Kagasheki: TRA wanahusika biashara ya meno ya tembo

Hiyo kesi baada ya miaka mitatu itakuwa mzimu, aidha watuhumiwa watapewa vifungo laini au wataachiwa huru kwa kukosekana ushahidi wa kutosha...! Mnaikumbuka kesi ya Zombe!!!? Nani alitegemea hukumu ingekuwa vile?
 
hii kesi mbona laini tu, no evidence! Kuwepo meno ya tembo kwenye magunia ndo kunishtaki mie? aka!
 
Mheshimiwa sana Kaga-shake, si serikali yako unayohudumu ina kitengo cha intelijensia? Vipi majukumu yake? Yana mipaka? Kama yana mipaka interpol si mna link nayo? Omba msaada basi wakakupeleleze ni nani aliyefanya biashara na huyo wa Philipine. Hii itasaidia kuwataja wenzake wote. Usihofu, hata kama ni wenye nchi walipue tu tujue moja hata kama nchi haitatawalika kama walivyozoea kusema.
Mh. Mwak-embe, hapo bandarini panakushinda eti eeh? Fagia wote na hata hao tra ajiri upya. Hebu tuzingatieni sheria tulizojiwekea ili tuepuke aibu hii.
 
Kagasheki is like a toothless dog!Analalamika badala ya kuchukua hatua.Hawaoni Mwakyembe na Magufuli?Vinginevyo wasubiri kupigwa chini 2015!
 
Inabidi na Kinana achukuliwe hatua maana kampuni yake iliwahi kusafirisha container hadi Hongkong lilivyokamatwa akadai hahusiki na kilichomo ndani ya container-mh msigwa tusaidie kwa huyu jamaa yako
 
Ahhhhh!!!! Mh hayo mbona tumeshayazowea hapa Tanzania?ikitokea issue kama hio au inayofanana na hio hua inavuma palex2 mwanzoni,then baada ya mwezi mmoja au miwili husikii tena hii habari kuzungumzwa na hatimae hao wote waliokamatwa wanaachiwa huru,kwa maana ni WATUHUMIWA,yaani (PRIME SUSPECT) Cha ajabu na kusikitisha once ikija bainika hilo zogo na la KIGOGO fulani,basi hutomsikia tena Mh Waziri kufuatilia hili sakata,Hii ndio hali halisi ya nchi yetu tulipofikishwa,msingi wa yote haya ni RUSHWA iliyokithiri katika Nchi yetu ya Tanzania,kwa kweli aliyetoa huu msamiati wa kua RUSHWA NI ADUI WA HAKI,mimi ningemjua mtu ningemtukuza sana.Kwa maana haya ndo maafa na majanga yaliotukuta kwenye Nchi yetu ya Tanzania.Kuna issue kubwa Nchi hii kuliko ile ya EPA?imeishia wapi?kimyaaaaaaa hadi leo, na hio ya Pembe za Ndovu itazimwa kimya -kimya kama zilivyo zimwa za EPA na zinginezo.
 
Tuache ujinga. tembo wauawe bara. meno yasafirishwe hadi znz tayari kwa kwenda kuuzsa ufilipino. mtuhumiwa ni kibarua wa bandarini znz. thamani ya mzigo ni bilioni kadhaa. huyu kibarua au kuli amepanga uswahilini hana hata vespa. Jamani muogopeni MUNGU
 
Back
Top Bottom