Kama Serikali Haiamini Katika Uchawi, Mbona Inaamini Katika Kuukimbiza Mwenge?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,700
6,409
Msimamo wa Serikali ni kuwa Haina dini, ila watu wake ndiyo wenye dini. Labda, inaweza ikawa ni kweli.

Serikali imetuambia pia kuwa haiamini katika uchawi, lakini ni wachache watakaoweza kulipokea hilo!

Kwani Mwenge ni nini kama siyo uchawi?

Inasemekana, Mbio za mwenge ziliasisiwa na mchawi aitwaye Forojo Ganze. Na kama ilivyo kawaida ya uchawi kufanywa kisiri siri, ndivyo na mwenge nao ulivyo. Watu wamekuwa wakidanganywa kuhusiana na mbio za mwenge ili wazione ni mbio za amani, kumbe kuna agenda zingine za siri.

Ukifuatilia yanayotendeka kwenye mikesha ya mwenge, ni dhahiri kuwa, kwa sehemu kubwa, ni mambo ya giza. Ni mikesha inayoambatana na ulevi pamoja na uzinzi kwa wingi.

Ulevi na uzinzi ni ibada ya sanamu.

Je, Serikali itaendelea kuudanganya umma wa Watanzania mpaka lini, kuwa haiamini katika uchawi huku yenyewe ikiendelea kufanya uchawi kila mwaka?
 
nitoke gheto kwangu niende kwenye mkesha wa mwenge nifanye ufirauni kama wote

serikali inakuwa inahusika na nini hapo kwenye dhambi zangu
 
Msimamo wa Serikali ni kuwa Haina dini, ila watu wake ndiyo wenye dini. Labda, inaweza ikawa ni kweli.

Serikali imetuambia pia kuwa haiamini katika uchawi, lakini ni wachache watakaoweza kulipokea hilo!

Kwani Mwenge ni nini kama siyo uchawi?

Inasemekana, Mbio za mwenge ziliasisiwa na mchawi aitwaye Forojo Ganze. Na kama ilivyo kawaida ya uchawi kufanywa kisiri siri, ndivyo na mwenge nao ulivyo. Watu wamekuwa wakidanganywa kuhusiana na mbio za mwenge ili wazione ni mbio za amani, kumbe kuna agenda zingine za siri.

Ukifuatilia yanayotendeka kwenye mikesha ya mwenge, ni dhahiri kuwa, kwa sehemu kubwa, ni mambo ya giza. Ni mikesha inayoambatana na ulevi pamoja na uzinzi kwa wingi.

Ulevi na uzinzi ni ibada ya sanamu.

Je! Serikali itaendelea kuudanganya umma wa Watanzania mpaka lini, kuwa haiamini katika uchawi huku yenyewe ikiendelea kufanya uchawi kila mwaka?
Elimu yako ya uraia ni hafifu sana
 
Back
Top Bottom