JUVIMA yaitaka Serikali kuwa sikivu kuhusu madai ya Katiba Mpya

Nicholas J Clinton

JF-Expert Member
Mar 13, 2014
877
486
Jumuiya ya Vijana wa chama cha NCCR Mageuzi (JUVIMA) wameitaka Serikali kuwa sikivu kusikiliza matakwa ya muda mrefu ya wananchi wake kuhusu katiba mpya.

Akizungumza makao makuu ya cha hicho jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa JUVIMA, Bw. Nicolas Clinton amesema kuwa takwa hilo la jamii ya Watanzania walio wengi tangu Serikali ya Awamu ya Pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi ni Katiba Mpya.

“JUVIMA tutaungana na yeyote mwenye mapenzi mema na nia njema na Taifa letu kudai Katiba Mpya usiku na mchana. Uhai wa Taifa hili, upo kwenye mikono ya Katiba Mpya na siyo kikosi kazi kinachomtumikia Rais,” Alisema Clinton.

Alisema Katiba ni uhai, kwamba Taifa hai, huongozwa na katiba hai, katiba ni kauli ya umma, inayotokana na umma kwa umma kuamua ujiongoze vipi.

Aidha Bw.Clinton aliongeza kuwa Katiba Mpya ndiyo jawabu la changamoto za kiuchumi, kijamii na kisiasa zinazotukabili, pia amesisitiza kwamba, madai ya Katiba Mpya si kwa sababu ya uchaguzi wa wanasiasa.

Aidha alisema JUVIMA inapinga hatua ya baadhi ya vyama na viongozi wanaodai Tume huru ya uchaguzi kwani ni mtoto wa katiba, na mtoto hawezi kumzaa mzazi wake.

"Katiba ni maisha halisi ya Mtanzani, Katiba inatakiwa imzungumzie mfugaji, mfanyakazi, mkulima na pia imzungumzie mtu mmoja mmoja na haki zake za msingi"Alisema

Alisema tume huru ya uchaguzi, ni sawa na kapunje kadogo ndani ya katiba. Tunapozungumzia katiba, tunazungumzia uhuru wa Bunge, Mahakama na mifumo ya uteuzi katika vyombo vya maamuzi, haki za kuishi, kufanya kazi, kutoa maoni na kupata habari, haki za wakulima, wafanyakazi, wafugaji n.k Mambo yote haya yatatokana na katiba na siyo tume huru ya uchaguzi.

“Tume huru ya uchaguzi inazungumzia wabunge wasiozidi mia tatu hamsini(350) katika nchi ya watu milioni sitini (60,000,000), Tume ya uchaguzi inazungumzia madiwani wasiozidi elfu kumi (10,000) katika Nchi ya watu milioni sitini (60,000,000) kudai Tume huru ya uchaguzi kabla ya katiba mpya ni kuuthibitishia umma ni kwa namna gani baadhi ya wanasiasa hawajui wajibu wao,” Alisema bw. Clinton

Hivyo Serikali kuanza mchakato wa Katiba Mpya haraka iwezekanavyo kutoka kwenye rasimu ya tume ya mabadiliko ya katiba mpya ya Jaji Joseph Warioba na wenzake.

Itambulike kwamba maoni ya wananchi kuhusu Tume huru ya uchaguzi, tayari tume ya Jaji Nyalari iliishatoa mapendekezo ambayo yapo kwenye makaratasi na yako wazi.

Screenshot_20220324-044925_Chrome.jpg
 
Wanajifanya mabingwa wa kuongea wakati huu mama kawapa ahueni, wakati wa mwendazake hakuna wote waliufyata

Nani aliufyata. Mboana Roma alitekwa na kina Lissu kulimwa risasi?. Hii nchi sio Mali ya mtu mmoja aamue Nani aongee na Nani asiongee. Ndio maana ilibidi aondoke maana alitaka kuleta Mambo ya Rwanda wakati huku Ni Tanzania.
 
Watanzania Mil.59,999,999 WALIUFYATA

Uliufyata mwenyewe. Huwezi kukimbizana na mwehu wakati anakurushia mawe bali unamuacha afanye vurugu maana wore mtaonekana wehu. Ndicho watanzania walichofanya.

Watu kukaa kimya haimaanishi wamekuogopa Bali wanakudharau na kukuona hamnazo.
 
Nani aliufyata. Mboana Roma alitekwa na kina Lissu kulimwa risasi?. Hii nchi sio Mali ya mtu mmoja aamue Nani aongee na Nani asiongee. Ndio maana ilibidi aondoke maana alitaka kuleta Mambo ya Rwanda wakati huku Ni Tanzania.
Alikufa natural death ambayo hata wewe utakufa regardless
 
Back
Top Bottom