Kalapina ''nabii koko'' na maneno yake mmh!

yani jamaa alipoandika barua ya kuomba msamaha Clouds kwa kosa walilomfanyia wao,kila mtu alimdharau...hadi Hashim dogo mpaka kesho anamcheka uyu jamaa..unajua kwa wasio mjua Pina wanamchukulia bonge moja la kamanda kumbe mweupe tu,utoto mwingi.

True dat mzee..
 
huwa nasikiliza nyimbo za huyu jamaa, kuna ule wa umoja ni nguvu humo ndani anasema ''siwezi kula nguruwe, siwezi kuabudu sanamu...''. wimbo wake mwingine mpya wa hivi karibuni anasema ''wanaabudu msalaba...'' .inafahamika yeye ni Muislamu sasa sijui maneno haya kwa nini anayapenda sana?
Sijaelewa, huyu jamaa muimba kwaya au hiphop? Ila mistari uliyoitaja ina 'ujumbe mzito'.
 
nini kula nguruwe, watu wanakula panya, mbwa na sokwe na wanaishi na wana afya safi. Wengine wanabudu Ng'ombe
na milima na wanaishi kama yeye asiyekula nguruwe wala kuabudu sanamu. Shika imani yako malipo ni huko mwisho wa
Maisha.
 
Kalapina a.k.a Nabii koko...ni mdini kweli..kama alivyo Hashim dogo..na si Pina Tu kikosi chote wana itikadi hiyoo ya kidini

ila tatizo la Pina ni kujifanya yeye Frontline kila kitu

Ishu ya yeye na clouds jamaa alihaidiwa kipindi cha Tv cha Hip hop..kipindi kile anafanya Hip hop bila madawa

Kwanini Pina hayuko na Vinega?

Pina Anadai wakati yeye anafanya harakati zake za kudai haki ..eti wasanii( VINEGA)..hawakumpa sapoti...kasahau kuwa alikuwa anawapiga baadhi ya wasanii...

Nitarudi....
 
Kalapina na Hashim Dogo walimfanyia kitendo kibaya sana Salu T, Salu T ndio alioandika ngoma yote ya Tunasonga,nyimbo ambayo inaibeba Kikosi mpaka kesho...awa jamaa walimzunguka na kwenda kurekodi peke yao ile ngoma kwa Majani..
 
Kala Pina mngese tu anaimba vitu utumbo kama ni mkali mpaka leo angedumu kwenye gemu ila asikiki aliwin tu kipind kile kupata airtime sio sasa Kasandaaa mbayaa
 
huyo mvuta bangi asiyejua kitu hana hadhi ya kujadiliwa kwenye jukwaa la magreatthinker.
 
Kalapina a.k.a Nabii koko...ni mdini kweli..kama alivyo Hashim dogo..na si Pina Tu kikosi chote wana itikadi hiyoo ya kidini

ila tatizo la Pina ni kujifanya yeye Frontline kila kitu

Ishu ya yeye na clouds jamaa alihaidiwa kipindi cha Tv cha Hip hop..kipindi kile anafanya Hip hop bila madawa

Kwanini Pina hayuko na Vinega?

Pina Anadai wakati yeye anafanya harakati zake za kudai haki ..eti wasanii( VINEGA)..hawakumpa sapoti...kasahau kuwa alikuwa anawapiga baadhi ya wasanii...

Nitarudi....

Mkuu sikubaliani na wewe kuwa Hashim Dogo ni mdini, ninavyoelewa na ninavyomuelewa ni kuwa anaamini dini yake na wala haingiliii imani ya mwenzake na toka nimfahamu sijaona elements zozote za kidini alizoonyesha kwa washkaji wake walio na dini na sisi tusio amini mungu.. Anaamini kivyake na anaheshimu dini nyingine angekuwa mdini asingeoa hata huyo mke wake mzungu. He is SMART mbaya na hilo namkubali...
 
Hana ukali wowote me namfananisha na Mr. Blue tu.

bora byser anauza hayo mapenzi na upuuzi anaoimba.muziki wa pina nauonaga wa kitoto tangu kitambo!hashimu,gwalu,msemakweri hawa walijua kufanya hip hop,huyu mkaza sauti anadhani anaweza kulazimisha kutoka kwa turufu ya dini,he's fake fake fake!!
 
kumbe dini inamzuia Pina kula nguruwe tu ,kijiti inamruhusu.....
huyo ndo Nabii koko beach
 
kumbe dini inamzuia Pina kula nguruwe tu ,kijiti inamruhusu.....
huyo ndo Nabii koko beach
Pamoja na kalapina kutofanikiwa sana kimuziki lakini alikuwa anaheshimika kutokana na misimamo yake against wanyonyaji wa sanaa.Amejivua nguo kujisalimisha kwa maadui wake wa longtime! Hao Clouds hawatamsaidia lolote na huu mwaka hautaisha hajarudi kule kule! Kalapina mwepesi tu hana lolote!
 
kalapina bonge la mdini,naona siku izi ameamua kujiweka wazi.eti sasa ivi anafanya harakati za kupambana na ukatoliki!
Msikilize tungo zake kwenye ngoma yake mpya "vatican ndio wanaotuchagulia viongozi"..kuna mstari mwingine anasema "sili nguruwe wala siabudu sanamu" sikiliza kwa makini 'mstari wa mbele' na 'umoja ni nguvu' utanisoma..
Ana misimamo ya kitoto sana ndio maana anaongoza kundi ambalo halipo'kikosi cha mizinga' kwenye kundi kabaki ye na mkewe tu mau,machizi wote wamemkimbia hadi mwanae msemakweri...
hadi gwalufandu??
 
Sasa naanza kuiona vita ya waabudu MUNGU na waabudu masanamu, cjui nani ataibuka mshindi.
 
Watu wamekuwa wakimlilia Hashim Dogo arudi kwn game ila hataki, sijui lini atakubali atubariki hata na album moja tu. He is the king of Hip hop in TZ. Watoto wa siku hizi hawamjui. Sad!

Dogo Mwanaharamu,
Kalamu inamwaga Damu,
Nakuacha mweupe kama Mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula Hongo,
Na hivi hii ni Serikali,
Sera ya mbali,
Au sera ya zamani kwa mbali,
Tunapokwenda pana zali,
Vichaa wangu walume, wanyaka hiyo hali,
Tujifunze tujitume,
Mwisho wa mwezi tuvune,
Kama hujipendi njoo nichune,
Kila mjuba sasa kivyake.
Na hivi nina dhiki,
Nikipata karatasi,
Wino hutoka kwa kasi,
Kwa haya nina wasiwasi,
Kiu ya jicho,
Ulichonacho ndicho ulicho,
Tokea '77 wabongo wamefunga mkanda,
(Kudadeki)
|
Sijui kwanin haya mashairi ya Hashim hayabanduki kichwani mpaka leo hii!!!
 
Dogo Mwanaharamu,
Kalamu inamwaga Damu,
Nakuacha mweupe kama Mkorogo,
Chata ka' wagogo,
Wabongo acheni nyodo,
Wote mnakula Hongo,
Na hivi hii ni Serikali,
Sera ya mbali,
Au sera ya zamani kwa mbali,
Tunapokwenda pana zali,
Vichaa wangu walume, wanyaka hiyo hali,
Tujifunze tujitume,
Mwisho wa mwezi tuvune,
Kama hujipendi njoo nichune,
Kila mjuba sasa kivyake.
Na hivi nina dhiki,
Nikipata karatasi,
Wino hutoka kwa kasi,
Kwa haya nina wasiwasi,
Kiu ya jicho,
Ulichonacho ndicho ulicho,
Tokea '77 wabongo wamefunga mkanda,
(Kudadeki)
|
Sijui kwanin haya mashairi ya Hashim hayabanduki kichwani mpaka leo hii!!!

kuna mwanamke mi ananipa kiwewe,
yani mchana akikosa usiku anajihukumu mwenyewe,
sumu asipewe na mwanaume mwingine anatema,
kwa kweli naona ni vyema,kuweka nanga mapema,
mtoto wa kitanga mtasema,
wanga tena mtapanga mengi,
machizi wanamtazama, kwa macho ya wizi mama,
kama hizi ndio namna za siku hizi,hizi ni njama,sisizi kuhama
kama ndoto unanijia,
leo nakuingilia,

unaipata iyo verse yake?
Au hii..
Mjeshi anapokufa mwanajeshi anazaliwa,hakuna cha kuchekesha ata ucheshi ungetakiwa,
vingapi unavijua na vingapi hauvijui,
adui mbaya kuliko wote ambae umtambui,
ni anaeichelewesha asubuhi,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom