JWTZ na taarifa ya Mabomu Gongo la Mboto

Hakuna jambo la maana watakaloongea kwani tukio zima limezingirwa na uzembe wa hali ya juu. Taarifa hiyo itakuwa siasa, sidhani kama kuna jambo ambalo litakwepa uzembe, wakati wa mabomu ya mbagala jeshi liliapa kuwa tukio hilo haliwezi kutokea, sasa limetokea na kupoteza idadi kubwa ya watu. sidhani kama kuna sababu ya kufuatilia propaganda hizo.
 
upuuzi mtupu, television ya taifa halafu inakata network. mtatujuza mnaendelea kusubiri waanze kutangaza. mi nimechoka kusubiri
 
Tamko la Baraza la Usalama la Taifa lililorekodiwa linasomwa na JK TBC Taifa sasa hivi. Sijui tumsikilize nani sasa. Tunawachanganya watu.
 
Brigedia gani hajanyoa nywele, atawezaje kuwadhibiti wa chini yake wanyoe nywele
 
JF nimewakubali.... yani in a few minutes mmeweza kurusha powerpoint slide muhimu.... hebu fungueni TV yaishe, tuachane na hizi TV feki dizaini ya TBC
 
Mi sidhani kama nahitaji kusikia hizi ngonjera.............mbona hamna jipya??? Aaaagggggghhhhhhhhhhhh......hii serikali bana inatia kichefuchefu kweli.
 
JF nimewakubali.... yani in a few minutes mmeweza kurusha powerpoint slide muhimu.... hebu fungueni TV yaishe, tuachane na hizi TV feki dizaini ya TBC

Na tena wamerusha kutoka makao makuu ya jeshi, ujue JF ilivyotandaa
 
Hili jeshi letu limeshapoteza face mara nyingi sana. Hii ni dalili kuwa tuna genge la wahuni tu na hatuna jeshi. Huoni mfumo wa kijeshi ukifanya kazi kwenye matukio makubwa. Kusema kweli sasa hivi Tanzania tulivyo tukivamiwa na nchi kama Rwanda, watatupiga vibaya sana. Hatuna jeshi na hatuna serikali, tuna magenge ya wahuni tu wanaofikiria kuiba na kujitajirisha.

Toka tukio la Gongo la Mboto litokee, ni confusion tupu. Hujui msemaji wa serikali ni nani kwenye mambo kama haya. Mara mkuu wa mkoa, mara mkuu wa polisi, Mara mnadhimu mkuu wa jeshi, mara waziri mkuu, mara Rais, na wote ukifuatilia wanachoongea ni kuwa HAKUNA COORDINATION. NERVE SYSTEM YA NCHI HAIFANYI KAZI SASA HIVI NA NCHI IKO KATIKA PARALYSIS.

Kauli za viongozi zilikuwa zinachanganya. Wananchi; wengine walikuwa wanakimbia wengine wanarudi. Wengine wanaambiwa waende umbali wa kilomita kumi wengine wanaambiwa mambo yameisha. Kigamboni watu waliambiwa wakimbilie kandoni mwa bahari na wengi wali respond. Kwa tukio kubwa kama hili, mkuu wa nchi alikuja kuonekana baada ya masaa zaidi ya kumi. Na hakuwa na jipya linalotofautiana na walio mtangulia.

Maana yake ni kuwa command structure ya nchi haipo!! Tukae tukijua hilo. Haya mambo ya kujichanganya tunayoyaona ndo sababu yake hasa. Hakuna anayejua afanye nini. Kila mtu anasubiri amri kutoka juu, lakini hiyo amri ama haiji au ikija haieleweki!!
 
Back
Top Bottom