Juu ya DOWANS: Mwakyembe ashangaa kutaka kulipa matapeli

Mwakyembe mwenyewe mwizi au tuseme kama wazungu.-----" SEND A THIEF TO CATCH A THIEF ".Wote corrupt...:Cry:
 
Kesi nyingine hii hapa Dowans Holdings S.A. et al v. RDEVCO, LLC :: Justia Dockets & Filings
Tutakufa. Je kulikuwa na ulazima kuvunja mkataba uliobakisha miezi 12 kuisha? Mwanasheria mkuu alikuwa wapi kuipa serikali ushauri wa kiufundi kabla ya kuvunja mkataba? Na hakika kisiasa tulishangilia sana na kumwona Dr. Idrissa shujaa,japo alituonya yatakayotokea tusimlaumu, kumbe tunameza ndoana. Imetukwama sasa nawajuaji wanavuta mshipi.
 
Pasco pamoja na uelewa wangu mdogo wa sheria lakini nnakumbuka vizuri kipengele kinachosema hamuwezi kukubaliana kuvunja sheria. Hii maana yake nini? Nni kwamba mfano kima cha chini cha mshahara ni Tshs 90,000.00 Lakini mimi kwa shida zangu tukakubaliana na kusainishana kulipwa Tshs 50,000.00 Halafu say baada ya miaka 5 nikaibuka kukushtaki kunipunja mshahara hakuna mahakama itakayoamuru eti sina kesi kwa sababu tulisainishana. Kifupi ni kwamba mkataba wetu ulikuwa illegal.

Tuje kwenye Dowans, ukiisoma vizuri hoja ya Mwakyembe, objectively na bila ushabiki utagundua kwamba mkataba kati ya Tanesco na Dowans ulikuwa illegal, simply kwa sababu Dowans ni kampuni ya kitapeli na hilo lilithibitishwa na kamati ya bunge yeye akiwa mwenyekiti. Sasa sijaelewa hapo upopulist uko wapi. Please nieleweshe.

Kaka umesema vizuri swala ambalo wengi tunajiuliza,

Unasema mkataba ulikuwa Illegal, NI WEWE UMESEMA au ndivyo ulivyo?

Kama ulikuwa ILLegal kwa nini walienda mahakamani in the first place?
Je ICC iko biased? je anajua mkataba ulikuwa illegal?
Je watetezi wa TANESCO hawakulijua hili??

Mpaka kesi imeenda ICC,ni kuwa huo mkataba ulisainiwa kwa misingi ya kimataifa, then illegality hapa inaweza kuwa questionable, au ICC credibility might be in question!

Au mawakili wa TANESCO walikuwa so silly kiasi cha kutoweza kugundua hilo?

Mkataba ulivunjwa na bunge siyo? kwa nini TANESCO hwakuchukua zile sababu na kuziwasilisha??

Hoja ya dowans walisema ulivunjwa kwa pressure za kisiasa! could this be true?

maana tusipopata utatuzi hapa, then we have many cases ahead us in this world of globalization and every time tutakuwa tunatafutana uchawi
 
I have got a Different take on this one.........

Hata kama hawa jamaa hawatalipwa hili tu halitoshi.....
Lazima kuna watu waliboronga...... na lazima kuna wahusika/wamiliki wa DOWANS hapa nchini; I wont be happy until we know the true owners of DOWANS na wawajibishwe ili liwe fundisho, we have got CANCER in our system and the problem with CANCER if left alone it will spread.. SO WE NEED TO CUT THE ORGANS WHICH HAVE BEEN INFECTED WITH CANCER....

Kutolipa pekee will save us money, but getting rid of this CANCER will save us a lot of more for generations to come.
 
Mwakyembe aibua mazito DOWANS

Tuesday, 11 January 2011 20:07 newsroom

* Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia
* Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga
Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary
Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.
ìUpande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo,î alisema.
Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.
Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.
ìKwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu,î alisema.
Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.
Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.

Wakuu kama haya yote yanajulikana ilikuwaje Ngeleja alikuja kuthibitisha hayo na kuwabambikia watu wasiokuwa wahusika ili kuthibitisha tu ulipwaji wa hizo fedha?
Nakumbuka katika maelezo yake wakati wakuwataja kama wamiliki wa Dowans alisema hao ndio wakurugenzi wanaohusika na masuala yote yanayohusu Dowans.je ni kweli Board of Directors huwa wamiliki wa Kampuni husika?

Kweli wanasheria tusaidie tuondokana na huu wizi wa Kikwete na bwana mdogo Riziwani wasiokuwa na huruma ya utu
 
Kesi nyingine hii hapa Dowans Holdings S.A. et al v. RDEVCO, LLC :: Justia Dockets & Filings
Tutakufa. Je kulikuwa na ulazima kuvunja mkataba uliobakisha miezi 12 kuisha? Mwanasheria mkuu alikuwa wapi kuipa serikali ushauri wa kiufundi kabla ya kuvunja mkataba? Na hakika kisiasa tulishangilia sana na kumwona Dr. Idrissa shujaa,japo alituonya yatakayotokea tusimlaumu, kumbe tunameza ndoana. Imetukwama sasa nawajuaji wanavuta mshipi.

Msavila, ahsante sana, ni mmoja wa wachangiaje wachache humu JF wenye muono huo.
 
Kuna mtu alisema Dowans ni kaburi la JK.

KAZI IPO MWAKA HUU
Habari za Kitaifa

JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd April 2009 @ 07:30 Imesomwa na watu: 13657; Jumla ya maoni: 10

Habari Zaidi:
· Chadema ruksa ibada ya mazishi
· Wahadhiri UDOM waendeleza ‘kikao’
· Mbunge amwaga chozi hadharani
· Serikali yatoa pole kwa waliouawa Arusha
· Pinda asisitiza kuimarishwa kwa uhusiano na Msumbiji
· Dk. Shein asamehe wafungwa kuadhimisha Mapinduzi
· Chambo ‘akimbizwa’ na mabango ya kero Tazara
· Serikali yapiga marufuku wanafunzi kudaiwa michango
· Safari za treni reli ya kati zasimamishwa
· Tanzania kutoa shahada ya uzamili ya Ustawi wa Jamii
· Mti wa mnazi waua
· Kesi ya Katiti sasa kupangiwa tarehe
· Kesi ya wadaiwa wa mauaji ya mhadhiri Januari 25
· Ugawaji wa vocha usiendeshwe kwa itikadi-Takukuru yaonya
· DC aonya magendo vocha za ruzuku
· Uhamiaji waaswa kusaidia wasiojiweza
· Wathamini Africare wagomea posho
· Wazoa tope Kigoma wazua jambo makazi ya watu
· Wajitolea kulifanyia usafi Jiji la Tanga
· Tanga waichongea bandari Dar es Salaam kwa Waziri Nundu

Habari zinazosomwa zaidi:
· Balaa lingine kwa Chenge
· Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
· Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
· ‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
· Vatican yamvua jimbo Askofu
· Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
· Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
· Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
· Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
· JK apigilia msumari wa mwisho Dowans

Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha malumbano kuhusu ununuzi wa mitambo ya Kampuni ya kufua umeme ya Dowans Limited. Alitoa mwito huo jana katika hotuba yake ya kila mwisho wa mwezi kwa taifa ambapo alilipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa uamuzi wake wa kuachana na ununuzi wa mitambo hiyo.

"Nawapongeza viongozi wa Tanesco kwa uamuzi wao wa busara wa kuachana na nia yao ya kununua mitambo ya Dowans. Wameyasoma vizuri mazingira na nyakati na kufanya uamuzi mwafaka. "Pili, niwaombe wanasiasa wenzangu kuwa, maadam waliokuwa na nia ya kununua mitambo hiyo hawanayo tena, suala hili limemalizika. Sioni sababu ya kuendelea kulumbana, kutiana vidole machoni na kutoleana maneno makali na mengine hata hayastahili kusemwa," alisema.

Aliongeza kuwa hali hiyo imewatia hofu wananchi kwa jambo lisilokuwapo tena na kuwataka wanasiasa wahifadhi nguvu zao na bongo ili wawafanyie wananchi mambo yenye tija kwao. "Wanalo jukumu kubwa la kujiletea maendeleo kwa lengo la kujiondoa kwenye umasikini na kuwa na hali bora ya maisha yao. Uongozi wetu wanasiasa unahitajika sana katika juhudi zao hizo.

Tuelekeze nguvu zetu na maarifa yetu huko. Wapeni pumzi wananchi kutokana na malumbano haya," alisema. Aliongeza kuwa kuhusu tatizo la umeme lililopo sasa, tayari Wizara ya Nishati na Madini imeshaanza kuchukua hatua ambazo zinaonyesha kuwa na mwelekeo wa kutia matumaini. "Naamini tutafanikiwa. Tukiwa tayari, taarifa itatolewa.

Penye nia pana njia," alisema Rais. Alibainisha kuwa kwa takribani miezi miwili sasa, umeme umekuwa gumzo kubwa nchini ambapo mjadala umekuwa wa namna mbili. Kwanza, kuhusu Tanesco kununua mitambo ya Dowans ya Ubungo. Na pili, kuhusu mgawo wa umeme unaoendelea tangu Machi 26 mwaka huu mpaka sasa hasa Dar es Salaam na wilaya jirani.

Alisema taarifa aliyopewa jana ni kuwa hitilafu ya mitambo iliyosababisha mgawo ni kubwa hivyo huenda ikachukua mpaka wiki mbili au tatu au zaidi kutengemaa. "Maana yake ni kwamba mgao utaendelea kuwepo kwa kipindi hicho ... mgao huu hauna uhusiano na ile hadhari aliyoitoa Dk. Idris Rashid, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, alipokuwa akizungumzia suala la Dowans kuwa nchi inaweza kuingia kwenye giza siku za usoni," alisema.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Tanesco, mfumo wa umeme nchini, kwa sasa, hauna ziada ya umeme unaosubiri kutumika kama akiba, alisema. Umeme wote unaozalishwa nchini hutumika na wala mahitaji halisi hayajatoshelezwa. Kimsingi umeme unaopatikana na kutumika ni chini ya mahitaji. Alisema ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata na kutumia umeme wakati watu wengi sana wanaohitaji umeme bado hawajapata.

Hata hivyo, alisema wakati wote serikali kwa kushirikiana na Tanesco, imekuwa na mipango ya kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini. Akifafanua kuhusu kauli ya Rashid, kwamba uamuzi wa kuachana na Dowans unaweza kusababisha nchi kuwa gizani hapo baadaye, alisema ilileta hofu kubwa katika jamii. "Nataka kuwatoa hofu na kuwahakikishia Watanzania wenzangu wote kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuhakikisha kuwa nchi yetu haifikii hatua hiyo.

"Tutahakikisha nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zitaendelea kama kawaida. Kuhusu hali ya chakula, Rais alisema bahati mbaya sana mikoa inayopata mvua za masika hivi sasa hazikupata mvua nzuri wakati wa msimu wa mvua za vuli mwaka jana. Na kwa sababu hiyo, kilimo katika mikoa hiyo kimeathirika, mavuno yamekuwa chini ya wastani na wako baadhi ya wakulima ambao hawakujaaliwa kupata chochote kabisa.

Katika hali hiyo basi, kama katika msimu wa masika hali itakuwa chini ya wastani, ni dhahiri kutajitokeza tatizo kubwa kwa upande wa upatikanaji wa chakula na mapato ya wakulima kwa jumla. "Napenda kuwahakikishia kuwa serikali inafuatilia kwa karibu hali hii na tumekuwa tunajiandaa kuchukua hatua zipasazo," alisema. Kuhusu msukosuko wa uchumi wa dunia na hasa mkutano wa Kundi la Nchi Ishirini Tajiri Duniani (G-20) ambao unaanza leo London, Uingereza, alisema umeitishwa kutafuta njia za pamoja za kukabili kudorora kwa uchumi duniani.

"Uchumi wa dunia sasa hivi unapita kwenye kipindi kigumu kuliko wakati wowote katika historia ya dunia. Hali hii isipodhibitiwa kwa haraka na kwa umakini, itakuwa na athari kubwa ya kushusha viwango vya hali ya maisha ya watu katika nchi zote duniani tajiri na masikini. Matajiri watakuwa masikini na masikini watakuwa fukara zaidi," alisema. Alisema kunahitajika hatua thabiti zichukuliwe na hatua hizo ziwahusishe na kunufaisha wadau wote. Nchi tajiri duniani zinao wajibu mkubwa zaidi kuhakikisha kuwa wanadhibiti hali ili uchumi wa nchi zao usiendelee kudorora.

"Nchi tajiri zimekuwa zinachukua hatua za kunusuru uchumi wa nchi zao na bado wanaendelea. Bahati mbaya nchi zetu masikini ambazo hazina uwezo wa kuwa na mipango kama hiyo, pamoja na ukweli kwamba nazo pia zinahitaji sana, bado hazijasaidiwa," aliongeza. Pia alielezea masikitiko yake kwa ajali tatu zilizotokea hivi majuzi, ya magari Mbeya; ya treni mbili zilizogongana Dodoma na ya mgodi kufukia wachimbaji, Geita.

"Kwa ajali zote hizo tatu, moyo wangu uko pamoja na familia za wafiwa na waliojeruhiwa. Majonzi yao ndiyo majonzi yangu. Na machungu yao ndiyo machungu yangu. Tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu wetu hao mahali pema peponi. Amin!" Alisema na kuwaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa taifa.

hoja ya mwakyembe ya richmond kuwa fake si ndio hiyo imepigwa mweleka puuu miguu juu kichwa chini au hamjasoma hukumu aliyotum invisible. tutafute sababu zingine
 
Mwakyembe aibua mazito DOWANS

Tuesday, 11 January 2011 20:07 newsroom

* Ahoji uhalali wa kampuni ya kitapeli kulipwa fidia
* Wanaharakati kwenda mahakamani kuipinga
Na Bakari Mnkondo na Furaha Omary
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza suala la kampuni ya kufua umeme ya Richmond, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kuhoji uhalali wa kampuni ya Dowans, ambayo ni ya kitapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake. ìNikiwa mwanasheria ninasubiri kwa hamu maazimio ya Mahakama ya Kimataifa ya Biashara (ICC) yasajiliwe Mahakama Kuu ili kuona maamuzi ya kuilipa Dowans yalifikiwajeÖ nataka kujua msingi wa tapeli kulipwa fidia kwa utapeli wake?î amesema. Alitoa maoni yake jana kuhusu sakata la Dowans baada ya kutafutwa na gazeti hili kwa muda mrefu. Hivi karibuni ICC ilifikia uamuzi wa kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuilipa kampuni ya Dowans sh. bilioni 97 kutokana na kuvunja mkataba kinyemela. Baada ya uamuzi huo, suala hilo lilifikishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye alitoa ushauri kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, wa kukubali serikali kuilipa Dowans endapo uamuzi wa ICC utasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kwa kauli hiyo, Dk. Mwakyembe, ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, anaungana na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, sasa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupinga kampuni ya Dowans kulipwa kiasi hicho cha fedha.
Akifafanua kuhusu msimamo wake wa kitaalamu, ambao alisisitiza ni tofauti na wa kisiasa, Dk. Mwakyembe alisema ana shauku ya kujua ni kwa namna gani serikali imepoteza kirahisi kesi hiyo, ambayo alisema hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria angeweza kuisimamia na kushinda.
ìUpande wa kisiasa sina tatizo wapo wa kulizungumzia, lakini kitaalamu nitalizungumzia kwa kina kwa kuwa nipo kwenye taaluma ya sheria kwa miaka 20 nikiwa mwalimu. Ningependa kujua msingi wa ICC kufanya lililo batili jana kuwa halali leo,î alisema.
Alisema kamati teule ya Bunge ilimaliza kazi kwa kutoa maazimio kadhaa, ambayo hadi sasa hakuna lililofutwa, na moja ya maazimio hayo ni kuiona Richmond ni kampuni hewa, hivyo kupendekeza ifutwe kwenye orodha ya kampuni za Tanzania na Oktoba, 2008 ilifutwa rasmi.
Dk. Mwakyembe alisema anasubiri kuona ICC ilimuonaje mmiliki wa Dowans Holdings SA, iliyosajiliwa nchini Costa Rica, ambako serikali ya nchi hiyo ilisema haimtambui kwa kuwa hana anuani wala ofisi.
ìKwenye kamati tulifanya utafiti wa kina na serikali ya Costa Rica ilitueleza mmiliki wa kampuni hiyo hajulikani kwa jina, ofisi, anuani ya posta wala namba za simu,î alisema.
Dk. Mwakyembe aliyewahi kuwa mwalimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema walichoambulia Costa Rica ni kutajwa jina la Bernal Zamora Arse, anayemiliki kampuni takriban 100 zenye kuishia na SA, lakini hazielezi zipo jengo gani, nyumba ama kumiliki gari au pikipiki.
Alisema kutokana na ukweli huo, anashangazwa kuona uamuzi wa ICC ulivyofikiwa, na kuhoji fedha hizo zitalipwa kwa nani?. Dk. Mwakyembe alisema anasubiri uamuzi huo usajiliwe ili apate fursa ya kuupitia kwa kina na kuoana hatua za kuchukua kama mwanasheria.
Wakati huo huo, wanaharakati kupitia Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wanakwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kupinga amri ya TANESCO kuilipa Dowans fedha hizo, wakisema haina uhalali wa kulipwa, kwa kuwa ilishafahamika kuwa Richmond iliyoirithi ni kampuni hewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, wakili Francis Kimwaga, alitangaza hayo jana mjini Dar es Salaam, alipotoa tamko la wanaharakati kuhusu mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri hilo la Dowans. Alisema katika kesi waliyotarajia kuifungua jana, wanapinga kusajiliwa kwa uamuzi wa ICC.
Alisema kituo hicho na mashirika mengine yanayotetea haki za binadamu, usawa wa jinsia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct), wameshitushwa na kusikitishwa na mtazamo na muitikio wa serikali kuhusu shauri la Dowans.
ìLHRC itafungua shauri leo (jana) Mahakama Kuu kupinga uhalali wa tuzo iliyotolewa kwa Dowans na ICC na isisajiliwe kwa kuwa mikataba ya awali ilipatikana kwa rushwa na kukiuka maslahi ya umma,î alisema.
Kwa mujibu wa Kiwanga, mwenendo wa Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo pia unatia shaka, hususan malipo kwa Dowans.
Alisema katika suala hilo kuna mambo ya kujiuliza, yakiwemo ya kuendeshwa kwa usiri kwa shauri hilo katika Mahakama ya ICC bila wananchi kuelezwa kilichokuwa kikiendelea tofauti na kesi ya Bi-Water dhidi ya serikali, ambapo walialikwa kama marafiki wa mahakama.
ìIkiwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kwa taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyoundwa Novemba 13, 2007 kikao cha 11, mkutano wa tisa), ilithibitisha Richmond ni kampuni hewa, inawezekanaje kuwa na mkataba wa kurithisha mali zake kwa Dowans?.
ìUhalali wa kisheria wa miliki ya Dowans kwa mali za Richmond haupo, kwa nini serikali haikutaifisha mali za Richmond tangu awali?î alihoji Kiwanga.
Aliyataja mambo mengine ya kujiuliza ni ikiwa Dowans haikurithi kwa uhalali mali ya Richmond, inawezekanaje kuwa mdai halali dhidi ya serikali kuhusu mali iliyopatikana kutokana na uhalifu, na serikali kuharakisha kuilipa Dowans kuhusu mali iliyopatikana kwa uhalifu.
Kiwanga alihoji sababu za TANESCO kulazimishwa kuilipa Dowans wakati tangu awali ilishakataa kuhuishwa mkataba haramu wa Richmond kwa Dowans.
Wanaharakati hao wameitaka serikali na maofisa wa umma wanaohusika na suala hilo kuzingatia maelekezo ya Katiba na waheshimu uamuzi wa Bunge kuwa, Richmond ni kampuni hewa, hivyo kuendelea kulazimisha Dowans ni kukiuka utawala wa sheria.
Wameitaka Wizara ya Nishati na Madini kuacha kuwabebesha Watanzania mzigo wa kulipa gharama hizo kutokana na kodi wanazolipa, kwa kuwa malipo hayo yanatokana na uzembe, ubadhirifu na ufisadi.
Kwa upande wake, Dk. Sengondo Mvungi, alisema wanakwenda mahakamani ili kupata majibu ya mambo mbalimbali, huku akisema mahakama haipaswi kusajili matapeli, ila isimame iungane na wanaharakati hao na kuwataka Watanzania kujitokeza kupinga hukumu hiyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, alisema inapaswa picha za wamiliki wa Dowans ziwekwe hadharani ili Watanzania wawajue wanaolipwa fedha hizo, badala ya kutajwa majina.

Ndago tata kyara akutule, mtu gwendeghe bo isara.
 
Ndaga tata kyara akutule, ntugwendege boisala
 
Richmond ilikwenda na mtu Dowans nayo lazima iende na mtu ebo tena hii ndiyo miezi yenyewe, ukipita pale Vijana Social Hall Ilala kuna kikundi cha kina mama kinaitwa 'Tumechoka kuonewa Group' wangekuwa wanaruhusu wanaume ningejiunga nacho.

Now this is a gud one... I know this aint a laughing matter but you just made me burst out... I guess me na-qualify kujiunga na hicho kikundi.
 
Ni wakati wa wanasheria kuungana na kutoa tamko lao kupinga malipo juu ya DOWANS. Pia vyama na taasisi mbalimbali ziibane serikali kuhusu hhaya malipo
 
hivi mtu unaweza kukemea ufisadi ukiwa bado uko ccm kweli???????
kwani unapomkosoa baba au mama au ndugu yeyote ktk familia ya c lazima uihame familia hiyo nauitwe jina la ukoo mwingine? Wapinzaniwangapi wakikemea maswala kama hayo na wanambiwa kuwa ni wapinzani!!! Huoni vita vya panzi ni furaha ya kunguru???!!!!
 
watunzi wa vitabu kama Shigongo, ua watumzi wa Muvi kali kama Chilo hawawezi kututengenezea Muvi kali ya Dowans na Richmond kama walivyoigiza IDI AMINI Dada maana watauza sana mtirirko mzima mtu unaweza kutengeze Muvi kali, Hii itatusaidia kuonyesha udhaifu wa serikali awamu ya nne wa zelikali juu kushindwa kulinda watu na mali zao hadi matapeli wanachukua kama zao, itakuwa kumbukumbu mzuri jinsi wageni wanavyoitesa nchi hii
 
Kaka umesema vizuri swala ambalo wengi tunajiuliza,

Unasema mkataba ulikuwa Illegal, NI WEWE UMESEMA au ndivyo ulivyo?

Kama ulikuwa ILLegal kwa nini walienda mahakamani in the first place?
Je ICC iko biased? je anajua mkataba ulikuwa illegal?
Je watetezi wa TANESCO hawakulijua hili??

Mpaka kesi imeenda ICC,ni kuwa huo mkataba ulisainiwa kwa misingi ya kimataifa, then illegality hapa inaweza kuwa questionable, au ICC credibility might be in question!

Au mawakili wa TANESCO walikuwa so silly kiasi cha kutoweza kugundua hilo?

Mkataba ulivunjwa na bunge siyo? kwa nini TANESCO hwakuchukua zile sababu na kuziwasilisha??

Hoja ya dowans walisema ulivunjwa kwa pressure za kisiasa! could this be true?

maana tusipopata utatuzi hapa, then we have many cases ahead us in this world of globalization and every time tutakuwa tunatafutana uchawi

Bahati mbaya sina ka senk yuu kwenye mobile version nnayotumia.

Thank You.
 
hoja ya mwakyembe ya richmond kuwa fake si ndio hiyo imepigwa mweleka puuu miguu juu kichwa chini au hamjasoma hukumu aliyotum invisible. tutafute sababu zingine

Jenifa umenena, hapa JF kuna watu hutazama upande mmoja tu wa shillingi, hawatazami wa pili. Hilo ndio tatizo.
 
Dowans imekaa vibaya!!Hata JK anajuta ila halikuwa hanachakufanya kwani uchaguzi ulioisha alijua kabisa watanzania hawamtaki!hivi fikiria nguvu iliyotumika utazani ndo anaingia ikulu kwa mara yakwanza!Ile pesa iliyotumika inarudije??walijua kuna mtego wao wameweka ukilipuka wamewin lakini Imekuwa sivyo tofauti na mategemeo hivyo wanaona watanzania wamechachamaa na wao wanakuna vichwa!Mambo magumu sana!
Usidhani hawajui wanajua sana ila mazoea yamewafanya kuwa vipofu!Ukiangalia kwa makini EL hataki kuchafuka kwahili la Dowans anajua akichafuka tu yatafifia malengo yake!2015
 
Naanza kuitilia shaka credibilty ya Harrison Mwakyembe. Sababu kubwa ni kutuambia kuwa Richmond Development ni kampuni hewa, wakati tunaona wanashitakiwa huko Merekani, sasa hawa mawakili watakuwa wanaishitaki kampuni hewa? Na hawa majaji wa Merekani kutoka April Mwaka jana wanasikiliza kesi ya kampuni hewa? Hapa panaanza kunifanya nimtilie mashaka huyu Mheshimiwa?

Dowans Holdings S.A. et al v. RDEVCO, LLC

Plaintiffs: Dowans Holdings S.A. and Dowans Tanzania Limited
Defendant: RDEVCO, LLC
Case Number: 4:2010cv01086
Filed: April 2, 2010
Court: Texas Southern District Court
Office: Houston Office
County: Harris
Presiding Judge: Nancy F. Atlas
Nature of Suit: Contract - Recovery of Overpayment and Enforcement of Judgment
Cause: 28:1332
Jurisdiction: Diversity
Jury Demanded By: Plaintiff

Source: Dowans Holdings S.A. et al v. RDEVCO, LLC :: Justia Dockets & Filings
 
Back
Top Bottom