Kaka umetukosea kumtesa wifi, mapenzi yake kwako yalionekana dhahiri, sidhani kama atakubali

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Rafiki yangu alimlaumu kaka yake, nami nikaumia kwa kuwa nilifahamu kisa cha ndoa ile. Nitaelelza machache nayofahamu ambayo yaliniumiza.

Sitaelelzea ndoa yao kiundani ndugu wa rafiki yangu hawa ambao kwa makadirio walifunga ndoa mwaka 2016 na kubarikiwa mtoto 1 huku binti akiwa alikuwa na mtoto 1 ambaye alimpata kabla ya kukutana na mume wake.

Mara baada ya ndoa binti yule mama wa watoto 2 alikuwa na upendo sana kwa familia ile na kwa mume wake, nilipata kufahamu hayo kwa kuwa mara kadhaa tulikutana pale kwa wifi yake ambaye mimi ni rafiki yangu, hakika alikuwa binti mkarimu sana, niliwahi fika kwake mara 2 nikiwa na rafiki yangu.

Nakumbuka binti alipoolewa mama mkwe wake ( mama wa rafiki yangu) alipata ajali na kuvunjika uti wa mgongo kwa kuwa falia ile haikuwa na pesa za kuweza kumudu gharama binti aliamua kuuza nyumba ya urithi aliyoachiwa na wazazi wake ili amtibishe mama mkwe wake ambaye hakupona, alifariki na baadaye wakakubaliana na mume wake kiasi kilichobaki ampatie afungue mradi wa familia, hii ilikuwa mara ya kwanza mimi kufika pale kwake kwa kuwa msiba ulikuwa pale na baada ya msiba niliondoka.

Mara ya pili ilikuwa kwenda kuona mtoto baada ya binti yule kupata mtoto wake wa 2 na hapo pasi shaka nikajua kuna tatizo, kwanza nilianza kuhisi wakati tupo na wifi yake kwenye bajaji tukielekea eneo la tukio, nikasikia wifi mtu anaongea na simu, jibu lilikuwa hili VUMILIA WIFI YANGU SIJUI SHETANI GANI KAMUINGIA MBAYA ZAIDI NAMI HANINIKII.

Tulipofika pale tukakuta mtoto hana nguo zaidi ya kufunikwa vitenge na kuvaa nguo kubwa za kaka yake wa kwanza, binti akamuita wifi yake pembeni waongee japo wifi mtu akasema sio siri ongea tu hapahapa.

Mama yule mzazi akaanza kusema wifi kaka yako kabadillika sana, hapa hata sijui yuko wapi kama nilikwambia tangu ile siku aondoke hajarudi nilimtumia sms kumjulisha mimi kujifungua akajibu sawa. Ila jioni yule mwanamke akanipigia akasema hataki usumbufu kwa mume wake wako mapumzikoni.

Sina hela ya kutumia hata mtoto hana nguo achu=ilia hela ya kujikimu kwa uzazi wangu, hela nilikuwa nimejiwekea kwenye biashara zangu nilitumia kujitibia kipindi kile kanipiga hadi kupelekea kulazwa na kujifungua kabla ya siku husika(huku akilia akasema nashukuru mtoto alikuwa kakomaa tayari)

Binti yule kwa moyo wa upendo akasema wifi nampenda kaka yako, najitahidi kuwa mke kwake lakini nini hiki nachopata mimi au sikutakiwa kuolewa naye, tayari anaishi na mwanamke mwingine, kafunga biashara na kuhamishia nisipopajua katuacha sisi ila chochote, tulimuona na kumpa tulichopeleka. Kilipita kipindi cha miezi 9 tangu yule binti kujifungua, nilikuwa nikimuulizia najibiwa anaendelea vizuri alirudi kwao Kigoma.

Turudi kwenye mada

Naam ya Mungu mengi mwanaume yule alikokuwa na penzi jipya likaanza kwenda mrama kiasi cha kumkumbuka yule mke wake, ambaye hakuwahi hata kurudi kuona mwanaye ama hakika alishikwa na penzi akashikika na kusahau yaliyopita akaganga yajayo na sasa anajuta.

Alifika kwa dada yake siku hiyo jioni, akiwa na begi kubwa kama mtu aliyetoka safari ya mbali, nilianza kumuona mimi kabla ya dada yake kwa kuwa njia ya kupita kwenda kwa dada yake inaanzia kwangu. Nashuru ilikuwa siku ya Jumapili.

Mara baada ya Kufika kwa dada yake wakapokeana dada mtu alitoka kuelekea dukani kununua vitu vya kumkarimu mgeni, akapita kwangu kunijulisha ujio wa kaka yake na kunitaka nifike pia kumsalimu akiwa pale kwake. Mara baada ya maongezi mafupi wakasogea pembeni ila niliweza kuwasikia.

Kaka mtu alianza kwa kuomba msamaha kwa yale yaliyotokea na kueleza mengi yaliyotokea kwa mke wake, aliyeenda kuishi naye akieleza mara baada ya kuanza biashara akajiona anahitaji mwanamke mwenye muonekano bora wa hela alizonazo binti mbichi ambaye hajazaa.

Akasema akakutana na yule mwanamke na kuanza naye akiwa hana mtoto ila bora yule aliyekuwa na mtoto mara elfu. Akieleza sifa za mke wa kwanza akisema binti alikuwa akinipenda na kunisheshimu sana, mpele mcheshi na mwenye upendo na familia yangu sema kelele za marafiki kuwa nitaanzaje mechi 1-0 zilinifanya nikaanza kuona kama nilikosea kuoa, na kuwa baba wa mtoto atakuwa anatembea na mke wangu hivyo nikaanza kumchukia na kumpiga na kumfanyia visa ili aniache lakini mwanamke yule aliniomba radhi kama amekosea chochote na wala hakuthubutu kunifanyia baya, wala sikuwahi ona chochote kibaya kwake. Ila huyu balazuli niliookota najuta kukutana naye.

Dada nimetoka Kigoma, kumfata mke wangu niuombe radhi lakini sikuruhusiwa hata kukutana naye wala sikupata chansi ya kuzungumza na ndugu zake japo niwaangukie waniombee msamaha kwa mke wangu lakini kila mtu alijibu hawajui alipo wanajua yupo kwangu.

Dada najua utakuwa unaongea na mke wangu kwa kuwa wewe na yeye hamjawahi kugombana nakuomba mkubwa wangu niombee radhi kwa mke wangu na kwa familia yake, akinisamehe nitamlea kama mtoto mchanga.

Rafiki yangu akitokwa na machozi, akasema Kaka yangu, ulikosea sana kumtesa wifi mapenzi yake kwako yalionekana dhahiri, sidhani kama atakubali, ulitutia aibu ukoo mzima hata mama kule kaburini huenda anaumia sana hasa kwa kile alichokifanya kwa mama yetu. Mimi dada yako mume wangu akinitendea hayo siwezi kumrudia ila nitajitahidi kumbembeleza.
 
Back
Top Bottom