Jumakidogo
R I P
- Jul 16, 2009
- 1,851
- 417
Siku moja baada ya Serikali kutangaza kutumia hospitali za Jeshi na madaktari wastaafu kunusuru afya za wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini, juhudi zaidi zimechukuliwa na sasa itatumia pia hospitali binafsi.
Hospitali zilizotajwa kukubali kushirikiana na Serikali kutoa huduma za afya kwa watakaohitaji tiba ya haraka na walio katika tiba isiyoweza kusitishwa ni pamoja na TMJ, Regency, Aga Khan, Hindu Mandal, CCBRT na Hospitali ya Jeshi Lugalo.
Aidha, nguvu zimeongezwa katika hospitali za Mwananyamala, Amana na Temeke za Dar es Salaam kunakodaiwa hakuna mgomo, ili kutotoa rufaa nyingi kwa wagonjwa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kunakodaiwa kuwa na mgomo.
Na sisi wa huku Tandahimba tutaenda hospitali gani?
Huko nako kuna mgomo (Tandahimba)