Kama unaamini kazini kwako una marafiki subiri uachishwe kazi

Daydream

Member
Oct 26, 2023
58
328
Watu wengi wana tabia ya kudharau watu wa mtaani kwake au marafiki zake aliokua nao mara tu baada ya kupata ajira na kupata marafiki wapya wakiamini hao marafiki wapya ni bora kuliko wazamani.

Ukitaka kuamini kwamba kazini una marafiki bora au la subiri siku uachishwe kazi (Termination) ndo utajua hujui.

Ukishaachishwa kazi hao marafiki wapya uliowapata kazini wote wataanza kukukwepa na kuna wakati hata ukimuomba mtu vocha ya Tshs 1000 atakutolea nje na wakati mwingine hata simu yako hatopokea.

Baada ya kupotezana na marafiki wapya uliowapata kazini ndipo utaanza kurudi kwenye phone book na kujaribu kurejesha mawasiliano na marafiki wa zamani ambao mara baada ya kupata ajira uliamini wao si lolote si chochote kwako.

Ukiwa kazini especially kama ni ajira mpya fanya majukum yako pokea mshahara wako rudi nyumbani katumie na familia yako, usiweke ukaribu sana na wafanyakazi wenzako na jitahidi pia usitengeneze chuki na wafanyakazi wenzako.Jitahidi sana ku balance

Anyway nisiongee sana lakini nakukumbusha siku zote heshimu sana marafiki ambao watakuthamini hata kama hauna kitu kuliko wale ambao umewakuta kazini na ndio maana mwanamke utakaempata kipindi ambacho unajitafuta ni bora zaidi kuliko yule ambae utampata wakati upo vizuri kiuchumi.

Ahsante
 
Uko sahihi kabisa,nilikuwa afisa mauzo kampuni Fulani nilikuwa natengeneza hela balaa,Nilpigwa bonge la termination,ila nashukuru sana Mungu,jamaa zangu wa Zamani sikuuwaacha wengi niliwasaidia sana.Wakazini!uwiii!Noma sana.
 
Back
Top Bottom