Kafulila kuendelea na ubunge

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
Ni amri ya Mahakama. Habari ndio hiyo!

SOURCE: http://twitter.com/#!/zittokabwe

===================

[URL="https://www.facebook.com/zittokabwe"]Zitto Kabwe



Kafulila kuendelea na Ubunge..... Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita.

Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote.
[/URL]

Kutoka Gazeti la Mwananchi:

KAFULILA aichanganta NCCR-Mageuzi

AMRI ya Mahakama Kuu iliyozuia utekelezaji wa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi kumvua uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila imeonekana kuuchanganya uongozi wa chama hicho ambao jana ulilazimika kutoa ufafanuzi wa hatua hiyo ukisema haujatengua uamuzi wake huo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu wa chama hicho, Dk Sengondo Mvungi alisema kabla ya kupokea hati ya Mahakama Kuu juzi juu ya amri hiyo, simu za wanachama wake mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii imekuwa ikiandika habari kuwa mahakama hiyo tayari imempa Kafulila ushindi katika shauri lake dhidi ya chama hicho.

“Msimamo wa chama kwa sasa ni kwamba maamuzi yake ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Desemba 17, mwaka huu bado hayajatenguliwa wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Isipokuwa kwa sasa tumepokea amri ya Mahakama Kuu ikizuia chama kisiendelee na hatua zaidi dhidi ya Kafulila na wenzake walioshiriki kushtaki chama kwenye kesi namba 218 ya mwaka 2011 mpaka shauri la msingi litakapoamuriwa,” alisema na kuongeza:

“Ufafanuzi wa kilichoamriwa na mahakama ni kuhusiana na yale waliyoyaomba ambapo hakuna hati yoyote inayoonyesha maombi ya kubatilisha maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa (ya NCCRR-Mageuzi). Suala la kuamuru upande katika kesi usifanye jambo zaidi ni katika mamlaka ya mahakama ambalo chama hakina tatizo na suala hilo.”

Hata hivyo, Dk Mvungi alisema hakuna amri yoyote ya mahakama iliyotolewa ya kuwabakiza waliovuliwa uanachama katika chama huku akisema suala la ubunge wa Kafulila lipo mikononi mwa Spika wa Bunge na kwamba wao kama chama nguvu yao inaishia katika kumvua uanachama.

Kauli ya Bunge
Akizungumzia suala hilo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliliambia gazeti dada la Mwananchi, The Citizen kwamba mahakama haiwezi kuiandikia barua Bunge kulitaka lisitoe uamuzi kuhusu Kafulila.

Alisema Mahakama inaweza kuiandikia barua NCCR na kuitaka iliandikie Bunge barua kusitisha utekelezaji wa suala lake.

Alipoulizwa kama Bunge litaendelea na taratibu za barua ya NCCR ya kumvua uanachama Kafulila, Ndugai alisema: “Bunge litaendelea na taratibu zake kama kawaida.”

Halmashauri Kuu ya NCCR-Mageuzi, ilimvua uanachama Kafulila, Desemba 18, mwaka huu, siku 10 baada ya kumwengua kwenye nafasi ya Katibu Mwenezi wa chama hicho kwa tuhuma za kutoa siri za chama.

Baada ya uamuzi huo, Kafulila aliandika barua kwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia akiomba kikao cha Halmashauri kuu kiitishwe tena kurejea uamuzi wake na baadaye kuwasilisha malalamiko yake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye alikiandikia chama hicho barua kutaka ufafanuzi wa malalamiko ya mbunge huyo kisha alikwenda Mahakama Kuu kuomba amri ya kuzuia utekelezaji wa uamuzi dhidi yake baada ya kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.


Hamad Rashid mambo bado mazito CUF
Katika hatua nyingine, Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kitendo cha Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed kugoma kuhojiwa juzi, imelenga kupoteza muda tu kwani hakiondoi msimamo wa chama kumshughulikia kwa mujibu wa katiba yake.

Juzi, Hamad aligoma kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu tuhuma za kuvunja katiba huku akiibua tuhuma nzito kwamba amenasa waraka wa siri wa viongozi wawili waandamizi wa chama hicho waliokuwa wakipanga njama za kumfukuza.Mbunge huyo alitoa sababu tano za kugomea wito huo ambazo ni* pamoja na kutoeleza tuhuma zake hasa vifungu vya katiba alivyodaiwa kuvikiuka na mamlaka ya kamati hiyo kikatiba.

Hata hivyo, jana Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema madai hayo ya Hamad hayana msingi zaidi ya kupoteza muda akisema kamati hiyo ipo kikatiba kwa kuwa iliundwa na Baraza Kuu la chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili, Abdul Kambaya alisema wanachama wake saba wamekwishahojiwa hadi sasa na wote wamekubali tuhuma wanazokabiliwa nazo za kuvunja katiba ya CUF na wameomba vikao vya juu vitakavyokaa kufanya maamuzi kwa kutumia busara ya hali ya juu.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari juzi, Hamad alisema anagomea kikao hicho hadi atakapopewa kanuni zitakazotumika katika kuendesha shughuli nzima ya kujibu tuhuma hizo na kupewa katiba iliyotumika ambayo ameivunja.

Alisema kati ya wajumbe wanane, hana imani na wajumbe watano kwa sababu wamekuwa wakimtuhumu hadharani: “Hawa wajumbe sina imani nao uamuzi wao hautakuwa wa haki kwangu.”

Jumatatu wiki hii Hamad na wenzake 13 waliitwa na Kamati na Nidhamu ili kujibu tuhuma za kuvunja katiba ya hicho baada ya kuwepo kwa mvutano wa muda mrefu kati yake na Katibu Mkuu Maalim Seif Shariff Hamad.
 
Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha.
 
Habari za kijiweni!
Kama ni gazeti basi habari imeandikwa "Na Mwandishi wetu"
 
Source nimeweka hapo juu.

Mkuu, hii ni amri ya muda pengine shauri la Kafulia likisubiriwa kutolewa uamuzi ,au mahakama imebatilisha kikao cha NCCR kilichomvua David ubunge? Hili zoezi lime-backfire. Badala ya kumjenga Mbatia, hata kale ka base kadogo alikokuwa nako NCCR kameondoka.
 
Mkuu, hii ni amri ya muda pengine shauri la Kafulia likisubiriwa kutolewa uamuzi ,au mahakama imebatilisha kikao cha NCCR kilichomvua David ubunge? Hili zoezi lime-backfire. Badala ya kumjenga Mbatia, hata kale ka base kadogo alikokuwa nako NCCR kameondoka.

mahakama imeamuru aendelee na Ubunge mpaka kesi ya msingi (kuondolewa uanachama bila kufuata taratibu) itakapokwisha
 
[h=6]Zitto Kabwe
[/h][h=6]Kafulila kuendelea na Ubunge..... Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita.

Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote.[/h]
 
NCCR bado hawajaiandikia barua Bunge, wakiandikia bunge barua kuhusu suala hilo basi hana ubunge
 
Na hii ya kwenda mahakamani ndiyo hatua stahiki na sahihi badala ya ile ya kumlamba miguu Mbatia. Kila la heri David, justice'll prevail.
 
Zitto Zuberi Kabwe@


@AnnieTANZANIA mahakama imeamuru aendelee na Ubunge mpaka kesi ya msingi (kuondolewa uanachama bila kufuata taratibu) itakapokwisha

4 minutes ago

huu uamuzi wa mahakama haujakaa vizuri

mimi nilifikiri mahakama ingeamuru kafulila aendelee kuwa mwanachama wa nccr mpaka kesi ya msingi ya kuvuliwa uanachama bila kufuata utaratibu itakapomalizika, kwanini mahakama ime rush kwenye ku withold ubunge?
 
Back
Top Bottom