Kama kweli simu za Mnyika na Lissu ziliingiliwa ni Kosa la Jinai: POLISI

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.

“Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.

“Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike,” alisema Senso.

Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.

Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.

Source:Mtanzania
 
Angalau angesemea na hoja za jana za Marando. Mimi ninavyowajua mapolisi, wanajua vizuri uhalifu huo na tena sio ajabu wanamlinda mhalifu huyo kwa amri ya vigogo wa serikali na ccm yao. Wamekalia kuti bovu haooo! Walianza kupinga kwa nguvu kubwa, amewaambia anao ushahidi 100% wanagwaya, wanamjua ni jembe Marando. Anaingia kona zote na hawawezi kumfanya lolote, sanasana kulalamika tu tuwaonee huruma. Nilishapoteza imani na mapolisi miaka mingi sana, sababu binafsi nimejikuta wananifanya vibaya wakiwa wanashangilia wameshinda.
 
Hawa walishawahi kufanya uchunguzi ukatoa majibu ya kueleweka, wanatuzuga tu hakuna lolote hapo, Jeshi la polisi sina imani nalo tena, hizo sinema zao haziuzi tena.
 
J
Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.

Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.

Source:Mtanzania

Na mimi ndio nilikua najiuliza...polisi wameunda kamati ngapi mpaka leo hii na hizo kamati zinalipiwa na nani? wasituchezee akili zetu...cdm wakilalamika polisi ndio wa kwanza kuchunguza...ccm ikitoa madongo wala hawachunguzwi au kuambiwa walete ushahidi....they're all just a bunch of currupt thugs
 
Wanachofanya polisi ni kuisafisha CCM kama TAKUKURU ilivyofanya kwenye sakata la Richmond, wangekuja Scotland Yard ningeamini lakini siyo polisi -CCM.
 
JESHI la Polisi nchini, limesema linaendesha uchunguzi wa madai yaliyotolewa hivi karibuni na Wakili Mwandamizi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando, kuwa kuna mtambo wa kunasa mawasiliano ya simu za mikononi umeingizwa nchini kinyemela.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Msemaji jeshi hilo, Advera Senso, alisema baada ya madai hayo kutolewa wiki iliyopita, jeshi hilo, kupitia Kitengo cha Simu na Ufuatiliaji, limeanza kazi ya kuchunguza ukweli wa mashine hiyo na kama kweli kuna aliyefanya kitendo hicho hatua kali sana zitachukuliwa.

"Taarifa za kuwapo na mtambo wa kuingilia mawasiliano ya simu ya mtu mwingine zimetufikia, tunachunguza kwa ukaribu, tunajua suala hili lilianzia bungeni na sasa lipo ndani ya jamii.

"Kuingilia mawasiliano ya mtu mwingine bila ridhaa yake ni kosa la jinai, sasa tusianze kuhukumu kitu ambacho hatuna uhakika nacho, tusubiri kazi ya uchunguzi ikamilike," alisema Senso.

Hata hivyo, alivyotakiwa kueleza ni kwa nini kumekuwapo na uundaji wa kamati nyingi za uchunguzi wa matukio yanayojitokea pasipokuwa na mrejesho wake kwa jamii, Senso alisema matukio ya uchunguzi hufanywa pole pole ili kutoa majibu ya uhakika.

Aliwataka wananchi kuwa na imani ya Jeshi la Polisi, kwani limejipanga kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa kuliongoza, licha ya kuwapo na kasoro ndogondogo.

Source:Mtanzania

KAMAKWELI HICHO KITENGO CHA SIMU NA UFUATILIAJI mpaka leo hii hakijui kwamba jambo hilo linawezekana mpaka kizinduliwe usingizini na Mabere marando, basi ama kimejaa vihiyo au kipo kwa agenda maalum ya kuhujumu makundi fulani fulani katika jamii, na maalum kabisa kama CDM na watu wengine vocal katika kutetea haki za wanyonge na raslimali za nchi, na kina dr. ulimboka na wengineo!! Adriana Mchawi wa jeshi la polisi na vyombo vya ulinzi na usalama vis a vis imani ya wananchi ni nyinyi wenyewe, imani imepotea siku nyingi ni bora liende tu na yote maisha.
 
Jeshi la POLISI limejipanga!!!

Hivi huwa wanajipanga vipi?
Njagu mmoja nyuma ya mwingine,Foleni?
Njagu mmoja kulia mwingine kushoto?
Wanapandiana mabegani?
wanashikana mikono na kuimba ukuuti! ukuuti !! wa! naaazi! wa naazi!??
Mduara?
Delta?
Mstatili?

Wanajipanga vipi?

Changa la macho hilo
 
Wanachofanya polisi ni kuisafisha CCM kama TAKUKURU ilivyofanya kwenye sakata la Richmond, wangekuja Scotland Yard ningeamini lakini siyo polisi -CCM.
Nilipata kusikia (sina uhakika kama ni kweli)kuwa Scotland Yard waweza kuwakodi kufanya upelelezi juu ya jambo fulani kwa gharama zako. Jee hii ni kweli? kama ni kweli Chadema wawaite na sisi tuchangie gharama kama tunavyochangia M4C ili kuwaumbua hawa wenye mbinu za kigaida na wananchi wajue ukweli wa nini kinafanywa na CCM.
 
Ila hii Serikali na watu wake nao hawana akili ingawa na wao wanatuona sisi akili zetu zimelala
Kwa watu Makini kama Kina Mnyika hata kama walitaka kutukana wangefanya mambo ya kijinga kama hayo..
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom