Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 31,275
- 31,404
Inaonekana nyumbani kwako pale meza ya chakula wewe unatengewa kuku na vitoto vyako vinahangaika na dagaa na maharagwe kila siku kwa vile tu wewe ni mleta mapato ya hapo nyumbani kwako. Na vile vile kwa sababu hiyohiyo unavaa nguo za dhamani kubwa na watoto wanatinga viraka... KULETA MAPATO HOME SI JUSTIFICATION YA KUKOSA UWIANO KATIKA KUGAWANA MAPATO.Msiwaonee hao wanaolipwa mapesa mengi wako kwenye eneo la income generation centre ya serikali wanaizalishia serikali mabilioni ya pesa kama gawio kwa serikali na kodi walipazo na mapato ya kodi ambayo ndiyo yatumikayo kulipa hiyo mishahara kwa watu ambao wako katika sekta ya matumizi tu (expenditure only sector) kama wabunge.wafanyakazi wa serikali n.k
Dunia nzima watu wanao-generate mapato wanalipwa sana iwe kampuni binafsi au serikali.Watu kama wa marketing au wale washughulikao na mauzo au dealing kwenye mabenki binafsi, makampuni ya simu na makampuni ya mafuta kwa mfano hapa nchini mishahara yao na bonus inapita kwa mbali hata ya huyo gavana na huyo wa NSSF.Hivi huyo kafulila anaiingizia serikali mapato ya shiliingi ngapi na hao wabunge na madaktari wanaiingizia serikali shilingi ngapi? Sana sana hao madaktari wanaitia hasara serikali sasa hivi serikali kwa kusababisha vifo vya walipa kodi mawodini na kusababisha mapato ya serikali kutokana na marehemu hao kupungua
Tusiwachokonoe hao watu wanaozalisha mabilioni ya pesa za kuingiza serikalini.Hakuna kazi ngumu duniani kama kuzaalisha mapato(Income).Hao wasipolipwa vizuri wakakata tamaa janga litaibuka la kitaifa hizo posho wabunge wanazollilia zitashushwa Kaangalie vitabu vya mahesabu vya makampuni ya hao wanaolipwa sana yakiwemo bandari,BOT,TRA n.k utagundua kuwa ukiangalia wanachoiingizia serikali na wanachopata wala haviendani kabisa.
Mwisho Kafulila bado kijana kama anaona ubunge haulipi anayo nafasi ya kubadilisha fani asome hasa aende huko anakoona kunalipa kama BOT,TRA,NSSF N.K .Mishahara ndivyo itakiwavyo kuwa mzalishaji mapato anatakiwa alipwe zaidi ya mtumiaji.