Juu ya tuhuma kwa Zitto na kundi lake kutoka kwa Mamuya...

Status
Not open for further replies.
Ben na mamuya wamefanya kazi yao kwa ufanisi nadhani leo wanakula bata mitaa ya sinza.lakinini Zitto amesema kulamba visigino miguu ya watu na kutumika ni hatari kwa siasa zako binafsi \ben/mamuya
 
dah!kama ungekua karibu tungeunda ka m 23 ketu dhidi ya huyu jamaa, nikizikumbuka kauli yake(zzk) "tunajiandaa kushika dola" khaah! labda ya marekani,,hakuna cha kushika dola wala nini tena eti "nitakuwa wa mwisho kukisaliti chama" kumbe unafki mtupuu.. ni ili achote akili za watu tu, huyu jamaa si wa kuaminiwa tena

Na wewe umeamini hii tamthiliya
 
dah!kama ungekua karibu tungeunda ka m 23 ketu dhidi ya huyu jamaa, nikizikumbuka kauli yake(zzk) "tunajiandaa kushika dola" khaah! labda ya marekani,,hakuna cha kushika dola wala nini tena eti "nitakuwa wa mwisho kukisaliti chama" kumbe unafki mtupuu.. ni ili achote akili za watu tu, huyu jamaa si wa kuaminiwa tena

huyu zito ilisemekana anataka kwenda NCCR, ishu ikastukiwa kafulila akasepeshwa sasa ameamua kukomaa na cc CDM aende akaazishe chama chake na kafulila pamoja na Hamad rashid
 
Am not undrstanding a kind of politics is underway at CHADEMA.well if at least fine everything will be exposed for the benefit of the party on the long run
 
Mkuu chama,
Ukiangalia kwa makini hii ngoma inachezwa kikanda zaidi hao watu watatu ambao ni waasi wanaonekana eti mashujaa halafu wamemuingiza Kitila Mkumbo, naye anaambiwa msaliti cha kushangaza hakuna msaliti kutoka kaskazini.

Kuna kamanda mmoja naye kamtaja Ritz, naye anahusika.

Nadhani ili ni somo kwa kina Mohamedi Mtoi, Mwita Maranya.

Mkuu Ritz
Ulishakia dawa ya kutibu unafiki? Wanafiki ni wengi sana Chadema matokeo yake hawajielewi hata wanachosema; hivi ukiwa kijana upeo wako wa kupima baya na jema unakuwa pungufu ? Ben Saanane anatuhabarisha alikubali kutumiwa hapo hapo anadai hana price tag huo kama sio uwongo uliojichanganya na unafiki ni kitu gani? je usaliti alioufanya chini ya Zitto kama anavyodai ulikuwa na manufaa kwake binafsi au kichama? Hivi ni katika huu uchungu anauongelea mchumia tumbo Ben Saanane walikuwa ni wachaga tu? Hapakuwa na mzigua; mhehe, mngindo au msukuma? Leo hii ben ndio amejua kuwa kuna vikao vya chama hii ni baada ya kufundishwa na walimu wake; watu kama Ben Saanane trustworthy yao ni negative; utamuamini ben iwapo tu unasimamia kundi fulani kwa maslahi kama alivyosema kamanda Chris Lukosi huu ni msafara wa kenge wameanza kuwaengua mamba.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
tuambie,,kwani huko kwenu hizi imani za kishirikina ni kweli zipo au kabwe tu anawaletea uchuro??

Hapa akiwa anaaga huko mwandiga


Hakuna kitu kama ushirikina kama watu wanavyojaribu kupotosha, watu wa kigoma ni watu wa kazi kazi, wanamaendeleo na uelewa wa hali ya juu.


ZZK ameteleza tu katika sentensi yake ya mwishoni, na watu wana-take advantage kum-attack; bado sikubaliani nae katika mambo kadhaa lakini naamini ni mtu muhimu sana kwa CHADEMA; hata viongozi wenzie nao wana mapungufu yao; wakae pamoja wayamalize mambo hayo, watanzania tunataka ukombozi kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.

Wana-CCM wengi wanaochangia kwenye hii mada wanajaribu kuongezea petrol kwenye moto kwa faida yao kwa kua chama chao kinapumulia mashine, yawezekana na wewe ni mmoja wao wana CCM ndio maana umeweka picha hiyo ambayo maelezo yake siyo sahihi... na unachojaribu kumaanisha..... tabia hiyo ni mbaya sana if not ujinga
 
huyu zito ilisemekana anataka kwenda NCCR, ishu ikastukiwa kafulila akasepeshwa sasa ameamua kukomaa na cc CDM aende akaazishe chama chake na kafulila pamoja na Hamad rashid

Huyu zitto yeye mwenyewe anaambiwa ccm,mara hauma,sasa nccr kweli huyu ni mtu wa kitaifa mbona vyama vinamng'ang'ania.\Zitto wewe unakituchatofauti kama ni sokoni upo juu sana.wanaokuchafua wacha wafanye kazi yao
 
Ndugu Zitto, Ben, Mamuya, Kitilya na 'Maslia',

Napenda kuwakumbusha kwamba Mwl J. K. Nyerere aliendesha harakati za kuikomboa nchi yetu akiwa kijana. Ninasikitika sana, tena sana kusikia mipango na mikakati kabambe ya kutaka kukwamisha harakati za ukomozi wa pili wa nchi yetu, UKOMBOZI AMBAO HAUPUKIKI! Nasema hauepukiki kwa sababu ya hali halisi ya maisha ya Mtanzania wa leo, mtanzania ambaye hana uhakika wa mlo wa siku, mtanzania ambaye hana maji ya uhakika, mtanzania ambaye hana uhakika wa kusoma, mtanzania ambaye hana uhakika wa matibabu (hili linaniuma zaidi kwani kwenye hospitali kubwa kama Muhimbili hupati huduma mpaka uzungumze vizuri!), mtanzania ambaye hana uhakika wa kusafiri kwa njia rahisi (gari moshi) achilia mbali kusafirisha mizigo, mtanzania ambaye hana umeme achilia mbali mgawo wa umeme.

Mimi kama kijana msomi (sijisifii) nilidhani vijana tumebeba matumaini ya watanzania walio wengi (maskini) na tunapigana kwenda mbele kuleta mwanga lakini kumbe ni kinyume chake. Mimi ni mojawapo ya watu ambao walikuwa nyuma ya Zitto nikiamini kuwa ni mpiganaji wa kweli, lakini hivi karibuni nimepoteza matumaini na huyu kijana mwenzangu kwa sababu ya hatua na misimamo yake mbalimbali ambayo amekuwa akionesha waziwazi ambayo kwa maoni yangu si matarajio yangu kwa mwanamapinduzi. Malumbano haya yamenisaidia kukubaliana na wasiwasi wangu juu ya Zitto. Naamini Zitto atanielewa kuwa simhukumu ila historia ndio itakayomhukumu.

Mwisho, nakishauri chama cha CHADEMA kuchukua hatua madhubuti na za busara kusaidia kunusuru chama hiki kilichobebe matumaini mapya kwa Watanzania. Ninawatia moyo wote wenye mapenzi mema na nia njema ya kupigania haki, usawa na ustawi wa Mtanzania popote alipo, Mungu yupo upande wetu! Huu ni mwanzo tu, wasaliti wote wataumbuka na watajitaja wenyewe kama hawa walivyofanya.

Kamwe tusikubali kurudi nyuma kwa sababu ya wanaharakati uchwara hawa wanaohangaika kila kukicha ili kurudisha nyuma harakati za ukombozi wa Tanzania yetu. kumbukeni, bado tuna safari ndefu na daraja refu la kuvuka ili kuikomboa nchi kwa mara ya pili baada ya miaka hamsini ya UKIRITIMBA, UZANDIKI, na UFISADI

Mungu ibariki CHADEMA
Mungu ibariki TANZANIA
Mungu waumbue WANAFIKI
AMEN.
 
Si amini kama unatetea wasaliti, Yaani mtu alikua msaliti tena kwenye Genge la wasaliti leo unamuona Jembe?
Hata Paulo ndiye aliyekuwa Sauli akiongoza anti christ persecutions!. Petro anayeelezewa kuwa "wewe ni mwamba na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu", alimsaliti Yesu kwa kumkana mara tatu kabla ya jogoo kuwika!.
P.
 
Kuna baadhi ya pro-ccm na masalia wa Zitto ambao wanataka kudiverge mjadala eti hapa sio mahali pake, basi kwa taarifa yenu huu uchafu ulianzia humu mitandaoni na wale vijana masalia wa Zitto basi itakuwa vizuri pia tukawachana live mitandaoni.
Pia kwa hoja ya kukivuruga chama huo pia ni unafiki mkubwa mithili ya shetani kwani kipindi kile wale masalia wa Zitto (TUNTEMEKE) wanakuja kuzusha humu tuhuma za uzushi kwa viongozi wa CHADEMA like Mbowe, Slaa na Mrema hivi inamana hawakujua kuwa huko nako ni kukivuruga chama? Sasa mbona hawakusema haya mambo yaende kwenye vikao vya chama kama sio unafiki ni nini huo?

Leo hapa ni MBIVU au MBICHI YANI HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.
 
Last edited by a moderator:
Tulisema tukaitwa Wanga, wakorofi, wachawi, vigagula na kila neno. Ni waka mmoja na ushee tangu tuyasema. Haya ni baadhi tu ya maonyo na ushauri. Kwa mengi tembelea Duru za siasa

Nilitaraji wangekuwa na brand ya uwajibikaji bila kusukumwa, bahati mbaya hilo halijatokea. Ingawa inaonekana hali ni shwari, kitendo cha kushindwa kusimamia kanuni kama ilivyo kwa Juliana Shonza na Shibuda kinaharibu taswira ya chama na kujenga kambi zitakazoleta machafuko.

Nasema kama hawatabadilika ndani ya miezi 18 kutatokea mtafaruku mkubwa sana. Ni suala la muda tu.
.....................................

CDM wafanye nini kwa wakti huu:
1. Kumfukuza Shibuda mara moja. Hili litajenga yafuatayo

a} Watu kuheshimu taratibu za chama na kujua kuwa chama ni watu na si mtu Katika kufanya hivyo, CDM wasifikirie idadi ya wabunge au mgao wa ruzuku. Waangalie hatari mbele yao

b) Litawaaminisha watu kuwa CDM ni chama chenye uwezo wa kuchukua maamuzi magumu bila kusita ili mradi yawe sahihi na kwa wakati sahihi

d)Litaepusha mvurugano(distraction) wakati huu chama kikihitajika kila kona ya nchi

Chadema wajiepushe na nini?
Chadema............Huu ni udhaifu mkubwa sana ambao mimi ninauweka wazi hata kama utaudhi au kuuma.

Hii inaashiria tatizo kubwa ambalo hatulioni na ipo siku litajitokeza. Litakisambaratisha Chama.
Mfano mzuri ni CUF ya Seif ambayo sasa inafutika. Tumeyaona NCCR ya Mrema pia.
Mwenendo ulikuwa huo huo kuwa chama hakifanyi kazi kama taasisi bali kuwa 'assembly of personalities'.

Siyaandiki haya kwa kuangalia tukio moja, nina mlolongo wa matukio na mengine nimeyaandika wazi. Chadema kama chama cha upinzani ............. Lakini kubwa zaidi kuna tatizo!
 
hapa naona kuna watu wanatafuta umaarufu tu kupitia wengine ambao ni wazoefu, hivi nyie watu mnajua kua watanzania wanaona kua CHADEMA ndio chama pekee ambacho kitawaleteea unafuu kwenye kila kitu??? acheni upuuzi mjenge chama,kwa ambao hamjatoka tafuteni njia nyingine acheni kuchafuana
 
[/COLOR]labda atudhibitishie, kwa ushahidi timilifu, kuwa tuhuma za kuwa yeye ni mghalula si za kweli. vinginevyo labda aka-rais ghalula wenzie
Lugha zetu Tanzania ni nyingi mno, kiswahili nacho ,kinakuwa kila siku, maneno mapya yanaongezeka, nadhani niko nyuma ya wakati naomba ufafanuzi juu ya maneno hayo MGHALULA
 
baada ya zzk,dr kitilla mkumbo atakaefuata ni prof safari na tundu lissu ili wenye chama wabaki wenyewe na wafanye ya kwao.


naona sasa umeacha kumtumikia boss wako zitto sio??
 

Attachments

  • AKIWA NA JK.jpg
    AKIWA NA JK.jpg
    52.6 KB · Views: 55
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom