Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 22:08 0diggsdigg

hamadrashid.jpg
Hamad Rashid

Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR) na Hamad Rashid wa Wawi(CUF) jana waliipiga vijembe Chadema wakieleza kuwa matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge yameonyesha chama hicho kutokuwa wakweli.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa wenyeviti hao jana, wabunge hao walisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia njema waliyokuwa nayo kwa kutaka marekebisho ya tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani katika kanuni za Bunge. "Labda niseme kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge nimeyapokea vizuri hasa kamati zile tatu zinazoitwa 'Watch Dog' ambazo hushikwa na wapinzani," alisema Kafulila.

Vita ya maneno baina ya CUF na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Chadema kwa upande mwingine ilionekana dhahiri kuhamia bungeni kufuatia Chadema kuonyesha msimamo wa kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, baada ya wabunge wa vyama hivyo kupeana mipasho katika kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge la kumi unaoendelea mjini Dodoma.

Hoja hiyo juzi ilifanya mkutano wa bunge la kumi kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi rasmi ya upinzani Bungeni’ na baadaye azimio hilo kupitishwa na bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa “kuivunja nguvu za kisheria Chadema”.

Jana Kafulila alisema juzi wakati wa mjadala wa azimio la Bunge kuhusu marekebisho ya tafsiri ya kanuni ya Bunge kuhusu maneno Kambi Rasmi ya Upinzani, wabunge wa Chadema walionyesha kuwa yeye Kafulila na Hamad Rashid walitaka nafasi za uenyekiti wa kamati hizo.

Alisema tofauti na mawazo hayo ya Chadema, matokeo yamekuwa tofauti na kuchukuliwa na Chadema yenyewe, UDP na TLP akiongeza kuwa hiyo ni salamu kwa Chadema. Alifafanua kuwa kwa matokeo hayo Chadema inapaswa kufahamu kuwa wao walitaka mabadiliko hayo kwa faida ya wabunge wote na si vyama vya NCCR na CUF kama Chadema walivyodhani.

"Hiyo ni salamu kwa Chadema, wajue kwamba sisi tulitaka mabadiliko kwa ajili na faida ya vyama vyote, umeona hata nafasi hizo zimekwenda kwa vyama vya UPD, TLP na Chadema yenyewe," alisema Kafulila. Hamad Rashid kwa upande wake alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamemfurahisha na kwamba yametokana na kazi waliyoifanya juzi kurekebisha kanuni za Bunge na kuwezesha Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP kuchaguliwa uenyeviti wa kamati.

"Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.
Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.

Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.
Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara.
 
Bunge kwa sasa ni jukwaa la vijembe!waendelee tu,pole ya watanzania wanaoumia!
 
I knew Hamad na Kafulila kutoingiza majina yao ni mpango wao ili waonekane walikuwa na nia njema. Ha haaa wadanganyeni wengine sio mimi. Mlijua mkiweka majina madai ya CDM yangepata traction mkaamua kuyatoa. Good strategy but in wrong time.
 
Wanafikiri tutawaamini tena kama siku za nyuma. Tunawajua wao ni akina nani. Wamekimbia vitani na kujiunga na adui hivyo hawafai hata siku moja.:A S thumbs_down:
 
Walichokitaka ni kuwashirikisha na wengine na sio kuhodhi kila kitu kwa chama kimoja mie sioni tatizo especial kwa wao kutogombea zile kamati tatu.............
 
Mambo ni mengi kwa kweli sasa zile Thread, Kafulila na Hamad Rashid wametoshwa,
Hamad Rashid aumbuka, Mh John Cheo amwaga vibaya Mh Hamad Rashid, hizi habari kumbe sio za kweli GOSSIP kumbe ni soga
 
Kafulila, Hamad waipiga vijembe Chadema Send to a friend Wednesday, 09 February 2011 22:08 0diggsdigg

hamadrashid.jpg
Hamad Rashid

Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR) na Hamad Rashid wa Wawi(CUF) jana waliipiga vijembe Chadema wakieleza kuwa matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge yameonyesha chama hicho kutokuwa wakweli.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa wenyeviti hao jana, wabunge hao walisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha nia njema waliyokuwa nayo kwa kutaka marekebisho ya tafsiri ya maneno Kambi Rasmi ya Upinzani katika kanuni za Bunge. "Labda niseme kwa ufupi, matokeo ya uchaguzi wa wenyeviti wa Kamati za Bunge nimeyapokea vizuri hasa kamati zile tatu zinazoitwa 'Watch Dog' ambazo hushikwa na wapinzani," alisema Kafulila.

Vita ya maneno baina ya CUF na NCCR Mageuzi kwa upande mmoja dhidi ya Chadema kwa upande mwingine ilionekana dhahiri kuhamia bungeni kufuatia Chadema kuonyesha msimamo wa kutotaka ushirika na vyama vingine kwenye kambi yake ya upinzani, baada ya wabunge wa vyama hivyo kupeana mipasho katika kikao cha kwanza cha mkutano wa bunge la kumi unaoendelea mjini Dodoma.

Hoja hiyo juzi ilifanya mkutano wa bunge la kumi kuanza kwa moto pale Naibu Spika, Job Ndugai alipowasilisha azimio linalotoa tafsiri ya nini maana ya ‘Kambi rasmi ya upinzani Bungeni’ na baadaye azimio hilo kupitishwa na bunge hali ambayo ilitafsiriwa kuwa ni mkakati wa “kuivunja nguvu za kisheria Chadema”.

Jana Kafulila alisema juzi wakati wa mjadala wa azimio la Bunge kuhusu marekebisho ya tafsiri ya kanuni ya Bunge kuhusu maneno Kambi Rasmi ya Upinzani, wabunge wa Chadema walionyesha kuwa yeye Kafulila na Hamad Rashid walitaka nafasi za uenyekiti wa kamati hizo.

Alisema tofauti na mawazo hayo ya Chadema, matokeo yamekuwa tofauti na kuchukuliwa na Chadema yenyewe, UDP na TLP akiongeza kuwa hiyo ni salamu kwa Chadema. Alifafanua kuwa kwa matokeo hayo Chadema inapaswa kufahamu kuwa wao walitaka mabadiliko hayo kwa faida ya wabunge wote na si vyama vya NCCR na CUF kama Chadema walivyodhani.

"Hiyo ni salamu kwa Chadema, wajue kwamba sisi tulitaka mabadiliko kwa ajili na faida ya vyama vyote, umeona hata nafasi hizo zimekwenda kwa vyama vya UPD, TLP na Chadema yenyewe," alisema Kafulila. Hamad Rashid kwa upande wake alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yamemfurahisha na kwamba yametokana na kazi waliyoifanya juzi kurekebisha kanuni za Bunge na kuwezesha Mrema wa TLP na Cheyo wa UDP kuchaguliwa uenyeviti wa kamati.

"Nimefurahi kazi yetu ya jana (juzi) imesaidia Mrema na Cheyo wamepata uenyekiti wa kamati zinazotakiwa kuongozwa na wabunge wa upinzani," alisema Hamad. Aliongeza:" Kelele zetu zilikuwa kuweka msingi ya demokrasia ambayo imetendeka, lakini dhana walizokuwa nazo wenzetu Chadema hazikuwa sahihi.
Kilichofanyika ni demokrasia." Alisema kuwa kimsingi kila mbunge alishiriki uchaguzi huo na kwamba waliochaguliwa wamechaguliwa kadri ya matakwa yao, kwa kuwa ndiyo demokrasia na kwamba kilichobaki ni kuwapa ushirikiano na kujiamini.

Alieleza kuwa hakuna haja kuwa na hofu na uongozi wa wenyeviti hao kwa kuwa wanaongozwa na taratibu na kanuni za bunge zilizopo ambapo zinamlinda kila mmoja.
Injinia Stella Manyanya, alisema kuwa viongozi wa kamati hizo wamepatikana kwa ridhaa ya wabunge na kwamba wamechagua kwa busara. "Huu ulikuwa uchaguzi wa wabunge wenyewe, ndio wenye ridhaa, wamechagua kwa busara," alisema ambaye pia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara.

Nyumba ya mipasho hiyo.
 
Mambo ni mengi kwa kweli sasa zile Thread, Kafulila na Hamad Rashid wametoshwa,
Hamad Rashid aumbuka, Mh John Cheo amwaga vibaya Mh Hamad Rashid, hizi habari kumbe sio za kweli GOSSIP kumbe ni soga

Kuna watu humu JF sijui ni kwa makusudi wanaeneza habari zisizo na ukweli kwa manufaa ya watu fulani fulani ila wajue siku zote uongo hujitenga na ukweli hudhihiri. Si Kafulila wala Hamad waliogombea nafasi za uenyekiti wao walifanya kazi kutetea na sio kujitetea hivi ndivyo nilivyowaelewa.
 
Shosi

Ujue kuwa watanzania hasa Tz bara ambako tuliwachagua CHADEMA tunawaamini kwa matendo yao na dhamira zao safi kwetu kitu ambacho CUF au NCCR Mageuzi ni ndoto kukipata. Manake ni kuwa tunaowaamini ndio tunaowataka wawe wasimamizi wa serkali iliyoingia madarakani kwa kutuibia kura. Kafulila na Hamad Rashid kwetu ni wasaliti tu. Haki wanayoidai ni haki ya matumbo yao lakini si kwa maslahi yetu. Kumpa mtu kama Cheyo kuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serkali ni tusi kubwa kwetu watanzania bara make tunajua wote hao ni vibaraka wa wakoloni wetu CCM.

Wanzibar tunawapenda lakini mlikofika sasa mmevuka mpaka. Hiki kitendo cha Hamada kitafanya watu wa bara tumchukie kabisa huyu mpemba na wapemba wapemba wenzake. Tunataka maendeleo tunataka kuona serikali yetu inafanya wajibu wake. Ambao wanauwezo kuishika shati CCM kutuletea maendeleo na kuwajibika ni CHADEMA hao ndio tuliowataka washike hizo kamati muhimu halafu mjinga mmoja kutoka pemba anakuja na uharo uliomkamata kwa tamaa zake eti haki kwa vyama vyote. Huo ukweli unaoutaka haupo hapa. Kama CUF au NCCR wangekuwa wanafanya kazi nzuri tungewaona tu na kuwaamini lakini tunajua sio hivyo. Na kamwe wasifikiri wananchi tutawapenda kwa usaliti wao. HAPA NDO WANAJICHIMBIA KABURI. Na nakwambia hatuna huruma kuwazika wapuuzi kama hawa kwenye hilo kaburi.
 
Acha wapige majungu, lakini mwisho wa siku si Kafulila wala Hamad. Yes, we need to see some changes in our government,we need to see that the government is fullfiling her responsibilities. Naimani hao waliochaguliwa watafanya kazi nzuri kwani mfano tayari walishaupata kutoka kwa chadema walivyofanya kazi bunge la 9 kwenye kamati zao.
Wakijichanganya ndo wanajichimbia kaburi, hakuna asiyejua leo hii. Nenda popote utasikia wanavyoichukia ccm kama njaa. Watu wamechoka including mimi mwenyewe hawataki porojo, wala mambo ya kijinga. Hawa wazee wetu kinachowaua ni umimi, udini, ukabila na ushikaji. Lakini wenye miaka kati ya 40 shuka chini mambo hayo hawapotezi muda nayo.
 
Kama hali ya malumbano ya vyama vya upinzani Bungeni itaendelea kuwa kama hivi ilivyo sidhani kama maslahi ya wananchi yatakuwa properly safeguarded - By the way, inaonekana wenyeviti wa kamati za bunge either wana influence kubwa sana ama wana marupurupu makubwa nini? mbona wanataka kutoana macho kiasi hicho? Just being a member of a Paliamentary Committee hakumpi mjumbe nafasi ya kutosha kuwakilisha mchango wake na chama chake ipasavyo?
 
Demokrasia ipi inayo ongelewa? kwa maana CDM Walipewa dhamana na wengi ili iwawakilishe bungeni kwa hiyo bunge lingewapa haki hiyo CDM Wachague viongozi wa kamati kwa upande wa upinzani hii ndio demokrasia endelevu ili wengine nao wafanye juhudi kwa wananchi kuipiku chadema.
Kwa mtindo huo tunaidumaza demokrasia kwa maana unaweza kujipendekeza na kufanya lobing uingie upinzani ili uwe mwenyekiti wa kamati fulani.
Tukumbuke kila chama ni mpinzani kwa chama kingine
.
TUACHE UPINZANI UWE UPINZANI NA HAKI YAO WAPEWE!
 
kwa kweli kila nikiangalia mwelekeo wa chadema nnapata kuwaelewa.

kwa hio wao wanaona ni peke yao ndio wenye haki ktk nchi hii au vp ?

jeee siku tukiwapa wao kwa asilimia 52 na nyengine tukawapa wengine, wataunda serikali peke yao ?

kwa udhati nnaona chadema kimekosa watu wa kikiongoza, laiti ingekuwa na viongozi shupavu sisi CCM tusingelala, ila kwa hawa wavivu wa kufikiri wala hatuna wasi wasi maana wanakufa wenyewe bila hata ya kubughudhiwa.
 
Shosi

Ujue kuwa watanzania hasa Tz bara ambako tuliwachagua CHADEMA tunawaamini kwa matendo yao na dhamira zao safi kwetu kitu ambacho CUF au NCCR Mageuzi ni ndoto kukipata. Manake ni kuwa tunaowaamini ndio tunaowataka wawe wasimamizi wa serkali iliyoingia madarakani kwa kutuibia kura. Kafulila na Hamad Rashid kwetu ni wasaliti tu. Haki wanayoidai ni haki ya matumbo yao lakini si kwa maslahi yetu. Kumpa mtu kama Cheyo kuwa mwenyekiti wa kamati ya hesabu za serkali ni tusi kubwa kwetu watanzania bara make tunajua wote hao ni vibaraka wa wakoloni wetu CCM.

Wanzibar tunawapenda lakini mlikofika sasa mmevuka mpaka. Hiki kitendo cha Hamada kitafanya watu wa bara tumchukie kabisa huyu mpemba na wapemba wapemba wenzake. Tunataka maendeleo tunataka kuona serikali yetu inafanya wajibu wake. Ambao wanauwezo kuishika shati CCM kutuletea maendeleo na kuwajibika ni CHADEMA hao ndio tuliowataka washike hizo kamati muhimu halafu mjinga mmoja kutoka pemba anakuja na uharo uliomkamata kwa tamaa zake eti haki kwa vyama vyote. Huo ukweli unaoutaka haupo hapa. Kama CUF au NCCR wangekuwa wanafanya kazi nzuri tungewaona tu na kuwaamini lakini tunajua sio hivyo. Na kamwe wasifikiri wananchi tutawapenda kwa usaliti wao. HAPA NDO WANAJICHIMBIA KABURI. Na nakwambia hatuna huruma kuwazika wapuuzi kama hawa kwenye hilo kaburi.
:msela:Sipendi matusi napenda hoja!Kama chadema inapendwa zaidi bara kwa nini Vunjo tulimchagui Mrema?Kisha naomba unijulishe Cheyo ni Mpemba?Chadema inapendwa zaid bara lakin bara unayomaanisha ni ipi kule ilikpshindwa na Kafulila au kule sio bara?
 
Ushauri wangu kwa wabunge wa Chadema. Katu msikate tamaa kwa vita vinavyopiganwa dhidi dhidi yenu na CUF wakishirikiana na CCM pamoja na NCCR. Kwa nafasi za uenyekiti zilizotolewa kwa wabunge vibaraka wa CCM, ili kudhibiti untendaji wao, ninashauri muunde wenyeviti vivuli (watch dogs) wa kuwafuatilia Mrema na Cheyo (create watchdogs to watch the works of watchdogs elected to by MPs as watchdogs of government financial institutions)
 
Back
Top Bottom