Kafulila kuendelea na ubunge

Hili la kuvuliwa UANACHAMA na kakikundi kadogo ka watu kanakotafuna RUZUKU yetu kwenye vihoteli vya hapa Dar halafu unapoteza UBUNGE wa JIMBO la wapiga kura maelfu mahakama zetu zitusaidie kwa kweli. Msajili wa vyama ameshindwa. Analialia tu kama mbwa aliyemwona chatu.
KATIBA ya JMT inatuangusha kwa hili. Inamtaka mtu kugombea kupitia chama lakini haisemi itamlindaje anapoandamwa na "best loosers" kama akina Mbatia.

Ha ha haaa. U besti Luza ndiyo sifa waliyonayo watanzania wengi, kuanzia kwenye siasa hadi kwenye michezo.

Si utawala bora wala kwenye sheria, si kwenye elimu ama kwenye afya!! nchi ya vituko hii.
 
Hii itabaki kuwa changamoto katika zoezi la kuanda katiba mpya
Msajili angetaka kuikabili hali hii angeweza. Ni kupeleka tu rekebisho la sheria iliyoiunda ofisi yake ikivitaka vyama vipeleke pendekezo kwake na jopo la wataalamu wake kuamua juu ya mtu kufukuzwa au kuvuliwa uanachama. Badala yake anapoteza muda kulalama tu kwenye Tv na magazeti!
Hii ni aibu kwa Tendwa kama halioni hili kama ni HAKI ya mtu aloopewa na KATIBA ya NCHI inanyang'anywa mchana kweupe kwa visasi tu na kulinda "UTUKUFU WA CHAMA".
 
We should make sure, we are civiliazed enough to conq. the victory, but we cnt do it while we are political allied, spinned and poluted ''If we beleave, we can..if we come together we can make a history'' mahakama kuu imenipa furaha sana kuamuru kafulila aendelee kuwa Mbunge kwani wanasiasa wenye tamaa za ubinafsi wa kumiliki vyama kama asasi zao hawatakuwa na nguvu za aina hiyo tena.
 
Nyie wanajamii forum mbona mna vichwa vigumu vya kuelewa. Maana yake ni kwamba atakuwa ameenda kuweka pingamizi la uamuzi wa yeye kukoma ubunge mpka hapo kesi aliyofungua itakapo kwisha. Kesi huchua muda mrefu wakati mwingine kusikilizwa sasa wakati kesi inaendelea kusikilizwa yeye aendelee kuwa mbunge. Kama mahakama itaridhia alifukuzwa kwa kufuata taratibu za chama then atakoma ubunge la sivyo ataendelea kupeta
 
We should make sure, we are civiliazed enough to conq. the victory, but we cnt do it while we are political allied, spinned and poluted ''If we beleave, we can..if we come together we can make a history'' mahakama kuu imenipa furaha sana kuamuru kafulila aendelee kuwa Mbunge kwani wanasiasa wenye tamaa za ubinafsi wa kumiliki vyama kama asasi zao hawatakuwa na nguvu za aina hiyo tena..Nyakarungu.
 
Kwani sheria inasemaje juu ya mbunge aliyefukuzwa uanachama na CC ya chama chake? Sheria ziko wazi sana ndugu yangu kuwa huwezi kuendelea kuwa mbunge pale ambapo chama chako kimekukataa. Huu uamuzi wa mahakama ni kuingilia sheria ambazo tayari zimewekwa.
 
Pamoja na kwamba hata mimi siungi mkono tabia ya watu wachache tu kwa maslahi yao kuamua kumfutia mtu uanachama na hatimaye kuipoteza haki ya wananchi waliomchagua, lakini pia sidhani kama huu ni muda muafaka wa kushangilia kwakuwa huu ni uamuzi wa muda tu huku kesi ya msingi ikisubiriwa kulindima.

Siku mahakama kuu itakapotangaza kutengua kabisa uamuzi wa nccr mageuzi kumvua kafulila uanachama, ndipo tutahitaji kushangilia, lakini kwa sasa ni mapema mno.
 
Kwani sheria inasemaje juu ya mbunge aliyefukuzwa uanachama na CC ya chama chake? Sheria ziko wazi sana ndugu yangu kuwa huwezi kuendelea kuwa mbunge pale ambapo chama chako kimekukataa. Huu uamuzi wa mahakama ni kuingilia sheria ambazo tayari zimewekwa.

Mahakama kuu haijaingilia sheria yoyote, kilichofanyika ni kuzuia kwa muda utekelezaji wa maamuzi ya NEC ya nccr mageuzi ya kumvua uanachama, ambao automatically alikuwa anapoteza na ubunge, kwakuwa kesi ya msingi bado haijasikilizwa.
 
mahakama imeona nini ndo ikaruhusu aendelea na ubunge wakati wale madiwani wa CDM walingonga mwamba au ndo yale yaliyosemwa kulikuwa na uchakachuaji katika kumfukuza waliletwa wajumbe mamuluki ,nafikiri hapkuwa na muhitasali wa kikao pia.
Yangu macho!!!
 
Nyie wanajamii forum mbona mna vichwa vigumu vya kuelewa. Maana yake ni kwamba atakuwa ameenda kuweka pingamizi la uamuzi wa yeye kukoma ubunge mpka hapo kesi aliyofungua itakapo kwisha. Kesi huchua muda mrefu wakati mwingine kusikilizwa sasa wakati kesi inaendelea kusikilizwa yeye aendelee kuwa mbunge. Kama mahakama itaridhia alifukuzwa kwa kufuata taratibu za chama then atakoma ubunge la sivyo ataendelea kupeta

Good move, lakini na msajili wa vyama vya Siasa asisahau kushikilia ruzuku ya NCCR mageuzi mpaka shauri litakapokwisha kwani akilipa kwa kuzingatia Kafulila bado ni Mbunge na mahakama ikaamua vinginevyo atakuwa amewalipa zaidi na akilipa kwa kuzingatia Kafulila si Mbunge na mahakama ikaamua kubatisha uamuzi wa NCCR mageuzi kumfukuza uanachama Kafulila atakuwa amewalipa pungufu.

Kuwashikiza adabu hiyo kamati tendaji ya NCCR mageuzi, ruzuku yote isilipwe hadi shauri la msingi litakapokwisha.
 
reality itabakia hivyo

kwamba kafulila kashaingia vita na chama chake, hata akishinda kesi hii lakini what about his political fortunes, his political future at nccr will always be in trouble if not finished, come 2015 nccr hatopata nafasi ya kutetea kiti hicho kwa makusudi kabisa ya kina Mbatia na Semgodo Mvungi,

Hashim Rungwe hajafungua kesi? what about others who have been expelled from nccr, were they proceduraly expelled from nccr? au hapa issue ni ubunge, hii kesi ingekuwa na nguvu kama wote waliofukuzwa pamoja na mzee wa malokasa Hashim Rungwe wangeungana kufungua shauri hili mahakamani

Kafulila should opt to another safe destiny rather than nccr mageuko
 
huu uamuzi wa mahakama haujakaa vizuri

mimi nilifikiri mahakama ingeamuru kafulila aendelee kuwa mwanachama wa nccr mpaka kesi ya msingi ya kuvuliwa uanachama bila kufuata utaratibu itakapomalizika, kwanini mahakama ime rush kwenye ku withold ubunge?

Mkuu nadhani maana yake ndiyo hiyo. Kwamba kwa maana nyingine Kafulila bado ni mwanachama kama asingekuwa mwanachama asingeendelea kuwa Mbunge. Hakuna mbunge Binafsi Tanzania, wabunge wote wa kuchaguliwa wanatokana na vyama vya siasa. Sasa kama Kafulila si mwanachama atakuwaje Mbunge wa kuchaguliwa?
 
We should make sure, we are civiliazed enough to conq. the victory, but we cnt do it while we are political allied, spinned and poluted ''If we beleave, we can..if we come together we can make a history'' mahakama kuu imenipa furaha sana kuamuru kafulila aendelee kuwa Mbunge kwani wanasiasa wenye tamaa za ubinafsi wa kumiliki vyama kama asasi zao hawatakuwa na nguvu za aina hiyo tena.

Kwenye Bold,,imekupa raha ipi? nakushangaa hata Zuberi nae namshangaa kuhusisha jambo hili na "Mungu+Unyonge" unategemea mahakama ifanye nn ilhali kuna kesi ya msingi imefunguliwa?ilikuwa lazima wafanye hivo mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa. Wewe na Zuberi mnaonyesha ushabiki binafsi wa hali ya juu katika jambo hili la Kafulila.
 
Back
Top Bottom