Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 255
- Thread starter
- #101
Bwana Paulo,kuwa makini katika kuyachanganua mambo,kama kuna sehemu zenye idadi kubwa ya watu na hasa wenye hali ya kawaida sana ni maeneo ya mbagala(Wilaya ya Temeke) na Gongo la mboto(wilaya ya Ilala) kisha kinondoni, Treni hizi za TRL na TAZARA hata kama unasema hazifiki kila sehemu kitu ambacho kwanza unadhihilisha ubazazi wako, kwani magari yanafika kila sehemu? hujashuhudia utitiri wa pikipiki kila sehemu na hasa sehemu ambako magari hayafiki?
Ikiwa treni ya TAZARA ina ruti 24 kwa siku na kwa sehemu kubwa itawahudumia watu wa Temeke walio wengi huoni mchango wake? Treni ya TRL itakuwa na ruti kama hizo na kwa sehemu kubwa watu Ilala itawahudumia huoni mchango wake?
Hapo kwenye nyekundu kwani tatizo la teknolojia ndo limeonekana kuwa tatizo zaidi kwa kuanzishwa hizi ruti? au vp ulitaka kufumba na kufumbua ziwepo treni za umeme zinazokwenda kasi ama zisizokuwa na muongozaji binadamu? Pls.. jifunze kutambua juhudi za wenzako, mi ninavyoona hapo walipoanzia sio pabaya huo ushauri wako utafuata baadaye lakini kwanza tambua jitihada za mwanzo, ndo ugomvi wangu mimi na wewe Bwana Paulo!!
Unachangia ukiwa biased na waheshimiwa tayari!!! Nadhani la msingi ukirudi kwa heading na posit nzima sijaongelea Reli tu? Hivi BRT hukuiona? Sasa imagine Mwakyembe anahamishwa Wizara na jinsi ujuavyo mawaziri wetu hujiamlia ata kwa kushahuriwa na wake zao...... na wakati mwingine maamuzi huwa ya kukurupuka na kuvunja sheria mf. Kufunga vizibiti mwendo amabao ulikuwa mpango wa kifisadi au kuamua masomo ya biashara kufutwa....,. Lowasa kuja na njia tatu.... nk.