punainen-red
JF-Expert Member
- Nov 18, 2010
- 1,731
- 450
Waongo wakubwa hao, mbona hawajawahi kuwachunguza wale wahuni waliowasumbua kwa kiwango kikubwa watumiaji wa simu za mikononi wakati wa uchaguzi wa 2010?!
Polisi ipi inachunguza ni hii ya shemejie jk
Ni kweli Firstlady1, mwanzoni nilijaribu kumuangalia mtu kama Tundu Lissu, Mbowe, Mnyika nk kama kweli wangeweza kukaa chini na ku-compose sms kama zile, nikajiambia tu moyoni kuwa haiwezekani.Ila hii Serikali na watu wake nao hawana akili ingawa na wao wanatuona sisi akili zetu zimelala
Kwa watu Makini kama Kina Mnyika hata kama walitaka kutukana wangefanya mambo ya kijinga kama hayo..
JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.
Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.
Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike, alisema Senso.
Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.
Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.
Source:Mtanzania
wamemaliza swala la Dr Ulimboka...
hapo kwenye red je al-haji kova alikurupuka?JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.
Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.
Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike, alisema Senso.
Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.
Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.
Source:Mtanzania
zina tija sana,wale wanaounda kamati hupata pesa,zile pesa huzitumia kwa ajili ya masuala mbalimbaliikiwemo kuwasomesha watoto wao,so huoni kama zina tija kwa mtanzania?Nchi hii ina kamati nyingi za uchunguzi ambazo hazina tija kwa taifa.