Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,150
- 18,810
Huwa najiuliza sana juu ya busara na hekima ya wengi wa viongozi wetu, na sasa suala hili limeangukia kwa uongozi wa JWTZ. Hivi kweli JWTZ walijiuliza kwa makini kabla ya kutoa katazo hadharanai kwamba ni marufuku kuandika habari za mgogoro wa DRC?
Katika karne hii unatoa katazo hama hilo - labda uwe mtu wa aina aliyepanda cheo kutoka private miaka ya 70 na sasa umekuwa na cheo kikubwa cha kukuwezesha kutoa amri za ujumla kama hii. Labda huko jeshini inawezekana, lakini uraiani utapata shida sana ukianza amri kama hizi. Uraiani hatuna watu waliomaliza darasa la pili wakapanda cheo kuwa ma judge katika mahakama zetu.
Kwanza, nikiandika habari za kweli na zenye kuthibitika juu ya mgogoro wa Rwanda, utanifanya nini, au utanishitaki kwa sheria gani?
Kwa maneno mengine - tatizo ni kuandika habari au kuandika habari za uzushi?
Kama ni suala la kuandika habari za uzushi - basi hilo ndilo lapaswa kushughulikiwa, sio kutoa amri ya ujumla kwamba hakuna kuandika kuhusu mgogoro wa DRC.
Nitawashangaa sana taasisi za habari kama watakaa kimya juu ya hili.
Amri ya JWTZ kupiga marufuku kuandika juu ya mgogoro wa DRC naifananisha na mambo yafuatayo;
Nchi hii bwana, kila mtu anakuja kivyake vyake tu!

- Baadhi ya madereva wanaendesha magari vibaya Dar - Moro na kusababisha ajali - Waziri anapiga marufuku kuendesha magari barabara ya Dar - Moro kwa madereva wote
- Baadhi ya wanaume wanapata mfadhaiko kwenye daladala na kuwafanyia vitendo vibaya wanawake - Waziri anapiga marufuku wanaume kupanda daladala
- My wife nyumbani anaunguza mboga - nampiga marufuku kunipikia!