Raia Mwema
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 535
- 79
Jiandae bunge litakuondolea kinga.
Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.
Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000, alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.
Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (SHah. 1,280,000) kwa siku.
IPP Media
Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??Huyu kashapotea...sina hata hamu ya kumsikiliza!!
naona hapa kuna haja ya kufanya utafiti zaidi maana inawezekana wenyewe 'miezi' yao ni tofauti na wengine hili tukijua hilo tukae kimya. Maana imesemwa katika baadhi ya Maandiko kuwa siku inaweza kuwa mwaka au mwaka kuwa sawa na siku!Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??
Deal with issues not personalities!!Elimu yako uliipata wapi?
Huyo nae ndio nini kuvaa tai la pinki? au ndio "pinky pinky"?
Hili swali lako Slaa atakuwa na nafasi nzuri sana kulijibu zaidi yangu mimi!!!!Usiangalie sura yake angalia anachoongea hapa mheshimiwa ni cha kweli au kina mantiki mtu alipwe milioni 7 kwa mwezi halafu mwalimu alipwe 150,000 kwa mwezi hepu tafuta ratio hapo kama unajua hesabu za uwianao??
mimi kinanikera kitendo cha kujadilikwa jumla mbunge au mfanyakazi fulani alipwe shilingi ngapi. mimi nataka watu walipwe kulingana na elimu yao kama mbunge ni darasa la saba au darasa la 12 alipwe kulingana na darasa lake na kama mbunge ni profesa alipwe sawa na maprofesa wengine.....unakuta mbunge ni darasa la saba anataka kujilinganisha na wafanyakazi kwenye sekta nyingine wenye degree mbili hii sio haki
Kafulila alisema ni aibu kuona daktari akilipwa mshahara wa Sh. 900,000, lakini wapo maofisa wadogo tu katika mashirika ya umma kama Benki Kuu (BoT) au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachota hadi milioni saba kwa mwezi.
"Angalia Gavana wa Benki Kuu analipwa mshahara wa Sh. milioni 20, Mkurugenzi wa NSSF Sh. milioni 18, mbunge Sh. milioni 1.8, daktari Sh. 900,000," alisema na kuhoji hapa haki iko wapi.
Aliongeza kwamba waziri akisafiri nje ya nchi posho yake kwa siku ni Dola za Marekani 420 (sawa na Sh. 672,000) lakini Mkurugenzi wa Mkuu wa Shirika lililo chini yake anachota Dola za Marekani 800 (Sh. 1,280,000) kwa siku.
Una maana kama Rais ana degree moja kama JK alipwe mshahara kidogo kulinganisha na waziri wake mwemnye PhD kama Prof Maghembe?
Elimu ni mojawapo tu ya vigezo vinavyotumika kupanga mishahara pia kuna uzoefu, Madaraka/Cheo, Specialization etc. Kwenye vyeo vya kisiasa kama Urais, Uwaziri, PS, Ubunge, U-kuu wa Mkoa na Wilaya etc, ELIMU huwa sio KIGEZO Kabisa, ndiyo maana utamkuta DC STD VII anapokea mshahara na marupurupu sawa kabisa na DC PhD holder!
Mishahara haiwezi kuwa sawa hata siku moja na huwezi kulinganisha mshahara wa gavana wa benki kuu na daktari wa kawaida. Ila unaweza kulinganisha mshahara wa gavana na neurosurgeon au cardiologist.
Wanasiasa wasitake kudanganya umma, kwa hili tatizo. Kinachotakiwa hapa ni kuona je mshahara wa laki 9 ni sawa kwa daktari ambaye fani yake ni rare huku mbunge akipokea mil 1.8? Ni muhimu kufanya "job analysis" katika sekta ya umma.
Halafu huwezi kulinganisha mshahara wa waziri na mkurugenzi wa shirika lililo chini yake hafahamu hata system ya career progression inayotumika ktk utumishi wa umma. Wanasiasa (mawaziri) mishahara yao sio mikubwa kiasi hicho kama anavyotaka watu tuamini, isipokuwa huku Afrika.
Yeye anadhani Rais wa Marekani analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa NASA? Au analipwa hela nyingi kuliko mkurugenzi wa CDC? Asidhani wananchi hatujui haya mambo tunafahamu sana.
Mbona ni mishahara midogo sana hiyo kwa watu wanaolinda mabilioni, nilitegemea dau awe anachukuwa kama milioni 200 kwa mwezi kumbe millioni kumi na nane tu? huu ni uonevu wa hali ya juu. Ma CEO wa kampuni binafsi zenye ukubwa kama wa NSSF wanakula mihela kibao duniani. Wafikiriwe hawa watu.