KELA 72
Usiwe mshabiki wakati mambo yaliyojificha enzi hizo yakifichuliwa kwa kuwa wakati huo pengine hukuwapo(sina hakika) au yalifichwa yakawa hayazungumzwi kwa sababu zinazoeleweka pengine ndo ukawa huyajuwi. Historia itayafichua popote yalipo na wale (kama wewe) ambao wanaamini hayakutokea watayaona ya ajabu, waliyoyaficha wanasababu zao za kuvifanya vichwa vya baadhi ya watu kama ww viamini siku zote kuwa wao ni watukufu na si vinginevyo.Mfano ikisemwa kuwa wakati Nyerere alimlazimisha na kumtisha Karume ili akubali kuiunganisha Zanzibar na Tanganyika , ww hauta amini kwa kuwa umezaliwa, ukakuzwa, ukaelimishwa kuwa Nyerere ni Mwadilifu na amepungukiwa na mapungufu mengi ambayo binaadamu wakawaida anayo. sikushangaa wakati anafariki na kuzikwa, walitokea watu pengine wenye maono kama yako ww kuwa Nyerere afanywe "MWENYE HERI". na ndo maana hauta amini hata Yesu arudi kuwa mapungufu aliyokuwa nayo wakati akitawala yaliwaumiza watu na hata waliokuwa wenza wake. Kwa kukusaidia tu rejea katika ile Kesi ya uhaini ya akina bibi titi na wenzake, simulizi za sk Thabiti Kombo na hata maandishi ya Jumbe, hao watu walifanya kazi na Nyerere kwa karibu sana na wanamjua kuliko mimi na ww na hapo utajua hasa "The animal side of J.K.Nyerere" na kama utakuwa na nafasi soma maandishi ya W. E. Smith, na nyaraka (archives) za W. DOURADO. Halafu urejee katika mjadala na mtazamo huo huo uliokuwa nao kwa baba yako wa taifa.
Mkuu, kuhusu mwalimu kufanya makosa pia, liko waazi kabisa hatayeye alikiri mara nyingi kuwa hakuwa malaika, ila nilichosema ni uibilisi ni hila za kutaka kubadilisha kabisa baadhi ya mazuri ya mwalimu aonekane siyo lolote katika nchi yetu kama ambavyo unataka watu waamini. Huko kuficha kusiwe kwa hila... kuwe na wema kabisa. Nimesoma maandishi ya watanzaia wengi tu kuhusu mwalimu, waliotutangulia umri na walifanya kazi na mwalimu kama vile Dk Salim Ahmed Salim, wewe huwaamini hao! unawaamini kina DOURADO tu!?
Na hapa umezidi kujifunua hila zako,.. Hivi Mwalimu kufanywa mwenye heri kunakuhusu nini wewe? au inatuathiri nini sisi kama taifa? hayo mambo ya imani za watu tuwaache waendelee nazo bwana. wewe ni mkatoliki? kama anatangazwa kuwa mwenye heri ni kwa wakatliki ndio maana wao ndio wanaongoza zoezil hilo, au kama wewe ni mkatoliki nenda kanisani huko katoliki kawalalamikie kuwa hafai.
Nakuomba uache tabia ya kuwaza kwa kutanguliza dini dini kwenye masuala ya taifa letu, itatuharibia bure nchi yetu nzuuri, dini zenyewe hizi tunazoziwaza kila dakika tumeletwa tu na watu weupe, tuendelee nazo kwenye nyumba za ibada tu....ndiko zinakostahili.