyeji wa huko anielezee mazingira yakoje? Je kuna baridi, au joto, umeme upo, mitandao inapatikana, kwa maana ya simu na internet. Vipi maji ya kunywa ni salama, je kuna mbu na hali ya barabara na usafiri ikoje?

Nimesita kumuuliza mwenyeji wangu, naogopa asije akadhani namdharau na ninapaona kwao ni Bush.
angalia ucje ukaenda kukata shauri la kutorudi zenjibar.nasikia vijamaa vya huko ni noma kwenye kare kamchezo ka "mi ni zaidi kunako brazamen mi namzid".
 
Back
Top Bottom