Kafulila na Hamad Rashid wametoswa?

Maskini hamad rashidi misuli yote ile amechemka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kafulila nae kachemka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Sasa wanatafuta lipi lingine? Wamekwisha kabisa kabisa! Chadema itaendelea kusimamia msimamo wake na tunaipenda hio -songeni mbele.

Kwani waligombea uenyekiti wa kamati zipi mkuu??....
 
..mpinzani serious aliyepata uenyekiti ni Zitto Kabwe.

..sasa hapo ndipo unapoona ujanja wa CCM kuchagua, Cheyo na Mrema, vichwa maji wa upinzani, kuongoza kamati muhimu za bunge.
Siioni tofauti kati ya Hamad Rashid na huyo ndugu kwenye red hapo juu
 
Mkuu Masanilo, hadi dakika hii jina la KAFULILA na HAMAD halijatokea kushinda kwenye kamati yeyote. Ninaimani kuwa hoja yao jana haikuwa kwa lengo la kushika kibendera. Sasa nauliza, ina maana hata wenzao wa CCM A wamewatosa?

Cha msingi tujue Hamad na Kafulila waligombea uenyekiti wa kamati zipi?,inawezekana pia hawakugombea nafasi yoyote licha ya wao kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha kuwa tafsiri ya kanuni inabadilishwa....
 
..nadhani Hamad Rashid Mohamed amekuwa mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara.

..sasa sijui kama suala hili ni la muungano ama la. kama siyo kwanini mbunge wa zanzibar aongoze kamati ya tanganyika?
 
Mimi mwenzenu Lowasa ukiacha maskata yake bado namkubali sana ila hiyo kamati aliyopewa ni tiketi ya kusafiri nje? Duh na mrema naye yupo ha ha mwaka huu kazi
 
Halafu daktari mwakyusa kapewa mifugo ha ha ha Tanzania bana
 
Mkuu taarifa hii unatujuza wewe, mimi nilitaraji nilipoona heading ningekuta majina ya wenyeviti wote waliochaguliwa ili tuwe kwenye position nzuri ya kuchangia, kumbe wewe unauliza swali!
kuna thread tayari ina majina ya wenyeviti wa kamati zote...............hebu kaitafute
 
PAULSS , here are the names of the WATEULE
(i) Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ni Abdallah Kigoda
(ii) Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na utawala ni Pindi Chana
(iii) Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ni Edward Nyoyai Lowassa
(iv)Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ni Magreth Sitta
(v) Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ni Jenista Mhagama
(vi)Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ni ………….
(viiMwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo na maji ni Prof.David Mwakyusa
(viiiMwenyekiti wa kamati ya Miundombinu ni Peter Serukamba.
(ixMwenyekiti kamati ya hesabu za za serikali za mitaa ni Augustino Mrema.
(x)Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma ni Zitto Kabwe
(xiMwenyekiti wa kamati ya heswabu za serikali ni John Momose Cheyo.
(xMwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara ni Mahamoud
(xiiMwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ni January Makamba

Kwa nini hizo kamati mbili zisingeunganishwa kupunguza matumizi ya fedha za watanzania? Kama Mambo ya nje, ulinzi na usalama ni kamati moja, kwa nini hizo zingine ziwe tofauti. Yaani ina maana zina unyeti sana kuliko ulinzi na usalama?
Just wondering.....
 
Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema VISINGIZIO

WASWAHILI HUSEMA TAKA MOJA mbili HUMCHOMOKA!


Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 22:08 0diggsdigg


hamadrashid.jpg
Hamad Rashid

Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR) na Hamad Rashid wa Wawi(CUF) jana waliipiga vijembe Chadema wakieleza kuwa matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge yameonyesha chama hicho kutokuwa wakweli.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa wenyeviti hao jana, wabunge hao walisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia njema waliyokuwa nayo kwa kutaka marekebisho ya tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani katika kanuni za Bunge.
"Labda niseme kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge nimeyapokea vizuri hasa kamati zile tatu zinazoitwa 'Watch Dog' ambazo hushikwa na wapinzani," alisema Kafulila.

Vita ya maneno baina ya CUF na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Chadema kwa upande mwingine ilionekana dhahiri kuhamia bungeni kufuatia Chadema kuonyesha msimamo wa kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, baada ya wabunge wa vyama hivyo kupeana mipasho katika kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge la kumi unaoendelea mjini Dodoma.

Hoja hiyo juzi ilifanya mkutano wa bunge la kumi kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi rasmi ya upinzani Bungeni’ na baadaye azimio hilo kupitishwa na bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa “kuivunja nguvu za kisheria Chadema”.

Jana Kafulila alisema juzi wakati wa mjadala wa azimio la Bunge kuhusu marekebisho ya tafsiri ya kanuni ya Bunge kuhusu maneno Kambi Rasmi ya Upinzani, wabunge wa Chadema walionyesha kuwa yeye Kafulila na Hamad Rashid walitaka nafasi za uenyekiti wa kamati hizo.

Alisema tofauti na mawazo hayo ya Chadema, matokeo yamekuwa tofauti na kuchukuliwa na Chadema yenyewe, UDP na TLP akiongeza kuwa hiyo ni salamu kwa Chadema. Alifafanua kuwa kwa matokeo hayo Chadema inapaswa kufahamu kuwa wao walitaka mabadiliko hayo kwa faida ya wabunge wote na si vyama vya NCCR na CUF kama Chadema walivyodhani.

"Hiyo ni salamu kwa Chadema, wajue kwamba sisi tulitaka mabadiliko kwa ajili na faida ya vyama vyote, umeona hata nafasi hizo zimekwenda kwa vyama vya UPD, TLP na Chadema yenyewe," alisema Kafulila. Hamad Rashid kwa upande wake alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamemfurahisha na kwamba yametokana na kazi waliyoifanya juzi kurekebisha kanuni za Bunge na kuwezesha Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP kuchaguliwa uenyeviti wa kamati.

"Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.
Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.

Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.
Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara
 
Hao walikuwa kama ile ya CHENGE na SITTA kwenye kugombea Uspika, Chenge alitumwa kuchafua hali ya hewa

KWa hiyo hata Hamad na Kafulila walitumwa kufanya Yaleyale ya Chenge
 
Wabunge wa CCM si wajinga kiasi hicho kumpa Mpemba badala ya Mtanganyika yeye asubiri mwaka 2015 ataungana na CCM kwenye upinzani usio rasmi.
 
KAtika matokeo ya uchagizi wa wenyeviti wa kamati za bunge sijaona majina ya HAMAD RASHID na KAFULILA. Kwa kuwa ninaamini wamegombea nafasi mojawapo kati ya zile zilizowatuma kuomba bunge kuwafungisha ndoa ya LAZIMA na CHADEMA ili waziongoze, je wametoswa?

Tunaomba mtujuze wenye taarifa.
Anza kwanza kutujuza kwamba waligombea kamati zipi,halafu ndio tujue kama walitoswa au la.
Kikubwa nilichoona Kafulila na Hamadi wameweza kujenga hoja iliyowezesha vyama vyote vya upinzani kuwa na fursa za kuwa viongozi katika kamati za bunge,wingi ni mzuri lakini uchache wa wabunge wa vyama vingine usipuuzwe ktk kamati kwani MTIKILA Peke yake ameanzisha mangapi?Mgombea binafsi katiba mpya please.
 
Anza kwanza kutujuza kwamba waligombea kamati zipi,halafu ndio tujue kama walitoswa au la.
Kikubwa nilichoona Kafulila na Hamadi wameweza kujenga hoja iliyowezesha vyama vyote vya upinzani kuwa na fursa za kuwa viongozi katika kamati za bunge,wingi ni mzuri lakini uchache wa wabunge wa vyama vingine usipuuzwe ktk kamati kwani MTIKILA Peke yake ameanzisha mangapi?Mgombea binafsi katiba mpya please.

Kafulila aligombea pamoja na mrema wajumbe wakamtosa kutokana na kiherehere chake wakampa babu mrema boya lao ambalo watalipeleka wanavyotaka..
 
..mpinzani serious aliyepata uenyekiti ni Zitto Kabwe.

..sasa hapo ndipo unapoona ujanja wa CCM kuchagua, Cheyo na Mrema, vichwa maji wa upinzani, kuongoza kamati muhimu za bunge.


Hakuna mpinzani serious hapo huyo zito vilevile ni mamluki/informer wao.
 
Back
Top Bottom