Nashauri watu wanapoanzisha mada yoyote waweke 'titles' zinazobeba ujumbe uliopo na siyo kujaribu kuvuta hisia. Tusimwumbie daktari hisia na hofu zetu. Tuache madaktari wanaomtibu ndiyo waeleze maendeleo ya mgonjwa na siyo kila mtu kurusha hewani kitu anachohisi au kuwaza. Iwapo tunaamini ukuu na uweza wa Mungu aliyekuwa naye tangu mwanzo, basi tuache kutangaza hofu zetu.