Kafulila kuendelea na ubunge

Kwenye Bold,,imekupa raha ipi? nakushangaa hata Zuberi nae namshangaa kuhusisha jambo hili na "Mungu+Unyonge" unategemea mahakama ifanye nn ilhali kuna kesi ya msingi imefunguliwa?ilikuwa lazima wafanye hivo mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa. Wewe na Zuberi mnaonyesha ushabiki binafsi wa hali ya juu katika jambo hili la Kafulila.

hata mie naelewa kaka wala usihofu, ingawa ningefurahi sana kama hojaji zetu zingevutana pale na wewe upo kwa jina halisi kama mimi, ila sio shida..nami niseme haya:- wajua mbatia na wenzake walitamani kama kafulila anakosa haki hata ya kikatiba ya nchi tangu walipompokonya kadi ya uanachama, pia unaposema kuwa mimi na zuberi tunaonyesha ushabiki wa juu kwa hili, je ulitaka nisononeke kaka? NO siwezi kufarijika kwa aina ya mifumo ya vyama vyetu vya siasa vinavyojimilikisha uhai wa kisiasa wa vijana wenye upevu na uono kaka, pls pls ninaungana na yeyote anaefurahia hatua za awali za kafulila kutafuta haki...
 
Hii taarifa ya uamuzi wa mahakama imejaa utata sana; 1/Ni vipi mahakama imbakizie ubunge Kafulila wakati bado haijatangazwa kuvuliwa ubunge? 2/Ubunge wake ni matokeo ya uanachama wake, ni vipi mahakama ishindwe kwanza kumbakizikia uanachama wake,badala yake inakimbilia kumbakizia ubunge wake? 3/Kwa namna taarifa ilivyokuja inaashiria kabisa Zito Kabwe yupo bega kwa bega na Kafulila kwa kila hatua. Hiki ndio kinachowafanya watu wengi wasiwe na imani na Zito Kabwe kama mwanasiasa makini,yuko kutumiwa au kutumia watu tofautitofauti wa kambi mbalimbali za kisiasa kwa malengo ya kujijenga kisiasa.
 
hata mie naelewa kaka wala usihofu, ingawa ningefurahi sana kama hojaji zetu zingevutana pale na wewe upo kwa jina halisi kama mimi, ila sio shida..nami niseme haya:- wajua mbatia na wenzake walitamani kama kafulila anakosa haki hata ya kikatiba ya nchi tangu walipompokonya kadi ya uanachama, pia unaposema kuwa mimi na zuberi tunaonyesha ushabiki wa juu kwa hili, je ulitaka nisononeke kaka? NO siwezi kufarijika kwa aina ya mifumo ya vyama vyetu vya siasa vinavyojimilikisha uhai wa kisiasa wa vijana wenye upevu na uono kaka, pls pls ninaungana na yeyote anaefurahia hatua za awali za kafulila kutafuta haki...

Ha ha haaa, Poti poti.

Kwani issue hapa ni hoja ama jina halisi? btw, sheria za kujiunga JF zinampa uhuru mtu kuamua ajiandikishe kwa jina gani, halisi ama nickname.
Tuendelee kumuombea kafulila kesi yake icheleweshwe kusikilizwa na kuamuliwa hadi 2015, vinginevyo itakula kwake, uamuzi wa nccr mageuzi ni sahihi kwa mujibu wa katiba yao.
 
hata mie naelewa kaka wala usihofu, ingawa ningefurahi sana kama hojaji zetu zingevutana pale na wewe upo kwa jina halisi kama mimi, ila sio shida..nami niseme haya:- wajua mbatia na wenzake walitamani kama kafulila anakosa haki hata ya kikatiba ya nchi tangu walipompokonya kadi ya uanachama, pia unaposema kuwa mimi na zuberi tunaonyesha ushabiki wa juu kwa hili, je ulitaka nisononeke kaka? NO siwezi kufarijika kwa aina ya mifumo ya vyama vyetu vya siasa vinavyojimilikisha uhai wa kisiasa wa vijana wenye upevu na uono kaka, pls pls ninaungana na yeyote anaefurahia hatua za awali za kafulila kutafuta haki...
Kwenye Cyber space ni hiyari yako kuwa na jina lako au jina lingine
Vijana tunawapenda munapoleta changamoto kwenye kusukuma gurudumu la demokrasia ,lakini nyie vijana muna pupa za ajabu,Kwa mfano Kafulila mdomo na lugha alizotumia nidhahiri ni dharau sana ,mimi simpendi Mbatia haswa,lakini siafiki vijana tunaowategemea kama akina Kafulila kisiasa kufanya mambo ya Kijinga ya kujikweza kujifanya wenyewe ndio wanajua siasa
Vijana kama akina Kafulila hawana tofauti na wazee wao akina Mrema kujifanya wao ndio dira ya mabadiliko katika vyama walimo

Ukweli kafulila amerudisha hatua kumi nyuma kuisaidia NCCR kubadili mfumo wao wakujitandaza kwa ajili ya tamaa zake na waliokuwa wanamtuma aukwae uenyekiti,Bado nasema angetumia strategy nzuri na busara na heshima siku moja angekuwa Mwenyekiti
Kwa sababu vijana munaona wazee wanawachelewesha kwenye vyama vyao anzisheni vyama vyenu ambako kila mmoja wenu atalopoka anavyotaka ,musidharau vyama mulivyoko kwa kisingizio cha vyama vimeshikwa na wenyewe ,kwa hiyo nyie munaposhiriki kwenye hizo kamati tendaji munakaa kama misukule
manake karibu vyama vyote kwa sasa kamati kuu zote zina idadi ya vijana
Punguzeni tamaa munatuchelewesha kwenye ukombozi na mapinduzi ya demokrasia
 
Kafulila ndio basi tena kashang'olewa meno ya chuma hatobweka tena akiwa bungeni atakuwa mpolee na meno yake ya plastiki.
 
huu uamuzi wa mahakama haujakaa vizuri

mimi nilifikiri mahakama ingeamuru kafulila aendelee kuwa mwanachama wa nccr mpaka kesi ya msingi ya kuvuliwa uanachama bila kufuata utaratibu itakapomalizika, kwanini mahakama ime rush kwenye ku withold ubunge?

Mwenyewe imenikanganya mkuu,kwa hiyo Kafulila ataendelea kua mbunge bila ya kua mwanachama wa chama chochote?
 
Kwa hiyo Kafulila ni mbabe?
Alikuwa mbabe alipoanza kuropoka CDM na kabla hajatimuliwa NCCR. sekunde chache baada ya kutimuliwa uanachama NCCR aligeuka mnyonge na kuanza kumlilia Mbatia. Ni unyonge ARTIFICIAL.
 
Ni amri ya Mahakama. Habari ndio hiyo!

SOURCE: http://twitter.com/#!/zittokabwe

===================

Zitto Kabwe

Kafulila kuendelea na Ubunge..... Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita.

Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote.

Mungu yupo na wanyonge na wanaoonewa na hasa kwenye haki.

Kafulila hakukosewa haki alipata malipo ya utomvu wa nidhamu kwa kuwa na uroho wa tamaa ya kupoka madaraka. Alistahili alichopewa. Anaingia chama na hapohapo anaanza mapinduzi!

Zito naye si alikuwa na mpango wa kujiunga huko baada ya mapinduzi hayo ili naye agombee uraisi kwa vile CDM mambo yake hayasomi vizuri?

Wakati mwingine naona hawa vijana wanajifunza kwa njia ngumu sana (they learn the had way) hasa hawa wawili.
 
Mbunge wa KGM kusini Mh. David Kafulila aendelea kupeta katika ubunge wake hali hii imetokana na mahakama kutengua uamuzi wa kamati ya maadili ya chama hicho kumsimamisha uanachama ili kukosa hadhi ya ubunge. Mahakama imesema bado anatambulika kuwa ni mbunge mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakapo toa maamuzi.

Source: TBC Taifa jioni hii.
 
Mnauliza zitto kaingiaje ktk sakata hili? Zitto ni mchezaji aliyefungisha goli, kwa hiyo likisawazishwa ni lazima awe na furaha kuliko mfungaji. Makosa yake yamefutwa. Thanks kwa mahakama kuanza danadana.
 
thread hii ipo mbona mnatuchangaya sana na huyo mnafiki alikuwa analia nini?
 
Nashauri vyama vya siasa vijiwekee utaratibu kama wa FIFA ambao wanasema ni marufuku wanachama wake kupeleka masuala ya mpira mahakamani navyo vitamke kwenye katiba zao kuwa ni marufuku wanachama wake kupeleka masuala ya siasa mahakamani.
 
Kafulila na kabwe hongereni kwa kupigwa tafu na serikali.zito mshauri mwenza ajiweka sawa maana ubunge waka upo mashakani.ili asiwe wa kulia lia ovyo na kupiga magoti kisa mshahara wa ubunge awe na miradi kame wewe au mpe mchongo kwenye kamati yako,coz akiwa safi kiuchumu atakusaidia kwenye harakati zako ya urais,ili mje mtuibie vizuri
 
Hii nayo inaweza kuwa ni sentensi ndefu kuliko zote ulimwenguni.
 
ni vizuri tukaacha suala hili maana injuction ni interim measure au sitisho la muda na mahakama ikaendelea na kazi yake!
 
Back
Top Bottom