Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
KAMA MTAALAMU WA SAIKOLOJIA YA MAHUSIANO, NAMSHAURI HAKI MANARA APUNGUZE KASI YA KUANIKA MAPENZI YAKE HADHARANI, HASA FARAGHA YAKE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Nampongeza Haji Manara kwa mafanikio aliyoyafikia, amekuwa mfano mzuri kwa Watu wa aina yake, nazungumzia Watu wenye ualbino. Na ameonyesha jamii kuwa hakuna sababu ya kuwatenga Watu wa aina yake. kwa sababu wanauwezo wa kufanya makubwa kama Watu wengine. Ingawaje anaweza asipende hili kuzungumziwa lakini hatuwezi kukimbia ukweli.
Tukirudi kwenye mada,
Kumposti mpenzi au mchumba au mkeo/mumeo mitandaoni sio jambo baya. Kuna Watu wenye tabia hii na hiyo ni namna yao ya kuonyesha furaha yao. Ni namna ya mtu kujivunia na kukubali kuwa naye amefanikiwa na anafurahia maisha. Sio Kosa kisheria, kidini, kiroho na hata Kimila.
Isipokuwa, inategemea unapost nini kwenye mitandao.
Post lakini usizidi kipimo.
Mathalani, unaweza kupost upo na mkeo mmeenda kutalii, Sawa.
Umepost upo nyumbani na familia mnaswali au mnafanya ibada, Sawa.
Umepost upo na mkeo/mumeo mmeenda kwenye tukio fulani la kifamilia au la marafiki, Sawa.
Umepost labda ni siku ya sikukuu fulani mnasheherekea, Sawa.
Umepost upo ndani ya gari mnaimba au mnatoa ujumbe fulani, Sawa.
Epuka Ku-post haya,
Ku-post uko na mkeo/mumeo kitandani, Big Ni.
Ku-post mkeo/mumeo anakunawisha miguu au mikono, Big No.
Ku-post mpo mmeanda kuoga au mpo beach mnaogelea, Big No.
Ku-post unajibu Ma Ex WA mkeo au mumeo. Big No.
Ku-post unaelezea mapenzi yenu labda kwa kuyatetea au kuyalinda. Big Noo.
Mapenzi na mahusiano hayatetewi wala kupondwa mtandaoni au kwenye vikao.
Mapenzi na mahusiano yanatetewa au kupondwa mkiwa wawili Faragha.
Ku-post unakandia Wanawake au wanaume wengine huku ukimsifia mkeo au mumeo. Big No.
Wéwe kama ni kumsifia msifie lakini usihusianishe na wasiohusika. Mapenzi ni yenu wawili.
Ku-post unajifanya unakuwekea visheria mkeo au mumeo mitandaoni. Big No.
Elewa kuwa Mkeo au mumeo ni kiumbe huru kumuwekea visheria vyako ni kujaribu kutafuta wavunjaji wa sheria.
Ukiwa public, jaribu kueleza kuwa mkeo au mumeo unamuamini (hata kama humuamini) kuwa anaakili nzuri, na yupo huru kuamua analotaka. Sema kabisa kwenye upendo Hakuna sheria.
Lakini FARAGHA unajua zipo.
Mahusiano ya ukubwani hayanaga SHERIA. Au tuseme mtu uliyekutana naye ukubwani huwezi mwekea visheria vyako.
Kadiri unavyomwekea mtu mzima sheria ndivyo anavyozidi kukaribia kuzivunja.
Upendo na sheria haviendi pamoja isipokuwa upendo ndio sheria yenyewe. Yaani mtu akikupenda huna haja ya kumtamkia sheria kwa sababu yeye atahangaika kujua nini unapenda na nini hupendi. Na yale unayoyapenda atahangaika kuyafanya na yale usiyoyapenda atajitahidi kuyaacha. Bila kuona ni utumwa
Huwezi zuia Watu wasimzungumzie mkeo au mumeo ikiwa kwa hiyari yako ulipost mtandaoni. Hivyo ni kazi yako kupambana na matokeo ya ku-post mtandaoni ikiwa ni pamoja na kumtuliza mkeo kama anahisia nyepesi pale anapoona anapondwa na Watu mitandaoni.
Kabla hujampost Mkeo au mumeo hakikisha mumejuana vya kutosha. Au kabla hujaanza tabia ya ku-post mahusiano yako mtandaoni hakikisha unamfahamu vilivyo mwenza wako.
Hakikisha mmejengana kwa ndani na mnaelewana vizuri.
Mke na mume hujengwa katika nafsi na mioyo yao kabla ya miili yao.
Unapopost mkeo au mumeo unapost mwili. Na sio nafsi au moyo wake. Unaweza kuwa umemjenga kimwili lakini kumbe moyoni akawa ni dhaifu.
Kuachana ni rahisi sana kwa Watu ambao hawakujuana vizuri. Hawakujengana vizuri.
Unapompata mchumba jambo la kwanza ni kuwekana sawa muelewane na mjuane. Na hiyo sio chini ya miaka miwili mpaka mitano. Wanasa Zimwi likujualo halikuli likakwisha. Sasa mtu hata mwaka hamjuani unaanza mbwembwe. Unatafuta fedheha.
Manara endelea kufurahia maisha ya mahusiano lakini punguza Faragha zenu zisiwe hadharani. Wekeni hadharani mambo ya kawaida ya kisosholojia.
Ni hayo tuu Ndugu yangu na wengine wenye hulka kama hiyo.
Nawatakia Sabato Njema.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam