Juu ya tuhuma kwa Zitto na kundi lake kutoka kwa Mamuya...

Status
Not open for further replies.
?hata kama mnasema anachafuliwa kaul ya kiongøz kusema eti anatokea kigoma ooh haogop kufa huo ni utoto na vitisho vya kijinga kama haogopi kufa ajiue
 
ZITTO usikubali kuwaachia chama hawa wababishaji wa siasa na wachumia tumbo,walifanya hivyo kwa Aman Kaburu safari hii hakikish wanachora chini.
 
hakuna kitu kama ushirikina kama watu wanavyojaribu kupotosha, watu wa kigoma ni watu wa kazi kazi, wanamaendeleo na uelewa wa hali ya juu.


Zzk ameteleza tu katika sentensi yake ya mwishoni, na watu wana-take advantage kum-attack; bado sikubaliani nae katika mambo kadhaa lakini naamini ni mtu muhimu sana kwa chadema; hata viongozi wenzie nao wana mapungufu yao; wakae pamoja wayamalize mambo hayo, watanzania tunataka ukombozi kutoka kwa mkoloni mweusi ccm.

Wana-ccm wengi wanaochangia kwenye hii mada wanajaribu kuongezea petrol kwenye moto kwa faida yao kwa kua chama chao kinapumulia mashine, yawezekana na wewe ni mmoja wao wana ccm ndio maana umeweka picha hiyo ambayo maelezo yake siyo sahihi... Na unachojaribu kumaanisha..... Tabia hiyo ni mbaya sana if not ujinga

zitto hakuteleza kwenye maneno yake,alikua anamaanisha

na ndio maana akakuambia pigia mstari maneno yale,,we kaa ukishangaa shangaa hivo hivo
 
tujiulize kwa nin wanachama wa ccm wanamtetea zito? Inaonesha wanajuana nae.shetan hawez kumuunga mkono yesu
 
Mkuu Ritz
Ulishakia dawa ya kutibu unafiki? Wanafiki ni wengi sana Chadema matokeo yake hawajielewi hata wanachosema; hivi ukiwa kijana upeo wako wa kupima baya na jema unakuwa pungufu ? Ben Saanane anatuhabarisha alikubali kutumiwa hapo hapo anadai hana price tag huo kama sio uwongo uliojichanganya na unafiki ni kitu gani? je usaliti alioufanya chini ya Zitto kama anavyodai ulikuwa na manufaa kwake binafsi au kichama? Hivi ni katika huu uchungu anauongelea mchumia tumbo Ben Saanane walikuwa ni wachaga tu? Hapakuwa na mzigua; mhehe, mngindo au msukuma? Leo hii ben ndio amejua kuwa kuna vikao vya chama hii ni baada ya kufundishwa na walimu wake; watu kama Ben Saanane trustworthy yao ni negative; utamuamini ben iwapo tu unasimamia kundi fulani kwa maslahi kama alivyosema kamanda Chris Lukosi huu ni msafara wa kenge wameanza kuwaengua mamba.

Chama
Gongo la mboto DSM
BEN SAANANE,
Amejitoa mhanga kwa kuleta hii mada ya kutungwa na wao wenyewe ili apate kwenda kinywani.Lakini mwisho wa kutumika ni mbaya sana
kibaya zaidi ni kwamba hii tamthiliya inapita leo au kesho na yawezekana isikumbukwe na yeyote hapa jf kutokana na mtindo wa matukio.
lakini uanasiasa wa ben na mamuya na zitto utaendelea kuwepo tena ndani ya chama kimoja.Hii italeta mpasuko mkubwa zaidi kusini na kaskazini.(kus na kas)
 
Aina hii ya watu wapo tangia enzi za Yesu .Yuda Iskarioti alimsaliti Yesu kwa tamaa ya hela,ila kusalitiwa kwa Yesu haikuwa mwisho wa maisha yake bali ni mwanzo wa maisha mapya ya ukombozi,Nandiyo maana kila baada ya ijumaa kuu huja pasaka.
 
ZITTO usikubali kuwaachia chama hawa wababishaji wa siasa na wachumia tumbo,walifanya hivyo kwa Aman Kaburu safari hii hakikish wanachora chini.

Zitto hawezi kuja na kubishana na kijana mdogo na kijakazi wa watu kama ben.Zitto hawezi kuachia chama
 
?hata kama mnasema anachafuliwa kaul ya kiongøz kusema eti anatokea kigoma ooh haogop kufa huo ni utoto na vitisho vya kijinga kama haogopi kufa ajiue

Ha hahahah!!!kwani wewe umekataliwa kusema unakotokea???
 
Nimefuatilia kwa simu nimeona kama nakosa ladha kamaili! Kwa namna ambavyo watu wamefunguka hapa,

tunapata kuwafahamu watu kwa rangi zao, ila of all sikutegemea @Dr Kitila Mkumbo! Na hapo ndio tunaona

udhaifu wa siasa za Tanzania? Kwanini wasomi kama Kitila na Zitto kuingia katika vita kwa gharama ya kutekea

kwa Tanzania? Kweli ubinafsi unatufikisha hapo? Ben Saanane umefanya vyema kukiri makosa uliyoyafanya

mwanzo. Sasa yakupasa ueleze yote katika vikao halali vya chama. Kwa namna hiyo utaisamehe nafsi yako na

utakuwa umekijenga chama imara!
 
Last edited by a moderator:
Fisadi said:
ZITTO ni wa hapa hapa! Hawezi kuondoka CDM kwa propaganda zenu chafu...Na mkimgusa tu, vipande vipande. Peleka agenda ya kumfukuza muone kivumbi! Zitto ni CDM na CDM ni Zitto. Vita vya panzi hivi ...
Fisadi said:
Chadema ni kama nyumba iliyojengwa kwa barafu, jua likiwaka itayeyuka yote ipotee. Na hilo ndio linalotokea sasa, heri yangu mie nimeamua kurudi home mapema kabla boti haijazama
Mpiganaji said:
Umeamua kuja kupima upepo mkuu? Hawajambo magamba wenzio? Waambie huku intelijensia ya chama ni kali imenasa mamluki wote waliokuwa mafichoni
Fisadi said:
Kuna wengi viongozi wa chadema hawakutaki na mimi binafsi niliwahi kuambiwa nisije kupoteza muda kuwasiliana na wewe kwa sabau ni nyoka. Hilo vumbi linalotimka huko Chadema ukiendelea kubaki nalo litakusababishia kifua kikuu ndugu yangu.
Mpiganaji said:
Umefanya vema sana kumkaribisha kurudi utumwani (Misri). Namsihi Zitto auchukue ushauri wako kwa faida yake...
Fisadi said:
Kijana, Wewe unazani hivyo lakini siku nikisema nazani wengi mtaona aibu.
Mpiganaji said:
...nikukate kilimi kuwa huna lolote zito unalolijua la kukiyumbisha cha Chadema. Tumia hata akili ya kitoto... kitengo cha ujasusi cha chadema kinamjua kila mwanachama kuanzia utosi hadi unyayo! Na wewe ukiwemo, kitengo kinakujua kuanzia nywele hadi nyayo!
Duh, mambo hayo...na baado!
Mpiganaji said:
Sasa Naiona CHADEMA Imara than ever before, ikiwa karibu kabisa kuchipua...
Fisadi said:
La hasha, hilo haliwezekani...tutahakikisha hata panya hawasalimiki!
Mpiganaji said:
... Kama vilemaumivu ya Mama anayekaribia kujifungua maumivu yasiyopimika ... BUT alas ... soon We have a Baby Boy!!!
Kusema kweli nimefuatilia huu mjadala toka mwanzo hadi mwisho na ninachoweza kuchangia ni jinsi nilivyofarijika, naamini ukombozi wa kweli sasa unabisha hodi. Kama anavyosema mchangiajo hapo juu haya maumivu ni kama ya Mama anayekaribia kujifungua! Kila siku nimekuwa nikiombea hali kama hii itokee, atokee mtu kama WASIRA, atokee mtu kama Chris Lukosi, atokee mtu kama MAMUYA, atokee mtu kama Zitto, atokee mtu kama ben, atokee mtu kama Nape...nawapeni hongera nyingi kwa kufanikisha lililoshindikana...kumfunga paka kengele hata kama paka mwenyewe ni paka shume.

Mafisadi wa CCM kwa upofu wao wanashangilia na ni lazima washangilie...si wameshiba wakavimbiwa? si wamelewa wakawa chakari? Yanikumbusha tamthilia ya mwandishi, Janes Hadley Chase The guilty are always afraid! Kama nilivyosema hapo awali ben kaamua kumkaanga kondoo mwitu, kwa nini ahangaike kununua mafuta? Yeye akae kitako akisubiri kitoweo kinavyojikaanga kwa mafuta yake mwenyewe. Hwa wenzetu wengine wanalinganisha hii na kum-grab the bull by its horns! Asanteni tena wote kwa kuturudishia hilo tumaini lililoanza kupotea hivi hivi tukishuhudia.
 
hapa naona kuna watu wanatafuta umaarufu tu kupitia wengine ambao ni wazoefu, hivi nyie watu mnajua kua watanzania wanaona kua CHADEMA ndio chama pekee ambacho kitawaleteea unafuu kwenye kila kitu??? acheni upuuzi mjenge chama,kwa ambao hamjatoka tafuteni njia nyingine acheni kuchafuana

nadhani hili umeliona vyema kabisa.Kuna watu wanatafuta posho ya x mass.Lakini ndio ujana huu na kutumika ndio huku.Zitto wewe ni hero katikati ya simba wenye njaa kali
 
Nimefuatilia kwa simu nimeona kama nakosa ladha kamaili! Kwa namna ambavyo watu wamefunguka hapa,

tunapata kuwafahamu watu kwa rangi zao, ila of all sikutegemea @Dr Kitila Mkumbo! Na hapo ndio tunaona

udhaifu wa siasa za Tanzania? Kwanini wasomi kama Kitila na Zitto kuingia katika vita kwa gharama ya kutekea

kwa Tanzania? Kweli ubinafsi unatufikisha hapo? Ben Saanane umefanya vyema kukiri makosa uliyoyafanya

mwanzo. Sasa yakupasa ueleze yote katika vikao halali vya chama. Kwa namna hiyo utaisamehe nafsi yako na

utakuwa umekijenga chama imara!
Usipoteze muda kuamini hiki kitu kamanda,Bado hujasikia upande wa pili.Hii ni tamthiliya ya viongozi wa juu wa chadema walipanga kumchafua zitto wametumia vijana wao wa nyumbani \mamuya na Ben kufikisha ujumbe
 
JK si alikuwa analindwa na majini (via sheh Yahaya) mnashangaa nini zzk kulindwa na hayo hayo hali wao ni marafiki?
 
Hapa kunajambo najambo lenyewe ndio limefikia mwisho!!Watu wanaulizana mbona M4C kunawatu hawaonekani?Sasa majibu yanaanza kuja taaratibu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom