Kagasheki: TRA wanahusika biashara ya meno ya tembo

Spanishboy

Senior Member
Apr 24, 2011
118
65
Balozi Kagasheki akiwa visiwani Zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena kubwa ya pembe za Tembo zilizokamtwa ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini, alisema kwamba TRA wanahusika katika ujangili huo kwa sababu wao ndiyo wenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba mizigo yote haramu haipiti katika bandari hiyo.

"Katika hili siwezi kumumunya maneno, lazima tu niseme ukweli hata kama wenzetu hawa watakasirika, lakini ukweli ni kwamba hawana pa kukwepea kwani wanahusika kwa asilimia 100 katika ujangili huu, kwa sababu kama watu wasingekuwa na maslahi katika hili kontena lisingekamatiwa hapa Zanzibar, hii ni ishara kwamba TRA wanahusika na kusaidia kulipitisha hadi huku," alisema Balozi Kagasheki.

Balozi alisema kwamba, shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea Philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda Philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.

Wakati huohuo,
Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemgine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.

Chanzo: Tabianchi blog
 
hv nina swali hayo meno wameshayashika mengi sana kwa sasa,huwa wanayafanyaje mwisho wa siku wanayachoma moto kama Rais Moi enzi zile alipiga moto ama yanauzwa tena mlango wa nyuma na hawa wakubwa wetu?
 
sheria ichukue mkondo wake haraka sana, tembo wetu wanaisha jamani, tena nasikia kama mbuga ya selous, tembo wanakwisha yaani. hawa wachina hawa na biashara zao, kama mnunuaji asingekuwepo wauzaji wangeua tembo kweli? SHERIA KWA KISWAHILI
 
Nikiagiza gari au mzigo wowote toka nnje Tra huwa wanakua nami mgongo kwa mgongo kufungua kontena na kukagua kwamba kilichomo ndicho kilichoandikwa kwenye document. Hata nikisafirisha bidhaa nje hatuani hizo hizo. Sasa pembe za ndovu zinapitaje!? Some people must be accountable.
 
hilo zigo si dili ya kitoto, na waliohusika ni watu wazito wenye cash ya kutosha, hii ishu itaishia hewani, watakamatwa wengine kabisa ila wamiliki halali wa huo mzigo hawatakaa wajulikane kamwe kwa nchi yetu hii
 
Nchi nzuri haina viongozi ccm chukua chako mapema hiyo ndiyo hali halisi mtu yoyote kama una mchongo wako kula tu n ww km hali inaruhusu
 
[font=&quot]balozi kagasheki akiwa visiwani zanzibar katika zoezi la kupakuwa shehena kubwa ya pembe za tembo zilizokamtwa ikiwa na vipande 1,021 na uzito wa kilo 2,915 ambayo haijawahi kukamatwa nchini, alisema kwamba tra wanahusika katika ujangili huo kwa sababu wao ndiyo wenye mamlaka ya kuhakikisha kwamba mizigo yote haramu haipiti katika bandari hiyo.

"katika hili siwezi kumumunya maneno, lazima tu niseme ukweli hata kama wenzetu hawa watakasirika, lakini ukweli ni kwamba hawana pa kukwepea kwani wanahusika kwa asilimia 100 katika ujangili huu, kwa sababu kama watu wasingekuwa na maslahi katika hili kontena lisingekamatiwa hapa zanzibar, hii ni ishara kwamba tra wanahusika na kusaidia kulipitisha hadi huku," alisema balozi kagasheki.

Balozi alisema kwamba, shehena hiyo iliyokuwa tayari kusafirishwa kuelekea philiphine ilikuwa katika magunia 98 yaliyochanganywa na magunia mengine ambayo yalikuwa yamefungwa pamoja na baadhi ya vitu vya baharini yalikuwa tayari yameshawekwa ndani ya kontena la futi 40 tayari kwa kusafirishwa kwenda philiphne yakiwa katika hatua za mwisho za mamlaka husika za bandarini.

Chanzo: Tabianchi blog
[/font]
hii nchi inaloelekea ni kibaya sana.
 
mapovu yanatutoka lakini serekali sikivu sisiem yaakina Mwigulu Nchemba kama haipo vile, sijui usikivu wake ukoje....?
Mkuu umesema vema,ila Serikali ni sikivu sana
Si mnaona! operesheni imesitishwa ili mzigo
uliokwisha kusanywa uondoke,afu useme siyo sikivu?
Hapa napongeza jitihada binafsi za kagasheki na intelijensia yake kule zanzibar
maana wataalam walitaka mzigo umwangukie ili ajiuzulu
walaji waendelee.
Wananchi tumuunge mkono kagasheki ili mzigo ambao haujasafirishwa
popote ulipo mafichoni au njiani kusafirishwa taarifa zimfikie kagasheki ili ukamatwe,
 
Jeshi la Polisi Zanzibar limewakamata watuhumiwa wemgine watatu wakiwemo Maafisa wawili wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA kituo cha Bandari Zanzibar kwa kuhusika na kashfa ya kupatikana kwa meno ya tembo yenye thamani ya Mabilioni ya shilingi.

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amewataja Maafisa hao wa TRA waliokamatwa kuwa ni Omari Hamad Ali(50) na Mohammed Hija(48) ambao wote wanafanyia kazi katika Bandari ya Zanzibar. Mtuhumiwa mwingine ni kibarua wa Mamlaka ya bandari Zanzibar Haidar Ahmad Abdallah(54).

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunaifanya idadi ya watuhumiwa waliokamatwa hadi sasa kwa kuhusika na sakata hilo kufikia watano.

Soma sakata zima NEWS ALERT: WATUHUMIWA WA MENO YA TEMBO ZANZIBAR WAONGEZEKA, WAMO MAOFISA WA TRA - Tabianchi


 
Back
Top Bottom