mangikule
JF-Expert Member
- Jun 11, 2012
- 6,054
- 5,432
Ninakubali ila tungoje serikali yenye hekima 2015 itoe maamuzi ya hekima!!Kutokana na ukweli kwamba Jamii ya kimataifa imejiridhisha kuwa Raisi kagame anahusika moja kwa moja kwa kuwasaidia March 23(M23) kijeshi na misaada mingineyo ya ki-inteligensia na kusababisha kutokuwa na amani nchini congo,kuuawa kwa watu,kubakwa kwa wanawake na kusababisha wakongo kukimbia eneo la goma na mashariki ya kongo na kuwa wakimbizi basi Rais kagame anayo kesi ya kijibu ICC
Week iliyopita shirika la haki za binadamu duniani(HUMAN RIGHT WATCH-HRW) ilitoa repoti kwa kuwahoji hata baadhi ya askari wa kagame ambao walipewa amri kuvuka mpaka na kuwasaidia waasi wa M23,ripoti hiyo ilitoa takwimu kuanzia mwezi march watu 40 wameuawa na wanawake 60 kubakwa na waasi wa M23,serikali ya Kigali bila hata aibu ilikanusha madai haya na uhusika wake
Serikali ya washington vilevile ilitoa wito kwa Raisi Kagame kuacha maramoja kuwasaidia waasi wa M23.Hii lazima ikumbukwe ni mara ya pili juu ya tuhuma hizi kwa wale wanaofuatilia mambo mtakumbuka mwaka jana Rwanda iliwekewa vikwazo na serikali ya uingereza kwa kuhusika kwake na tuhuma hizi hizi
Ukweli wa mambo unajulikana Rais kagame anaendesha operations za kuiba madini nchini Kongo kwahiyo asingependa hata kidogo kuona kuna amani na ndio hata maana aliposikia Amiri Jeshi mkuu wa Tanzania anamrisha JWTZ-TPDF kwenda kwenye ulinzi wa amani katika kikosi cha umoja wa mataifa(MANUSCO) alileta chuki binafsi na kuanza kumtolea maneno ya kejeli alipoambiwa afanye negotiations/mediations na FDRL
Jamii ya kimataifa imeshaliona hilo huu ni muda sasa wa kagame kutafutwa na kukamatwa akajibu tuhuma za kuwa adui wa amani ya CONGO kwa manufaa yake binafsi hivo basi natoa rai JWTZ,MANUSCO kwa weredi mkubwa hakikisheni operations za congo mnaunganisha na kumkamata kagame dead or alive kwa sababu anayo kesi ya kujibu ICC